wazee wa Nyakato mpo? unakumbuka nini hasa katika shule hii? mi nilifika pale mwaka 1996, Du! nilishangaa kuona viranja wakichapa wanafunzi wenzao, kiukweli form one hakua na thamani pale{kijana}. wakati huo mzee Kalema ndio alikua mkuu sijui yuko wapi kwa sasa! mchaka mchaka wa kila asubuhi saa kumi na moja na wakati huo lazima bogi lishuke. upande wa msosi ilikua noma, asubuhi lazimu mscramble nyuka, mchana ugali maharage ambayo hajakarakaniswa, mafunda ndio usisema hadi waalimu kama akina kadasto! na hapo form one mnapigwa kwanza ndio mnapata msosi, na baada ya msosi mnakimbia nyamshongoma kuleta maji! ila taaluma ilikua poa