Tujikumbushe MV Bukoba enzi za uhai wake

instanbul

JF-Expert Member
Jun 26, 2016
11,381
14,186
49084f27b80275392537b418022a96b5.jpg
f4604464002f7be1e1669c1df1b6359f.jpg

MV Bukoba ilikuwa moja ya meli kubwa katika ziwa Victoria. Ilikuwa ina uwezo wa kusafirisha watu zaidi ya 400 na tani zaidi ya 100.

Meli hii ilikuwa ikiondoka Bukoba siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa. Meli hii sio kongwe kama ilivyokuwa MV Victoria iliyojengwa mwaka 1961; hii ilijengwa mwaka 1979 lakini ilikuwa chini viwango na mbovu kuliko MV Victoria.

Meli iliua watu zaidi ya 800 siku ya Jumanne ya tarehe 21 ya mwezi wa tano mwaka 1996 eneo la Bwiru KM 30 kutoka bandari ya Mwanza.

Basi nawakaribisheni mwenye kujua chochote kuhusu meli hii au alishasafiri na meli hii au aliponea chupuchupu ajali atupe experience.

Karibuni
 
Mkuu hii meli ndo wanasemaga muwa uliizamisha si ndo hii mkuu
Sijui story huwa ni kweli? Ila Tatizo kubwa ni uchakavu wa meli,kutoboka na kuzidisha tani meli ilikuwa na uwezo wa kubeba watu 400 lakini siku hiyo ilikuwa na watu 1000 kitu ambacho sio cha kawaida wengine walikosa usafiri bandari ya bk lakini walisafiri kwa daladala had I kemondo km 13 ili wahiwahi wengine wangine wanahusisha ajali na mjini ya ziwani na uchawi
 
Hii inafanana na Mv. Mwongozo la Lake Tanganyika
 
Back
Top Bottom