Tujikumbushe "MSAZENGO" Mazengo and Msalato Secondary. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujikumbushe "MSAZENGO" Mazengo and Msalato Secondary.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Sikonge, Dec 4, 2008.

 1. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2008
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kwa wale mliwahi kusoma Kikuyu na kuacha watoto wenu pale Kikuyu na vile Vibinti VIKUYU basi jikumbusheni shule yenu. Bahati mbaya kwa sasa haipo tena maana kimekuwa Chuo kikuu cha Wa-Anglican. I wish ningeinunua tena na kuwapa Wa-Anglican eneo jingine na kuirudisha Mazengo yangu.
  Mie nilikuwepo hapo mwaka 1982-1985. Enzi tunatesa sana kwenye timu ya Mpira wa miguu (akina Black Madonna, Kalonga, Mtutwa, Jabili Kasenga, Pocent Moyo, Kondo, Hanzuruni ...). Kwenye mbio kijana Shahanga alikuwa akizunguka watu sijui mara ngapi. Mpira wa vikapu alikuwepo yule Mkurya aliyenifanya nisicheze huo mchezo kwani nilijua milele sintafikia level yake, jamaa alikuwa akiitwa Sammy Marwa. Nilikuja muona Dar kanenepa sikuamini. Kijana Pius Moremi (kijana wa Stretoz), Kindaza wa bweni la ujamaa (Ex-Tabora JAzz) na gitaa lake........
  Msalato alikuwepo Mama Nanofu, Halima Msomali.... haya watoto wa Six leteni story zaidi.
  Ukitaka kuangalia picha za Mazengo:-
  The Buildings
  mazengo secondary picture - Google Image Search

  Kwenye mpira nakumbuka mwaka 1984 tulikuwa tukicheza UMISETA, basi timu za Dodoma za Secondary zilipata sana shida. Tulikuwa tukienda shangilia mechi tunasubiri goli la Saba (wiki). Likifungwa tunaondoka. Siku tulikaa hadi mwisho ni pale Mpwapwa walipotugomea kufungwa wiki, tukawafunga sijui goli 5, basi Mazengo ilikuwa huzuni saaaaana na Mpwapwa ilikuwa furaha kubwa.
   
 2. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Basi mlipotoka tuu nyie sisi Mpwapwa tukawapiga mazengo goli 8 Kibuyu ila nyie kwenye Drama mkatoa best actor na Msalato wakatoa best actress.
   
 3. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Hivi kalonga yuko wapi siku hizi?
   
 4. Ngonalugali

  Ngonalugali JF-Expert Member

  #4
  Dec 5, 2008
  Joined: Jan 12, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Jamani wengine tulitumwa na vijiji kusoma kwa hiyo ilikuwa ngumu sana kufika Msalato. Nakumbuka Msalato nilipita nikiwa naelekea Veyula. Ila kwnye suala la futiboli bana hapo ndo tulikuwa tunavunja miguu yetu.

  Kuna jamaa mmoja wa DomSec nimekutana naye kwenye mahangaiko ya kikazi na baada ya kutambulishana kwa kina alitamani alipize kisasi maana anakumbuka walifungwa na kichapo wakapata.

  Jamani ilikuwa foolish age na si kingine.

  Ila hata mimi kuna jamaa namtafuta aniombe radhi maana alitaka kunidhalilisha kwa adhabu ya unyoya.

  Picha hizo zimenikumbusha mbali sana!!! Natamani siku moja nitembelee pale. Kuna siku nilikutana na Ishengoma akaniambia kwa sasa wanaendeleza libeneke Kikuyu day!!!!!!!!

  Sina uhakika kama ndoa ya MSAZENGO bado ipo.
   
 5. N

  Nyani New Member

  #5
  Dec 5, 2008
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  naskukuru sana kwa kukumbushia Msazengo, tena nasikia HEADMASTER wetu mtanashati Mzee Mkoba alifariki dunia, je mnahabari?
   
