Tujikumbushe marufuku ya hayati Abeid Aman Karume visiwani Zanzibar?

Wang Shu

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
2,563
3,708
Mchezo wa Masubwi (ndondi) ni moja kati ya michezo mikubwa na yenye umaarufu mkubwa dunia kote, lakini mchezo huu ni marufuku kuchezwa katika visiwani Zanzibar.

Je ni kwanini? mchezo huu haurusiwi kuchezwa katika visiwa hivyo vya Marashi ya karafuu.

Jibu la Swali hili ni la kihistoria, katazo la kutopigana kwa vijana wa kizanzibar lilitolewa na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Aman Karume, baada ya visiwa hivyo kujitawala baada ya mapinduzi wa mwaka 1964.

Abeid Aman Karume, ndie aliyetoa kauli ya kukataza kuchezwa ngumi baada ya kualikwa kwenye pambano la masumbwi ambalo liliandaliwa na raia mmoja wa Ghana.

Alipofika katika eneo hilo ndipo mzee Karume alipotoa kauli ya marufuku kuchezwa masumbwi.

Alipofika pale aliangalia na kuuliza kwanini wanataka kupigana?

Alipoambiwa ni mchezo wa ndondi akasema mwisho leo, kwa vijana wa Kizanzibar - 'kupigana masumbwi ni kufanywa kama watumwa.

Historia inaeleza zaidi kuwa hayati Karume alifikia uamuzi pia kwa kuzingatia historia ya namna Visiwa vya Zanzibar vilivyopata Uhuru wake kwa mapinduzi, hivyo kuhusisha kupigana huko kuwa sawa na kuendelea kuwa chini ya wakoloni.

"Katika sera ya michezo mzee Karume alisema tufanye michezo ambayo ni mizuri na yenye maadili, michezo yoyote yenye madhara na sisi na madhara yanayoonekana na yasiyooneka, michezo hiyo tusiicheze na tuipige marufuku".

Maamuzi haya ya miaka mingi ni sukari chungu kwa mabondia wengi walioko Visiwani Zanzibar, mabondia wanaruhusiwa kufanya mazoezi tu lakini kupigana ni aidha wapigane Tanzania bara au nje ya nchi.
 
Katika sera ya michezo mzee Karume alisema tufanye michezo ambayo ni mizuri na yenye maadili, michezo yoyote yenye madhara na sisi na madhara yanayoonekana na yasiyooneka, michezo hiyo tusiicheze na tuipige marufuku".


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alipiga marufuku mashindano ya ulimbwende kwa madai wanawake wa kizanzibari wote ni warembo.
 
ila tuache utani,burudani ya ngumi zozote huwa siioni zaidi ya kutizama movie.watu wanavimbishana mimi nafurahi
 
Wanawake wote ni warembo.
Haya mashindano kwa upande wangu naona yanamdhalilisha zaidi mwanamke kwa kumuanika akiwa anatembea uchi mbele ya jamii.

Wanatembeani uchi wakati wanakuwa wamevaa chupi.

Isitoshe hata jamii za kale walikuwa wanavaa mavaz ya kuziba sehemu za siri tu na maisha yanaendelea.
 
Back
Top Bottom