TUJIKUMBUSHE - Kweli hata mimi kura yangu kwa JK na CCM - BIG NO!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TUJIKUMBUSHE - Kweli hata mimi kura yangu kwa JK na CCM - BIG NO!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ELNIN0, Aug 13, 2010.

 1. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Mdau mmoja wa JF alishazileta hizi - na mimi nimeamua kuwakumbusha tena na tena napenda hizi ziwe kama sara zenu asubuhi na jioni. Mtafanya hivi kuokoa kizazi chenu. JK ameshindwa kutekeleza haya yote sasa hakuna sababu za msingi za kumpa kura yako. Nimeileta leo Ijumaa ili Weekend hii mtafakari ninyi na familia zetu. Kuchagua CCM ni sawa na kuamua kuuza familia kwa walaghai.

  1. Chini ya uongozi wake uchumi umeshuka na thamani ya shilingi dhidi ya dola imezidi kuporomoka zaidi
  2. Ameshindwa kuboresha maisha ya mtanzania wa kawaida (tofauti na kauli mbiu yake “maisha bora kwa kila mtanzania”. Amepiga kelele ya KILIMO KWANZA huku tunaona dhahiri hana nia yoyote kukuza kilimo! Ni msaliti
  3. Ameshindwa kuboresha miundombinu (barabara etc)
  4. Chini ya uongozi wake, amefanya uteuzi wa aibu kwa Mkurugenzi wa ATC ambaye ni mshikaji wake, matokeo yake ameua kabisa ATC…Tanzania (kama nchi) inashindwa hata na mfanyabiashara binafsi anayendesha Precision Air kwa mafanikio
  5. Akiwa rais wa Tanzania ameshindwa kusimama imara kutetea maslahi ya nchi dhidi ya wizi wa mali ya umma na kashfa ya mabilioni ya shilingi ya Richmond...JE NAYE ALIHUSIKA? PCB NA USALAMA MNAJUA WENYEWE...ENDELEENI KULINDA MASLAHI YENU!!
  6. Yeye kama kiongozi wa Nchi amewakebehi hadharani wafanyakazi wa Tanzania na viongozi wao pale TUCTA ilipotaka kuitisha mgomo. Yeye kama kiongozi mkuu wa nchi hakuwa na taarifa sahihi kutoka kwa watendaji wake, akawanawa viongozi wa wafanyakazi mbele ya wazee wa CCM, cha ajabu yeye ndiye alikuwa hana taarifa sahihi! Kama kiongozi alitakiwa kuwajibika mara moja. URAIS NA USWAHILI WAPI KWA WAPI?
  7. Katika kipindi chake cha uongozi amefanya uteuzi wa viongozi wasiokuwa na uwezo, wakiwemo baadhi ya mawaziri (washkaji) ambao wamekuwa wakiweka mbele maslahi binafsi na kutojali wananchi.
  8. Katika kipindi chake cha uongozi RUSHWA IMEONGEZEKA na hakuna hatua madhubuti alizochukua zaidi ya kuwa msemaji saaaaana bila vitendo.
  9. Katika kipindi chake cha uongozi matimizi mabaya ya fedha katika manunuzi ya magari ya kifahari na fanicha kwa viongozi wa serikali, wakiwemo wakuu wa mikoa, mawaziri na yeye mwenyewe AKIONGOZA UOZA HUO KWA KUNUNUA BMW X-5 kwa matumizi yake.
  10. Ni kiongozi aliyesafiri mara nyingi zaidi ya waliomtangulia (katika awamu ya kwanza ya uongozi wao), safari hizi zimetumia mabilioni ya feadha za watanzania lakini hakuna faida tunayoiona kutokana na safari zake
  11. KAGODA anamjua lakini kwa sababu zake mwenyewe kashindwa kumshughulikia ingawa katiba imempa marungu yote.
  12. Mwisho hataki KURA za wafanyakazi, sasa kwa nini tujikombe kwake?

  ANGALIZO:
  Tunataka kiongozi atakayejali maslahi ya wananchi wake, kuwatetea na kulinda raslimali za taifa.

  TUUNGANE KUSEMA NO KWA KIKWETE.
   
 2. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  untitled3.JPG untitled1.JPG untitled5.JPG untitled.JPG untitled4.JPG untitled6.JPG untitled2.JPG

  Maisha ya Watanzania yakiwa yanazidi kudidimia - Maradhi, Njaa, Ujinga vikizidi kuwaandama - Miaka 40 ya uhuru bado hatusogei. Wakati huo huo wajanja wachache wakijichumia mali asili zetu.
   
 3. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  lakini wakuu,
  ina maana huyu JEIKEI hakuna hata moja zuri ambalo amelifanya?
   
