Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 6,860
- 12,291
Habari zenu ndugu zangu. Baada ya kuwajulia hali, ningepeenda niende moja kwa moja kwenye mada iliyonileta hapa. Bila shaka asilimia kubwa ya vijana tuliozaliwa na kukulia Dar es Salaam miaka ya 90, tuliwahi kucheza au kupitia michezo mbali mbali kama vile karate, ngumi, soka (mpira) na michezo mingine mbali mbali. Katika aina hizi za michezo, mi niliwahi kujifunza michezo miwili ambayo ni ngumi na soka.
Nikiwa na umri wa miaka 12 Tu, nlijifunza ngumi kupitia kwa baba angu mdogo ambae alikuwa anaishi Tabata makuburi kama unaenda kule ilipokuwa kambi ya jeshi zamani (sina uhakika kama kambi hiyo bado ipo mpaka Leo). Bamdogo alikuwa anapenda ngumi kwahiyo enzi za utoto wake alitumia muda wake mwingi kujifunza mchezo huo kupitia wataalam mbali mbali. Japo hakufanikiwa kufika mbali kutokana na changamoto za maisha, lkn aliamua kuutumia ujuzi huo wa kurusha madongo kuwagawia na wengine ambao walikuwa na lengo la kujilinda na vibaka wa mitaani (waliozaliwa na kukulia bongo miaka hiyo, nadhani wanafaham vizuri hali ya usalama ilivyokuwa mitaani).
Baada ya mimi kujifunza na kuujua mchezo huo na baadae kupambanishwa na watu mbali mbali ambao wapo walionipiga (asiekubali kushindwa, sio mshindani) na niliowachapa kweli kweli. Baadae pia nikajielekeza kwenye mchezo wa soka. Huku nilichezea timu mbali mbali, lkn nilichezea zaidi timu mbili za mtaani. Kwanza nilichezea timu moja ya mtaani iliyoitwa YOUNG KIDS ambapo tuliwahi kufika fainali mara tano, ila tukabeba kombe mara mbili.
Kombe la kwanza lilikuwa la jogoo wawili, na kombe la pili lilikuwa la jogoo mmoja.. bata mmoja na njiwa wawili. Baadae nilichezea timu nyingine ya mtaa ila mbali kidogo na maskani ya timu ya YOUNG KIDS FC. Timu hii ya pili iliitwa SUPER INTER SPORT CLUB. Nikiwa captain wa timu huku nikicheza namba 6 uwanjani, nikishirikiana na wachezaji wenzangu wenye bidii uwanjani, tulifanikiwa kuiingiza timu yetu fainali mara 8 na kubeba makombe manne.
Tumebeba makombe ya mbuzi mara 2, na makombe ya kawaida aina kama silver pia mara mbili. Ila pia pamoja na uwezo mkubwa wa kusakata kabumbu uwanjani, lkn kuna mechi zingine tulikuwa tunapoteza katika round za mwanzo mwanzo kutokana na makosa madogo madogo ya hapa na pale.
Hii ni baadhi ya michezo iliyokuwa inapendwa sana jijini Dar es Salaam miaka ya 90. Kama kuna mungine ambae aliwahi kupitia mchezo fulani na kuleta au kupata mafanikio kutokana na mchezo au michezo hiyo, anakaribishwa kuchangia uzi huu.
Asanteni sana.