Tujikumbushe: Nahau, Misemo na Methali za Kiswahili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujikumbushe: Nahau, Misemo na Methali za Kiswahili

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Hebrew, Aug 7, 2009.

 1. Hebrew

  Hebrew JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2009
  Joined: Jul 3, 2008
  Messages: 509
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Ningependa sana kujikumbusha hizi..na sina uhahika kama bado zinafundishwa shule zetu za msingi!!

  Amevaa mawani =amelewa
  Amekula chumvi nyingi = amezeeka
  Mgaa gaa mpwa hali wali mkavu
  Kipya kinyemi ...
  Kitanda cha uvunguni sharti uiname

  Wenye kumbukumbu za Nahau, Misemo na Methali za kiswahili (hata vitendawili) naomba michango yenu

  KARIBUNI SANA!!
   
 2. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hapo mkuu umefulia... hii sio hivyo ila ni

  Mtaka cha uvunguni ...
  Ukimwona nyani mzee, amekwepa mishale mingi
  Hapa kuna wanasiasa wakongwe waliokwepa kashfa nyingi kama...
  Jungu kuu, halikosi ukoko
  Ndo maana watu wanawasikiliza sana watu wenye hekima
  Kuchamba kwingi, ...
  Uchafu ni uchafu tu.
  Ukimwiga Tembo kunya, utapasuka msamba
  Usiige mambo usiyoweza.
   
 3. k

  klf Member

  #3
  Aug 14, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ile Kamusi ya Semi za Kiswahili (watungaji Ndalu na King'ei) nimeitafsiri binfafsi kwa kimombo. Je, kuna mtu ambaye angependa kusoma tafsiri langu aone kama masahihisho lazima yafanywe au la? Kusudi langu kusambaza kazi hiyo kwa wanaotaka kuendeleza kiingereza chao.
  Huku nyuma nimeshindwa kabisa kuwasiliana na Mabwana Ndalu na King'ei. Nifanyeje?
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Aug 24, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Sokomoko: Hali ya furugu, magomvi na kutoelewana.

  Kizabizabina: Mtu mmbea, mwenye kupeleka maneno ya uchonganishi kwa watu. Hasiye na msimamo thaabiti.
   
 5. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #5
  Aug 25, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Paka mapepe havai nguo isiyofumwa
   
 6. K

  Kinnega Member

  #6
  Aug 25, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama hiyo ndio maana ya msemo huo.

  Wataalam wengine wameeleza msemo huo kumaanisha chagua moja, kujisafisha sana au nusu nusu uondoke na uchafu. Na sio ``uchafu ni uchafu tu,`` hata ukifanya usafi hausafishiki, la hasha. Sugua kadri uwezavyo.
   
 7. Companero

  Companero Platinum Member

  #7
  Aug 25, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  1. Kozi mwana mandanda kulala na njaa kupenda

  Hii mpaka leo sijui maana yake!

  2. Mwenda tezi na omo hurejea ngamani

  Hii nilielewa nilipopanda mashua Zenj!
   
 8. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #8
  Aug 25, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  MTENDA AKITENDEWA UHISI KAONEWA.
  Mkuki kwa nguruwe,kwa binadamu mchungu.
   
 9. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #9
  Aug 25, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Lila na FILA havitengamani!
   
 10. Hebrew

  Hebrew JF-Expert Member

  #10
  Aug 25, 2009
  Joined: Jul 3, 2008
  Messages: 509
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Haba na haba hujaza kibaba
  Adhabu ya kaburi aijuaye maiti
  Ganda la mua la jana chungu kaona kivuno
  Heri kufa macho kuliko kufa moyo
  Mwamba ngoma ,ngozi huivuta kwake
  Kutoa ni moyo usambe ni utajiri
   
 11. K

  Kekuye Senior Member

  #11
  Aug 25, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  1. Ana mkono wa birika
  2. Kikulacho ki nguoni mwako
  3. Aisifuye mvua, imemnyea
  4. Mkono mtupu haulambwi
  5. Paka akiondoka, panya hutawala
   
 12. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #12
  Aug 25, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Mla ni mla leo, mla jana kala nini?
   
 13. M

  Msindima JF-Expert Member

  #13
  Aug 25, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Heri nusu shari kuliko shari kamili
  Ukistaajabu ya Musa utaona ya firauni
  Kila mficha maradhi kifo kitamuumbua
  Mti mkubwa ukianguka ndege huhangaika
  Subira huvuta heri
  kila lenye mwanzo lina mwisho
  Mvumilivu hula mbivu
  Hasira hasara
   
 14. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #14
  Aug 25, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Nyingine hizi hapa:
  1. Papo kwa papo, kamba hukata jiwe
  2. Ndugu chungu, jirani mkungu
  3. Mwenye njaa hana miiko
  4. Mume wa mama ni baba
  5. Mtembezi hula miguu yake
  6. Mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba
  7. Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe
  8. Mjinga akierevuka mwerevu yupo mashakani
  9. Mchama ago hanyeli,huenda akauya papo
  10. Jino la pembe si dawa ya pengo
   
 15. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #15
  Aug 25, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usiomuone simba kanyeshewa na mvua ukadhani nyani!!!!!!!

  Hakuna marefu yasiyo na ncha.
   
 16. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #16
  Aug 25, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuchamba kwingi kuondoka na mavi
   
 17. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #17
  Aug 25, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nyepenyepe za mvua hazimzuii mgeni kwenda kwake wala mwenyeji kula chake.

  Kuchuma kwingi utachuma na mboga chungu
   
 18. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #18
  Aug 26, 2009
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kutwanga nisile unga,nazuia mchi wangu.
   
 19. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #19
  Aug 26, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Nyani haoni kundule
  Nguo ya kuazima haistiri ******
  mgaa gaa na upwa hali wali mkavu
   
 20. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #20
  Aug 26, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,391
  Likes Received: 672
  Trophy Points: 280
  Hii ganda la mua la jana chungu kaona kivuno mimi sjui inamaanisha nini,naomba mnifasirie sababu nimeiona na kuisika muda mrefu lakini sijui chungu ninani na kivuno ninini,sawa na ridhiki mafungu saba,mi nafuatisha semi tu kakini sjui maana.Nisaidieni jamani!
   
Loading...