Kiswahili: Methali, Vitendawili, nahau, Misemo n.k

Hicho mkuu ni kitendawili jawabu lake KISIMA
Lakini muuza ugoro nafikiri ukitoa msamiati usimalize ili mdau ajibu
Mfano Mficha uchi.....? baadae jawabu HAZAI.
Sasa na mimi natuma vya kwangu
Kitendawili..?
1. kuku wangu kalalia mibani? ......

Methali:
Mwenda tezi na omo?..............
 
Najibu:
Mwenda tezi na omo_ marudio ngamani.

Kuku wangu kalalia mibani...Nanasi!

Malizia methali: dunia hadaa .....
 
Simba mwenda pole...iko gonjwa kama si gonjwa basi ******* :)
Mtaka cha uvunguni...Pindua tanda taona :)
Asiyesikia la Mkuu...chapa yeye :)
 
Umepata
Najibu
Dunia hadaa - Ulimwengu shujaa.

Tunaendelea

Kitendawili: Hogo haliogoki ila kwa hogo lenzake....

Methali: 1. Baniani mbaya .............
2. Hamna hamna..............
 
Niaje Great thinkers? Munaonaje tukajikumbusha methali, nahau n.k coz nina hofu zinaanza kutoweka gradually!
Kwa kuanzia natoa methali híi:
Kombe la mungu liwazi.
Nasubiri majibu wakuu!
Then, kama unazo basi lets share.

The bark of yesterday sugar-cane is like a whole harvest for an ant.
 
tumbi tumbi...............
mm nyumba ya udongo.......................
chanda chema........................
 
Hicho mkuu ni kitendawili jawabu lake KISIMA
Lakini muuza ugoro nafikiri ukitoa msamiati usimalize ili mdau ajibu
Mfano Mficha uchi.....? baadae jawabu HAZAI.
Sasa na mimi natuma vya kwangu
Kitendawili..?
1. kuku wangu kalalia mibani? ......

Methali:
Mwenda tezi na omo?..............

Kama ameenda na tez na homo basi aje achukue na sabuni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom