instanbul
JF-Expert Member
- Jun 26, 2016
- 11,381
- 14,186
MV Bukoba ilikuwa moja ya meli kubwa katika ziwa Victoria. Ilikuwa ina uwezo wa kusafirisha watu zaidi ya 400 na tani zaidi ya 100.
Meli hii ilikuwa ikiondoka Bukoba siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa. Meli hii sio kongwe kama ilivyokuwa MV Victoria iliyojengwa mwaka 1961; hii ilijengwa mwaka 1979 lakini ilikuwa chini viwango na mbovu kuliko MV Victoria.
Meli iliua watu zaidi ya 800 siku ya Jumanne ya tarehe 21 ya mwezi wa tano mwaka 1996 eneo la Bwiru KM 30 kutoka bandari ya Mwanza.
Basi nawakaribisheni mwenye kujua chochote kuhusu meli hii au alishasafiri na meli hii au aliponea chupuchupu ajali atupe experience.
Karibuni