Tujikumbushe: "Mimi naitwa Paul Makonda kama jina langu lilivyo"

Andrew Mushi

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
630
696
Leo ni siku ya kuongea na kurudia matamko ya Mkuu wetu wa Mkoa na Mh Rais ktk ujenzi wa taifa letu, katika sehemu ya utendaji kazi, wasifu wa Mh Paul Makonda na uwajibikaji

Mimi naitwa Paul Makonda kama jina langu lilivyo, maneno hayo aliyasema wakati akihojiwa na Bi. Salma ktk kipindi cha Mkasi, alipoulizwa
"Wewe ni nani na unafanya shughuli gani?"
2ec5a47037b52488bbcb02baf0ce350e.jpg

Ktk sehemu ya utendaji kazi wa Mh Paul Makonda kama Mkuu wa Mkoa ktk kusimamia uwajibikaji ktk serikali za mitaa..
Makonda - "Wenyeviti wa mitaa mumepewa jukumu la kusimamia sheria"

Maneno hayo aliongea Mkuu wa mkoa Mh Paul Makonda alipokuwa ziarani Na kufanya vikao vya hadhara ktk moja ya kata na vitongoji vya Dar

Mh Paul M, alishurutisha mwenyekiti huyo wa Mtaa apelekwe rumande, baada ya kubainika na mahakama ya hadhara kuwa ni mbadhilifu wa mali ya wanakata..

26e56fbb92cfd380150c8b790c62145e.jpg


VIJANA KUKOSA AJIRA.

Vile vile alipokua akihojiwa Na kuulizwa swali ktk kipindi cha Mkasi, kuhusiana na malalamiko ya vijana wengi kukosa ajira..

Makonda - "Mimi kwa bahati mbaya ni mwanasiasa nina majibu mengi"

KUHUSU KATIBA ILIYOPENDEKEZWA NA MAREKEBISHO YAKE KTK BUNGE LA KATIBA

Ktk maelezo yake kuitolea tafsiri ya ibara ya 6 ya katiba mpya,

Mh Paul Makonda anaelezea na kusema - "mtu yeyote akayeingia kwenye Ofisi ya umma, azingatie yafuatayo :-...

Uwazi..., uwajibikaji,... ushirikishwaji..., utu.. na uadilifu...."

WASIFU WA MAKONDA


Mama Suzan akielezea wasifu wa Paul Makonda ktk kipindi cha Zamaradi

Mama Suzan - "Paul Makonda alizaliwa tar 15/02/1982 ktk kijiji cha kolomije, Mkoa wa Mwanza wakati wa majira ya saa 1:30
asubuhi ktk zahanati ya kolomije"

Mama Suzan aliendelea na kusema - "alianza shule ya msingi kolomije, baadae alikwenda sekondari, na baadae chuo kwa sababu unasema kwa ufupi, siwezi kutaja mwaka baada ya mwaka, na wakati fulani naweza kusahau sahau."

Vile vile Mh Paul aliwahi kuongelea wasifu wake wakati yuko Mwanza, na kuongea yafuatayo,

Mwaka 2001-2002 -mchimba mchanga na Mkata Mkaa

Mwaka 2099?? - tingo wa kubeba Magunia ya watu, ktk jitihada zake kutaka kupanda cheo kuwa kondakta

7c8f5c338e0b9806cc5acbf958d88f80.jpg



KUMALIZIA MH RAIS KUTOLEA MAJIPU

Mh Magufuli, alipotumbua jipu la Mkurugenzi wa jiji Dar wa kipindi hicho, Marehemu Kabwe, alisema haya yafuatayo baada ya Mh Makonda kutolea maelezo ya ufupi kuhusiana na kutokuwajibika kwa Mkuregenzi huyo..

"pakitokea jipu, sitasubiri, kwa sababu nikisubiri litaota usaha...."

Hatma yake alimuachisha kazi Mkurugenzi wa jiji pale jukwaani..

Kauli ya Rais Magufuli kuhusu vyeti feki, alisema haya

".... yule mwenye vyeti vya forgery ataondolewa kwenye nafasi yake, wewe uliyesema umemaliza darasa la saba unabaki
na kazi yako... hatutaki tuwe na viongozi, wewe unasema uko la saba kumbe bosi wako darasa la pili.... Na kila siku unaenda unasema shikamoo bosi, alitakiwa wewe akupe shikamoo.."

Naomba na wachangiaji wengine watoe, mchango wao kuhifadhi haya maneno na matamko mengine ya viongozi wetu, na vile vile kutoa tafsiri ya uzito wa maneno haya na mengine..

Tushikamane na viongozi wetu ktk ujenzi wa nchi yetu na kuondoa rushwa, ubadhirifu wa mali na tuwe pamoja ktk vita ya kupambana na mapapa ya wauza unga.
 
mimi nampenda sana makonda jinsi anavyojituma..

ila nimeanza kutokuwa na imani nae.. naanza kuhisi kweli hana elimu halali... clip ya clouds na mapolisi na wanajeshi imenitisha

msomi wa ukweli hawezi fanya ule uzembe.. hata kugundua kuwa kuna cctv maofisin kote alishindwa kweli
 
Kila mwenye macho haambiwi tazama, mwenye akili basi aitumie na kila mwenye mdomo basi ale matapishi yake.

Na wengine daraja ya mimi na wewe tunachokiganga na kukihitaji nimuongozo, basi muongozo huo tushikamane nao.

Tusichanganyane hapo kati.


Nawakilisha!
 
mimi nampenda sana makonda jinsi anavyojituma..

ila nimeanza kutokuwa na imani nae.. naanza kuhisi kweli hana elimu halali... clip ya clouds na mapolisi na wanajeshi imenitisha

msomi wa ukweli hawezi fanya ule uzembe.. hata kugundua kuwa kuna cctv maofisin kote alishindwa kweli
Hivi unayo Mkuu hiyo clip....
 
mimi nampenda sana makonda jinsi anavyojituma..

ila nimeanza kutokuwa na imani nae.. naanza kuhisi kweli hana elimu halali... clip ya clouds na mapolisi na wanajeshi imenitisha

msomi wa ukweli hawezi fanya ule uzembe.. hata kugundua kuwa kuna cctv maofisin kote alishindwa kweli

Hii kitu Inaitwa "it gets into your head", sort off attitude, kumbuka

Kwa kauli ya Makonda, kumbuka alisema haya
Baba yake alikua jeshini, na alimaliza la kwanza au la pili tu, kama hajakosoea, na huyo alishikishwa silaha.

Sasa imagine vyombo vya jeshi na silaha ndani ya chombo cha habari, it means one thing, kufanya mapinduzi ya muono wa mawazo ya mwenye kutangaza habari, au fanya na kusema unachoshurutishwa kusema.

Au kuna definition nyengine, labda kikosi kile, kimeenda kufanya rehearsal ya utoaji habari.
 
Back
Top Bottom