zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 19,039
- 28,688
Habari za jioni wakuu moja kwa moja niende kwenye mada husika za kukumbushana kuhusu watu wa kale waliofanya makubwa leo ningependa tumgusie Nimrod aliyetawala Babylon ya kale huko mashariki ya kati. Kwa ufalme wa sumeria alifahamika kwa jina la Mfalme Enmer-kar alipata kuishi hapa duniani takribani miaka 5000 iliopita.
Kwa tafsiri za biblia na maandiko ya kiislam na kiyahudi (dini kuu 3 za mashariki ya kati) Nimrod alikuwa kitukuu wa Nuhu na mjukuu wa Ham...
Mwanzo 10
8 Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi.
9 Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za BWANA. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za BWANA.
10 Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari.
11 Akatoka katika nchi ile akaenda mpaka Ashuru, akajenga Ninawi, na Rehoboth-iri, na Kala;
12 na Reseni, kati ya Ninawi na Kala, nao ni mji mkubwa.
UMAARUFU WAKE
1.Inaelezwa kwenye simulizi za kale kuwa mfalme Nimrod/enmer kar baada ya kusimuliwa kuwa mababu zake waliuawa na YHWH/MUNGU/ALLAH kwenye gharika kuu, aliamua kujenga mnara mkubwa ili kumfikia Mungu ili aweze kulipa kisasi kwa "unyama" waliofanyiwa mababu zake. Simulizi zinaeleza aliweza kukusanya watu wengi wa ulimwengu takribani laki 7 na kwakuwa alikuwa mfalme wa himaya kubwa na ya kwanza duniani aliweza kuwakusanya wengi kumfanyia hiyo kazi ya kujenga mnara wa kumfikia Mungu. Mradi huo wa kujenga mnara huo wenye umbo kama pyramid za misri kuanzia ramani kuchorwa,vifaa kuungwa na mnara kukamilika kwa 80% ulichukia takribani miaka 20 hatimaye Mungu alipoona Nia yao ni ovu akawachanganya lugha na baadae kuleta tetemeko lilioangusha mnara huo
NB: Mnara haukuwa wa kumfikia Mungu kimwili yaani mawinguni bali ilikuwa ni kufanya matambiko ya kutengeneza kma GETI la kiroho kuwapeleka mbinguni na simulizi zinasema walipoona GETI hilo limetokea wakaanza kurusha mishale ambayo haikuzaa matunda na baada ya hapo wakatawanywa
Mfano wa mnara wa babeli ulivyokuwa
2. Nimrod anaelezwa kwamba ndio mfalme wa Kwanza hapa Duniani na alikuwa ndio wa kwanza kujenga Himaya duniani yaani babeli/sumerian empire... Inaelezwa mifumo mingi ya ujenzi,vita,utawala,jeshi,serikali n.k vilianzia kwake hivyo alikuwa na ushawishi sana kiasi kwamba alitawala koo zote za shem ham na japhet na hata mataifa mengi kutoka pande zote za dunia kufuatana na kitabu cha Jasher walikuwa wanakuja babeli kumuinamia!!!
3. Inaelezwa pia ndio alijenga jiji la kwanza duniani ambao ulikuwa mji mkubwa sana Babylon/babeli... Miji mikubwa na maarufu kwenye historia ya biblia kama shinar,babeli,Ninawi na ashuru na yote ilijengwa na Nimrod huko mashariki ya kati hii pia ilimjengea umaarufu sana nimrod.
4. Kufuatana na kitabu cha jasher zile familia tatu yaani shem japhet na ham ziliingia kwenye vita kubwa sana na Nimrod aliongoza majeshi ya familia ya HAM na kuwatandika ndugu zao hao na toka siku hiyo akawaweka chini ya utawala wake hili pia lilimpa umaarufu sana Nimrod kipindi chake.
5. Ikumbukwe baada ya gharika wanadamu wote yaani familia ya Nuhu na vizazi vyake walikuwa wakimuabudu MUNGU/ALLAH ila alipokuja Nimrod ndio akarudisha ibada za masanamu,matambiko,uchawi hivyo hii dini yake ambayo sanamu lake ndio liliabudiwa nalo ilimpa umaarufu na alipata wafuasi wengi sana maana ndio alileta dini ya kwanza kabisa baada ya gharika tofauti na ile ya asili ya kumuabudu Mungu pekee.
FREEMASONRY
Nimrod pia anahusishwa na kuweka misingi ya Freemasonry na kuna baadhi ya lodge na baadhi vitabu na majarida yao wanamtambua Kama Grand master wao wa kwanza kabisa..... Hata leo hii ukiwa mwanachama wa Freemasons kwenye baadhi ya lodge inatakiwa ule kiapo kwa Nimrod inaitwa NIMROD's OATH..... Pia miongozo,sheria,viapo,taratibu nyingi za freemasons wamezicopy kutoka kwa chama cha kwanza cha giza (secret society)alichokianzisha nimrod cha wajenzi wa mji wa NINAWI, hivyo yote yanayofanywa na freemasons leo na dini zote za kipagani misingi yake iliwekwa na Nimrod
ALIPATAJE USHAWISHI
Simulizi za vitabu kadhaa hasa Book of jasher (kinatambuliwa na baadhi ya waandishi wa biblia) vinaeleza alipata hizo nguvu kutoka Vazi ambalo Mungu alimfanyia Adam kipindi alipojiona yupo uchi baada ya dhambi ya bustani ya edeni.
