TUJIKUMBUSHE: Mafisadi EPA waruka kiunzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TUJIKUMBUSHE: Mafisadi EPA waruka kiunzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Halisi, Sep 3, 2008.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  SOURCE: Mtanzania 14.05.2008

  http://www.newhabari.com/mtanzania/habari.php?id=4929&section=kitaifa


  http://www.newhabari.com/mtanzania/habari.php?id=4929&section=kitaifa
   
 2. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Niliweka hii habari kwa makusudi mazima ili watu wajue kwamba alichosema JK si bahati mbaya ni mkakati ulioandaliwa na wahusika kuhakikisha wanapotosha maana halisi ya Sheria ya Fedha Haramu na Sheria nyingine za makosa ya jinai.

  Maana ya sheria ya fedha haramu ina maana kwamba kuna uharamu na kunapokuwa na uharamu, huwezi kusema unarudisha fedha na watu waendelee kupeta.

  KUna habari nimeisikia kwamba Prof. Costa Mahalu, kupitia wanasheria wake kina Alex Mgongolwa na wenzake, wanakusudia kuwasilisha mahakamani maombi ya kutaka apewe muda wa kulipa na kesi ifutwe, wakidai kwamba hata kama hahusiki na upotevu huo, basi badala ya kuhangaika na mahakama, apewe muda wa kulipa hizo fedha na kesi ifutwe kwa kuwa kuna "Presidential Order" kuhusiana na kesi zinazofanana na hizo.

  Huyo ni Mahalu, lakini kuna wanaotaka hata magereza yote wafungwa wa wizi wapewe muda wa kulipa na waachiwe wote
   
 3. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hawa viongozi wetu wanaf****. Huwezi kuamini ujinga huu unafanywa na viongozi walio chaguliwa kwa kura za wananchi.

  Hivi tunashindwa nini kuwawajibisha 2010?
   
 4. M

  Masatu JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mtanzania,

  Pole sana naoina unaandika kwa uchungu mkubwa. Kuna msemo unasema "inaanza na wewe" sasa waonaje ukafungasha huko uliko na kuingia uwanjani. Mie ntakuwa kampeni meneja wako teh tehe tehe
   
 5. M

  M$awa Member

  #5
  Sep 3, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Haya ndio Mambo ya " Plutocracy " Thats why Mwalimu JKN was very pessimistic na

  ku-unleash "Capitalism" Socialism [and] (Failed Azimio la Arusha) was bad since it denies citizens to own property and accumulate wealth but its opposite Plutocracy is Worse ! It denies (Democracy) and rule of people ! How to strike a balance its the tricky part !
   
 6. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Masatu,

  Mimi nimeanza kufunga mizigo, 2010 nimo. Huko nyuma nchi ilikuwa inaongozwa na watu
  wenye maadili hata kama walikuwa na makosa yao.

  Inaelekea sasa wamehalalisha ujambazi. Nikiangalia hii EPA na kule kumwachia Ditopile, kwa kweli imefika mahali hakuna haja ya kukaa pembeni.

  Jiandae kunipeleka Bagamoyo kwi kwi kwi!!!
   
 7. Z

  Zanaki JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2008
  Joined: Sep 1, 2006
  Messages: 544
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mnaorudi mtushtue mapema,ili na sisi tutafute makada wa kutosha tuwapige t shirts za Jamiiforums wawe pale airport wengi kwa sana tu.Tupige vigelegele na makofi na kelele nyingi tu...kwi..kwi...kwi
   
 8. M

  Masatu JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hang on a minute, jamani hivi hili sakata la EPA na vurugu zote mtu mmoja simsikii kutajwa Mh Sumaye. Hivi hili jamaa lilikuwa zezeta kweli michongo yote hii illikuwa inapita juu juu na yeye kashangaa. Poor FTS!
   
 9. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #9
  Sep 4, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mhhh mengi yanawezekana....

  Pengine Sumaye alichagua pa kula na hakuona haja ya kuiba mchana kweupe kama walivyoiba EPA.

  Au pengine hakujua dili lililokuwa linaendelea.

  Au pengine badala ya EPA yeye alikabithiwa scholaship ya Harvad akaambiwa funga mdomo utulie kama unanyolewa.

  Au pengine ni msafi tu.
   
 10. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #10
  Sep 4, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Ni rahisi mno kupindisha sheria mkiwa mmekalia viti, lakini sheria hizo hizo zikipindishwa wakti mmekali jamvi hapo tutasikia kilio cha midomo na makalio.

  Tanzania siyo ya mtu binafsi, cham fulani, kikundi au genge la wazee wahuni wachache ndani ya serikali. Mkiwa bado na fursa pindisheni mambo muwezavyo saa yaja wengine mtavaa baibui ili ziwawezeshe kutoroka kwa ulaini.

  Nasi tuwasubiri huku Ughaibuni.
   
 11. l

  lawino New Member

  #11
  Sep 4, 2008
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaani uchungu ulioandika nao mi nau-feel kinoma hususan pale ninapozidi kuona mikutano ya kuunga mkono hotuba ya yule mheshimiwa sana bungeni! Yaani ukute hao wanaoandamana hivyo wamepewa vilemba,t shirt na kofia tu kama motivation ya kuandamana!

  Only asilimia 2 ya uchumi wa Tanzania uko formalized while the remaining is informal economy meaning that kodi za 98% imebebwa na hiyo 2%.Kwa hiyo wale asilimia mbili ndio watakao finance kununulia battery ya radar,na kufinance hayo mashangingi ambayo hao waheshimiwa wanatembelea bila kusahau posho zao.

  Swala zima la maadili ya uongozi has been flushed down the toilet na sasa tu viongozi ambao wako gut less na swala zima la maadili halimo kwenye dictionary zao! Wat i can say hiyo asilimia 2 is a walking time bomb siku ya kulipuka na kusema enough is enough.....patakuwa hapatoshi na litachimbika shimo!
   
 12. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #12
  Sep 4, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  EPA yageuka kaa la moto

  2008-09-04 12:08:04
  Na Muhibu Said

  Hatima ya mafisadi wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) bado ni kitendawili kutokana na kila kiongozi wa serikali anayezungumzia suala hilo kukwepa kwa mbinu zote kutoa kauli mahususi kama watafikishwa mahakamani wote bila kujali kama wamerejesha fedha walizoiba au la.

  Umma ukiendelea kutafakari kauli ya Rais Jakaya Kikwete bungeni hivi karibuni kwamba mafisadi wa makampuni 22 yaliyojichotea Sh. bilioni 133 za EPA wana mpaka Oktoba 31, mwaka huu wawe wamerejesha fedha hizo, vinginevyo watashitakiwa ifikapo Novemba mosi, Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Elieza Feleshi, ametoa kauli inayoonyesha wazi kwamba yu gizani kwa asilimia 100 kuhusu EPA.

  Akizungumza na Nipashe jana, Feleshi alisema hajui lolote kuhusu EPA na hata kama alishiriki kutoa ushauri kwa Timu ya watu watatu ya Rais inayochunguza jinai katika sakata hilo, haina maana kwamba anafahamu kuwa kuna suala EPA.

  ``Mimi kila mahali napoitwa kwenda kushauri nakwenda tu,`` alisema bila kuwa tayari kuingia kwa undani juu ya ushauri aliokuwa anautoa kwenye Timu hiyo na kama kuna makubaliano yoyote yalifikiwa ya kushitakiwa kwa wahusika wote wa EPA.

  Feleshi alikuwa mmoja wa wataalam wa serikali waliokuwa wanatoa ushauri kwa Timu hiyo inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika.

  Wajumbe wengine ni Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hosea.

  DPP huyo alisema hana la kusema kama watuhumiwa wa EPA watashitakiwa au la, kwani suala hilo liko mikononi mwa Timu ya Rais ya Kuchunguza wizi huo.

  Feleshi alitoa kauli hiyo alipotakiwa kueleza sheria inasemaje iwapo mtu akiiba fedha na kisha akazirejesha.
  Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Jinai namba 258, kuiba ni kosa la jinai.

  Hata hivyo, alisema timu hiyo inayoongozwa na Mwanyika ndiyo yenye wajibu wa kutoa maelekezo iwapo watuhumiwa hao wakabidhiwe kwa Polisi, Takukuru au katika Ofisi ya DPP kwa ajili ya mchakato wa kufikishwa mahakamani.

  ``Rais akishaunda timu, ni wajibu wa timu, ndiyo inayotoa maelekezo kama watu hao wakabidhiwe polisi, au Takukuru au kwangu,`` alisema Feleshi.

  Kauli hiyo imetolewa na Feleshi siku chache baada ya Gavana wa BoT, Profesa Beno Ndullu, kukaririwa na Nipashe akisema kwamba benki hiyo ina wajibu wa kuwashughulikia watumishi wake kwa kuwawajibisha kinidhamu tu, lakini kama kuna kushitakiwa mahakamani ni jukumu la timu ya Mwanyika.

  Hata hivyo, Feleshi alisema hawezi kuzungumzia suala la watuhumiwa wa wizi wa fedha za EPA kwa madai kwamba, suala hilo halijafika rasmi ofisini kwake na pia, hawafahamu watuhumiwa hao na pia, hafahamu kiasi cha fedha walichoiba.

  ``Hilo lina wasemaji wake, kwani sifahamu ni makubaliano yapi waliyofikia, hotuba ya Rais sina, ripoti ya timu sina, ni kina nani hao na waliiba shilingi ngapi,`` alisema Feleshi.

  Timu hiyo ilikabidhi ripoti yake kwa Rais Jakaya Kikwete, ambaye pia aliitumia kueleza Bunge kwa kirefu hatua alizochukua kutaka makampuni yote 22 yaliyoiba fedha hizo, yawe yamekwisha kuzirejesha ifikapo Oktoba 31, vinginevyo, Novemba Mosi, mwaka huu, watafikishwa mahakamani.