 4. Democrasia

  Democrasia Member

  #4
  Aug 13, 2010
  Joined: Feb 1, 2008
  Messages: 80
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Mimi nadhnai imefikia wakati sisi Watanzania Tuamke kama wenzetu wakenya... Tukizubaa tuu Jumuiya ya Africa Mashariki tutakuwa tukiburuza Mkiani.
  Tumpatie DR. SLAA tena kwa kuwa ni Mtanzania mwenzetu

  Mwaka huu hoyeeeeeeeee kwa Chadema
   
 5. K

  Kagasheki Member

  #5
  Aug 13, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata kama kuna mazuri aliyofanya kama yamezidiwa uzito na mabaya unatarajia yaongelewe yapi?.Ni wazi yatazungumzwa mabaya yanayoathiri maisha ya walio wengi kuliko mazuri yanayonufaisha wachache walio na ubinafsi wa kupitiliza.Tukubali tunahitaji mabadiliko na muda ni huu na si vinginevyo
   
 6. M

  Mkulima mimi JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 233
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Hamna! Ndio maana hata wewe huoni unaamua kunauliza!
  Ila hata kama yapo mabaya ni mengi ambayo hayatakiwi kuvumiliwa sababu yanatishia mstakabali wa taifa yakiachwa yaendelee! Na jeikei hajaona kama ni tatizo tukimrudisha atayaendeleza! Ni sawa ukapika ugali afu juu likadondoka tone la chakula! Chakula hakifai kuliwa tena!
   
 7. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,939
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Ameshindwa kulinda katiba ya jamhuri ya muungano mpaka inachezewa na Wazenj!!
   
 8. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #8
  Aug 13, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Yataje mambo 12 mazuri JK amefanya kama mabaya yalivyotajwa na ELNINO nitakupa thank you!
   
 9. M

  Mkulima mimi JF-Expert Member

  #9
  Aug 13, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 233
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Pia kikwete hafai kuwa mgombea na mwanachama wa chama cha mapinduzi kwa sababu amekiuka ahadi za mwanachama wa ccm ahadi alizo kiuka ni
  Ahadi #1 binadamu wote ni ndugu na afrika ni moja. Hapa amekiuka kuna watu ambao wakikamatwa nchi itayumba na wengine wakamatwe kwa hiyo kuna matabaka
  ahadi no.2 nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote, yeye anatumikia walio nacho tu ndio maana hataki kura za wafanyakazi!
  Ahadi no.3 nitajitolea nafsi yangu kuondosha umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma. Hapa kuhusu kila umaskini kila mtu anajua kuwa umeongezeka. ujinga ndio hivyo kuna shule za maskini hazina waalimu wala vitabu. dhuluma imezidi
  ahadi no.5 Cheo ni dhamana,sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu. Ametumia cheo chake kufanya utalii sehemu mbalimbali za dunia
  Ahadi na 7. Nitashirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu sina uhakika kama ametimiza hii ahadi!
  Ahadi #8 nitasema kweli daima fitina kwandu mwiko. Ametudanganya kuwa ana majina ya madawa ya kulevya hajataja mpaka leo hii ni fitina!
  NAWASILISHA
   
 10. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #10
  Aug 13, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Labda haya.....
  1.Kumleta George Kichaka
  2.Sullivan summit
  3.Kuwa mwenyekiti wa AU
  4.Kuleta mkutano wa WEF
  5.Kuongeza foleni(maendeleo kwa mujibu wake mwenyewe)
  6.Kuwaleta Brazil kwa 7bn/-
  7.Kutooa mke wa pili pasi na kuwa na ruksa na nafasi ya kufanya hivo
  8.Kuwezesha wanafamilia wake watatu kushika nyadhifa CCM
  9.Kumteua entertainer kuongoza CCM(Makamba)
  10.Kumpandisha chati First Lady mapaka kuwa na motorcade ya kufa mtu
  11.Kuongeza kicheko chake
  12.Kukuza uchumi wakati shiling ikishuka thamani(a feat no joke about it)
   
 11. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #11
  Aug 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  unajua wakuu hoja zenu hazieleweki kwasababu hamleti MAZURI YA JK japo mawili tu....!
  1)-ujenzi wa UDOM
  2)-ujenzi wa barabara
  3)-kuongezeka kwa miundombinu ya elimu
  4)-
   
 12. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #12
  Aug 13, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Mmmh ni hayo tu kwa muda wa miaka mitano? Kaazi kwelikweli. Mbona mapungufu ni mengi zaidi kuliko mazuri? Halafu ukumbuke alichaguliwa ili afanye hayo aliyofanya. Ilikuwa ni sehemu ya kazi yake. Kile ambacho alivurunda, hatukumtuma sisi. Ndiyo maana tunaangalia zaidi mahali alipokosea kuliko alipofanikiwa. Kwa kuwa mafanikio ndiyo kazi tuliyompa akaifanye na mabaya aliyafanya mwenyewe bila ridhaa yetu.
   