Mwanzo 3
21 BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika
Vazi lile alimrithisha mwanaye - Seth naye likazunguka hadi kufikia kwa nuhu ila Ham aliiba vazi hilo kutoka kwenye safina na likarithishwa kwa cush ambaye alikuwa mwanaye wa kwanza naye akamrithisha Nimrod. Ukisoma the first book of adam and eve,adam alionyesha hofu alipotimuliwa bustanini kuwa Wanyama wakali watamla ila Mungu alimwambia hilo vazi litamlinda na wanyama wote wakali yaani wakimuona tu wanamuinamia na hii ilimfanya Nimrod pia kutetemekewa na wanyama kila alipowaona na ndio maana biblia inasema;
mwanzo 10:9
Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za BWANA. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za BWANA.
Pia inadaiwa uwezo huu wa wanyama kumuogopa ulifanya hata wanadamu wa kawaida wampe heshima ya UUNGU fulani bila kujua siri ya nguvu zake..... Hivyo alipata nguvu za ajabu za kuwatawala watu na kujenga ushawishi sana enzi zake.
ANGUKO LAKE
Kulingana na kitabu cha jasher baada ya maasi kuzidi sababu yake Mungu alikasirishwa sana na siku moja Nimrod akiwa amelala aliota ndoto kuwa utawala wake utaangushwa na mtoto anayekuja kuzaliwa..... Sio miaka mingi akazaliwa abraham na wataalam wa nyota na elimu ya kiroho wa utawala wake walimuambia kuwa huyu abraham ndio atakayekuja kufuta ufalme wake.
Story ni ndefu kidogo ila abraham alitoroshwa mapangoni alafu baba yake akaleta mtoto feki akauawa wakijua ni abraham ila bado kwa miaka 50 nimrod alikuwa anamuota huyo mtoto kuwa anamkata kichwa mwisho wa siku akashtuka lazma abraham hajafa.... Akasakwa na akakamatwa na akatupwa kwenye tanuru la moto ila bado hakuungua ikabidi nimrod amuachie kwa kuhamaki na watu wengi wakamfuata abraham na wakaona wazi nimrod ameshapata bingwa wake!!! Ushawishi tokea hapo ukaanza kuporomoka na miji iliokuwa chini yake kama ELAM ikaanza uasi chini ya mfalme Kedorlaoma aliyemtandika Nimrod na kumuweka chini yake... Mwishoni unabii ulikuja kutimia kwa nimrod kuangushwa na mtu wa kutoka uzao wa abraham yaani mjukuu wake alieitwa Esau.
KIFO CHAKE
Simulizi kadhaa za hadith,tafseer za kiislamu kama tabari II zinaeleza baada ya kumtupa Abraham kwenye tanuru la moto anashangaa kumuona Ametoka akiwa mzima bila kovu na ndio hapo ubishani ukaanza na kejeli kwa Mungu wa Abraham maana Nimrod alidai yeye ana ubavu kuliko huyo Mungu wa Abraham na ndipo zikatokea MBU zikaanza kuwala wale walinzi na Nimrod mwenyewe maana mbu wale walipenya maskioni puani na mdomoni na kumfanya nimrod ajipigize kichwa huku na kule hadi kufariki
Nadharia ya pili kutoka book of jasher inaeleza Nimrod aliuawa na Esau mwana wa Isaka alipokuwa akiwinda ili amuibie VAZI lake la maajabu na inadaiwa baada ya mpambano huu mkali esau akiwa amechoka sana ndipo alipodai chakula kwa yakobo hadi akaishia kuuza haki zake za uzaliwa wa kwanza
Nadharia ya tatu inaeleza baada ya kuona nimrod anaeneza upagani na dini yake ya kishetani... Shem mwana wa Nuhu anapatwa jazba na anaunda umoja na maadui 72 wa Nimrod wanakwenda kuvamia kasri lake na wanamteka kisa wanamkata vipande vipande na wakamzungusha kwenye miji yote aliyotawala kuwaonyesha kuwa Nimrod hakuwa mungu ila mwanadamu tu.
UTATA
Inaelezwa kwenye vitabu mbalimbali vya kishitoria nilivopata kusoma kuwa Nimrod alimuoa Mama yake baada ya baba yake ''kustaafu''uongozi , mke huyo alifahamika kama semiramis ila kiebrania alifahamika kama Shinar kwenye biblia yaani jina ambalo ndio inaelezwa kama Mji alioishi Nimrod.... Huyu mama naye alikuwa sio wa mchezo mchezo wajuaji wa mambo humu wanamfaham sana ila itabidi afunguliwe uzi wake siku nyingine na kwenye biblia anatambulika kma MALKIA WA MBINGU soma Yeremia 7:18
HITIMISHO
Mengi yamesemwa kuhusu mfalme huyu ningependa wajuaji wa mambo pia mtuongezee mbili tatu mnazofahamu kuhusu nguli huyu ili tuzidi kujifunza kuhusu nature ya wanadamu tulipotoka na tunapokwenda..... naomba kuwasilisha
Cc wanajukwa wotee