 6. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #6
  Dec 5, 2008
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Majita,
  Inawezekana kuwa mliwafunga ila si mengi namna hiyo. Siku zote kulikuwa na jamaa wengi wanaoupiga mpira vizuri. Na ni kweli mwaka wetu ulikuwa na wachezaji wengi sana na wazuri. Hata kwenye mashindano ya FORMS, walituonea tu mwaka wa kwanza. Jamaa wakawa "wanakula miwa" ya vijana wetu akina Feruz Hanzuruni. Mwaka wa pili tukatesa hadi tunamaliza. Mwaka wetu ulikuwa unatoa wachezaji wengi kishule, kimkoa na hadi kanda. Nakumbuka mwaka 1985 kama sikosei, mashindano yaliyofanyikia Arusha (umiseta Taifa), kanda ya kati walishinda. Kuna huyu jamaa tuliyekuwa tunamwita (Black Madonna) kwa jina hasa Musa zuberi tulikuwa tunasema anatanguliza mpira mbele, akikimbia humkamati. Akishaufikia mpira basi hilo shuti lake tukawa tunaita RADI. Bahati mbaya aliumia na kuanza kutibiwa (operation) ila kwa matibabu ya pale Dodoma, nafikiri ndiyo ukawa mwisho wake. Sijui aliishia wapi.
  Mpwapwa mlikuwa na Golkipa mzuri sana. Bila huyu na nyie mgelichukua WIKI. Tishio letu siku zote lilikuwa ni Centrum, hasa enzi hizo wakiwa na yule golkipa wao machachari na mbele Mzee mwenyewe "Adolf Kondo". Ila nao mwishoni walikubali na wakanywa wiki.
   
 7. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #7
  Dec 5, 2008
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Gembe,
  Huyu jamaa nilisoma naye darasa moja. Tulikuwa wote kwenye masomo ya ujenzi (Plumbing and Brickwork). Kilivyokuwa na mwili mdogo huwezi kuamini kuwa ni ki-beck kizuri. Kikizidiwa nguvu kina tumia "Hand Break" yaani kinakamata shati. Ila kukamata shati mzinga wa mtu kama alivyokuwa yule Mnyakyusa "Mapilau?" au mtu wa Chenga za maudhi "Jabir Kasenga" inakuwa ni shida sana. Ila ukimpita huyo unamkuta Athman Mtoro, hapo huendi popote.
  Kalonga Jumapili mwishoni nilisikia alikuwa wizara ya mambo ya ndani kwenye kitengo cha Passport. Nasikia alikuwa kanenepa wala huwezi amini. Mie tangu tumalize hapo hadi leo sijawahi muona.

  NYANI :- Mkoba pana wakati walimu wakuu walikuwa na mkutano pale Arusha Tech. na akaja. Tukafanya kimkutano cha harakaharaka na akaja kutuona vijana wake wa Mazengo. Akatupa hongera kwa kufaulu na kututakia kila la kheri. Baadaye akaenda kuwa Mkurugenzi wizarani na mwisho nikasikia kuwa amefariki dunia. Nitamkumbuka kwa maneno "... Mwenzenu Map***** yameoza..." na ile ya "...You come here alone and you will go home alone.."
  RIP Mkoba.
   
 8. k

  kwemwale Member

  #8
  Jul 22, 2013
  Joined: Mar 2, 2013
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu Sikonge.

  Habari za siku?

  Hivi Shule ya Mazengo ilihamia wapi? kuna jamaa yangu alimaliza pale miaka ya 90's na haja chukua cheti chake kwa kuwa alikuw nje ya nchi. Kurudi akaambiwa kuwa Shule imekuwa Chuo kikuu na anataka afuatilie cheti chake. Unamshauri aende wapi?.
   
 9. wijei

  wijei JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2013
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  aende dodoma sekondari vyeti vyote viko pale.
   
 10. MKOBA2011

  MKOBA2011 Senior Member

  #10
  Jul 22, 2013
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 143
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Baada ya kutoka Mazengo Mkoba alikuwa wizara ya elimu na utamaduni kama kamishina wa elimu Tanzania then akaenda SUA kuwa REGISTRAR ambapo alifariki akiwa pale SUA bad enough baada ya mwaka mke wake nae akafariki pale SUA kuna mtoto wake bi Daktari hospitali ya Mazimbu.
   
 11. G

  Galapagos JF-Expert Member

  #11
  May 16, 2014
  Joined: Nov 26, 2012
  Messages: 253
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Dah, hii ni kumbu kumbu nzuri sana mkuu, me nimeingia hapo Complex "96 nikakuta jamaa (Mkoba) ndo anaaga akaingia Kazimoto Msasa, RIP
   
Loading...