  Suala la EPA limekuwa gumu kupata wasemaji, hata wajumbe wa Timu ya Rais inyoongozwa na Mwanyika wamekuwa wepesi kukwepa kuzungumzia sakata hilo linalodaiwa kuigharimu serikali Sh. bilioni 133 zilizochotwa kwa njia za kifisadi BoT.

  Mara kadhaa, Mwanyika amekuwa bubu kuzungumzia suala hilo, ama amekataa kutoa maoni yoyote mbali tu ya kusema uchunguzi unaendelea.

  Serikali kwa ujumla wake imefanya bidii zote suala hilo lisijadiliwe kwenye vyombo vya habari na kuthibitisha nia hiyo, hata makabidhiano ya ripoti ya akina Mwanyika kwa Rais Kikwete yalifanyika kimyakimya.

  Awali waandishi wa habari walikuwa wamealikwa Ikulu kushuhudia makabidhiano hayo, lakini ghafla walipofika Ikulu walielezwa kwamba hafla hiyo imeahirishwa, na baadaye jioni picha na habari ya makabidhiano hayo vikasambazwa kwenye vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais.

  * SOURCE: Nipashe
   
 13. K

  Kazi ipo Member

  #13
  Sep 4, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani unategemea DPP atasema nini? suala la EPA ndio limefikia mwisha wake. Hakuna wa kupelkwa mahakamani wala wa kurudisha pesa. Wadanganyika tuliwe tu.
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Sep 4, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,408
  Likes Received: 81,441
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama huyu alikuwa msafi maana katika kipindi cha miaka 10 aliyokuwa waziri mkuu aliweza kukusanya utajiri wa kupindukia. Kabla ya kuwa waziri mkuu alikuwa hana utajiri wowote. Sijui katika kipindi hicho cha miaka 10 alifanya biashara gani kuweza kujilimbikizia utajiri huo. Pia kama mtakumbuka alichukua mkopo toka NSSF wa shilingi 50 millioni ambao ulipigiwa kelele sana maana haukuwa na riba na pia yeye hakustahili kupata mkopo toka NSSF maana si mwanachama wa mfuko huo.
   
 15. c

  care4all Senior Member

  #15
  Sep 4, 2008
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeshuhudia na wala si mara moja watu wanaoitwa wananchi wenye hasira jinsi yanavyo surubu vibaka. Simu tu, tena used, kibaka atapigwa mawe ,nondo,nk, na hatimaye moto kama hakutokea wa kumuokoa....Lakini mabaka (mafisadi) wanaoiba mamilioni, kutumia hela zetu wenyewe kutunyanyasa, kudidimiza uchumi wa taifa na kusabisha maafa wa watu wasio hatia, lakini wananchi hao hao wenye hasira kali wanaishia kuwapiga kupitia kwenye magazeti na mtandao..Mafisadi wanajulikana na tunatanua nao mtaani na hata kuwapiga mizinga, tunawakopa,then tukija kwenye magazeti ndio tunajifanya kutema cheche? je hizi hukumu za kwenye magazeti na mtandaoni ni effective kiasi gani? au je zinatosha kutokomeza mafisadi?....Hukumu ya kibaka ni kifo na fisadi madongo kweli jamii nzima inahitaji darasa
   
 16. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #16
  Sep 4, 2008
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Watanzania eh!? Mimi Rais wenu....

  --------------------------------------------------------------------------------

  JK: "Watanzania eh"

  WTZ: "Eh"

  JK: "Mimi Rais wenu!"

  WTZ: "eh!"

  JK: "Sina nguvu tena!"

  WTZ: "Eh"

  JK: "Ya kukamata mafisadi"

  WTZ: "Eh"

  JK: "Mafisadi ni wajanja"

  WTZ: "Eh"

  JK: "Wamekomba Benki Kuu" Watoto wanaendelea kuitia "Eh" kwa shauku!

  JK: "Wamelangua na Rada"

  "Wameiba Meremeta"

  "Wamechota nayo EPA"

  "Na makampuni mengine"

  "Sasa kimbieni!

  Watanzania kila mmoja anavyojua anaanza kutimkia kwake na kufanya mambo yake kuokoa maisha yake na ya familia yake.
   
 17. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #17
  Sep 5, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Kwetu Tanzania ukiiba fedha nyingi kila mtu anakuona wewe mjanja.
  Ukiiba simu unaleta udhia katika jamii ni bora ufe.
  Kwetu fedha ni mbadala wa maendeleo.

  Kwa akili na msimamo kama huo tutaanzia wapi kuwabana Wezi wakubwa wa EPA,RICHMONDULI,LOLIONDO, DEEPGREEN,MEREMETA, TANGOLD na KAGODA AGRICULT?

  WAKATI WAHUSIKA WA WIZI HUU NI MACELEBRITY WA KUIGWA??
   
 18. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #18
  Sep 5, 2008
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Unajua mkuu, tatizo tulilo nalo ni kwamba kuna deep ethical problem Tanzania! Mawazo ya watu ni kwamba kila kitu ni ujanja, lakini pia kama wanadamu wengine wote tunaona pesa ni kipimo cha utu.
   
Loading...