Tujikumbushe; Nini Kilitokea Kabla na Baada ya Mitihani ya Kidato cha Nne?

666 chata

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
1,688
3,816
Najua wengi wetu tuna expirience kubwa na tunakumbukumbu za ajabu na za kuchekesha sanaa, wakati tunaelekea kufanya mitihani ya form four enzi zile, siku za kabla ya mitihani, wakati wa mitihani na matokeo yalivyo toka;

wiki moja kabla mtihani wa kumaliza form 4 haujaanza watu walikua bize sanaa, wale wasiopenda shule enzi zile walikua wanawai mpaka namba, saa moja asubuhi form 4 wote tupo hakuna utoro na madarasa kimyaa, watu wako bize wanajisomea kuanzia notisi za form one mpaka four, kituko shuleni kwetu ilikua ni kwenye mathematics, watu walitaka kuzijua topic zote za maths. ndani ya wiki moja, mtu ambae hata log halikua hazijui ila siku hio yuko bize anataka kuzijua mpaka pythagorous, vijana waliokua Arts wao walikua wanajiona tayari wana divishen one kila mmoja, hali ilikua inatisha.
mitihani ilikua jumatatu, sasa wikiend ya kuamkia mitihani kuna watu walikua bize wanatafta pepa zilizovuja na wanapigiana simu kua kitu kimevuja, wikiend hio yalivuja matango pori mengi sanaa, watu wanapata hawaambiani, sasa jumapili jion kuna mwenzetu alikamatwa na polisi kwa makosa ya wizi na akalala jela siku tatu aliwaambia polisi wala hata hawakujali na ndio ukawa mwisho wa elimu yake hio, kwenye pepa la kwanza hio j3 maths. mtu mmoja kwenye chumba cha mtihani akapiga kelele kwa nguvu "wanangu tumekwisha pepa sio lenyewe",wasimamizi walicheka sanaa, vituko vilikua vingi ila kuna mwenzetu yeye aliumwa kuarisha ile sugu kila baada ya dk 5 anakimbia chooni watu wote walikua wana uhakika tayari ziro ya kwanza imeshapatikana, kituko kingine ilikua ni kwenye practical za biology watu walikua wanachoma nyanya kwa moto bila kuweka chemical na hakuna kinachotokea, kuna wengine walilaa bweni ile ya kujipumzisha mitihani ya saa nane wakaja kuamka mitihani imeisha, kuna wengine walichanganya ratiba wale wa day wanakuja kupiga pepa bado dk 10 mitihani kuisha.

Matokeo ndio ilikua full of saplaiz kuna vilaza wawili walipata divishen two mpaka walimu wote wakabisha, kuna wengine walifanyaga graduation kama harusi wakaita ukoo mzima, ila siku ya matokeo wapala zero, yule aliekuaga Genius sanaa alipata four moja matata hata ualimu haendi, na ituko vingi, kila mtu ana vyake sio mbaya kukumbushiana na kuelezeana ilivyokua mwisho wa siku tunafurahi tu na kusogeza siku.
 
Haya bhna ila mm sikuzote nilikuwa mchelewaji shuleni yan naenda nawakut wko assemble au darasani kabisa...Hii ilikuwa hadi kwenye paper mbili nilichelewa kuingia nikafinywa na teacher akaniombea niingie ila nilipita salama labda kwasababu nilikuwa nilikuwa miongon mwa karata turufu
 
Haya bhna ila mm sikuzote nilikuwa mchelewaji shuleni yan naenda nawakut wko assemble au darasani kabisa...Hii ilikuwa hadi kwenye paper mbili nilichelewa kuingia nikafinywa na teacher akaniombea niingie ila nilipita salama labda kwasababu nilikuwa nilikuwa miongon mwa karata turufu
sheria ilikua ukichelewa nusu saa haufanyi mtihani.
 
Sijui kwa nini sikuwahi kufikiria kama kuna kufeli mitihani,utadhani najisahihishia mwenyewe. Nimekuja kuanza kushikwa kwenye professional exams. La 7 mpaka Versity sikuwahi kuonja failure

Cha kushangaza kwenye ngazi zote hizo sikuwahi kuwa kiongozi isipokuwa time keeper nikiwa std six.
 
Back
Top Bottom