 13. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #13
  Aug 13, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Kwa pesa ya nani?...kama ni kodi yetu basi hajafanya jema bali amefanya kazi aliyotakiwa kuifanya
   
 14. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #14
  Aug 13, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mchakato huo uwote hapo juu ulianza tangu awamu zilizopita so mmh, we need something new eeh! and gud 4 tha country
   
 15. L

  Lubaluka JF-Expert Member

  #15
  Aug 13, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 496
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  -- ????????
   
 16. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #16
  Aug 13, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Huwezi kujisifu umewafanyia kazi wananchi wako kama hujatekeleza yafuatayo, then unaomba upewe muda zaidi -
  1. Unashabikia uuzaji wa viwanda na zoezi zima la ubinafisishaji kwa mikataba mibovu
  2. Unashabikia uomba omba - serikali ombaomba
  3. Unashabikia kuzikwa kwa kilimo ambacho ni uti wa mgogo na unadiriki kuwadanganya wananchi wako
  kwa wimbo wa KILIMO KWANZA
  4. Unashabikia Ujenzi wa majengo kila kata ambayo unayaita eti shule za upili - unaua elimu
  5. Unashabikia wizi wa mali za umma na unasaidia kuwaficha wezi
  6. Unasema uwongo kwa wananchi "Maisha bora yako wapi so far?"
  7. Unashabikia uundwaji wa serikali kubwa hali ukijua nchi iko hoi bin taabani - matokeao yake bajeti yote
  inaishia kwenye vikao na magari ya kifahari
  8. Unasahau afya na kina mama na mtoto - zahanati vijijini kabuti
  9. Unawasahau wastaafu - watu waliotumikia taifa hili kwa moyo wote, leo hii unawalipa elfu hamsini
  unataka wafe mapema
  10. Unaunda serikali ya matanuzi - nyumba ya Jaji mkuu hadi million xxx ? kwani akikaa ya million 10 hawezi fanya kazi ya kuwatumikia wananchi

  Nitamchagua mtu atakayekuwa na uwezo wa kurekebisha hayo yote - kwangu hayo ndiyo KEY ya kutokukuchagua.
   
 17. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #17
  Aug 13, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Kura kwa chadema.
   
 18. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #18
  Aug 13, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Mkuu Teamo sijakupata hivi hizi ndizo key perfomance za serikali ya CCM chini ya JK kwa miaka mitano?
  kama ndiyo hizi basi shughuli pevu.
   
 19. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #19
  Aug 13, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ameshindwa kuonyesha ujasiri kama mkuu wa nchi kwa kuyashughulikia kwa ukweli na uaminifu masuala nyeti na mazito kama:
  1. Kagoda (wahusika ni jamaa zake)
  2. Deep green finance (kama hapo juu)
  3. Ameshindwa kuwawajibisha watendaji walioiingiza nchi katika mikataba ya kifisadi kama vile Richmond, RITES, IPTL, Buzwagi, ATCL
  4. Aemeleta siasa kwenye masuala yanayohitaji taaluma mfano kuruhus ujenzi wa shule holela bila kuwa na miundombinu kama walimu, maabara, mabweni, nyumba za waalimu
  5. Ameshindwa kulishughulikia kwa uaminifu janga la UKIMWI na badala yake ameweka siasa zaidi huku watanzania wakiendelea kuteketea kwa maambukizi mapya hasa hasa maeneo ya vijijini (mfano kanda ya ziwa ninakotoka hakuna hata dalili za kwamba kuna janga la ukimwi) huku serikali ikitumia fedha nyingi za walipa kodi na wahisani
  6. Hajui chanzo cha umasikini wa nchi yetu, hili alikili mwenyewe katika mahojiano na mwandishi mmoja wa nje wakati akiwa katika moja ya safari zake nyingi ughaibuni
  7. ................................ mengine mengi tu, vidole vinauma kuendelea kuandika naomba wadau muendeleze
   
 20. Safina

  Safina JF-Expert Member

  #20
  Aug 13, 2010
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 498
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hoja zinaeleweka sana 2: Haya uliyo-orodhesha hapa JK hajayaanzisha wala kuyaendeleza, mfanyo ujenzi UDOM, hii shughuri aliikuta inaendelea aliyeianzisha ni Ben, Ujenzi wa barabara ipi? Kuongezeka kwa mindo mbinu ya elimu wakati ameanzisha shule za kata zisizokuwa na waaalimu, miundombinu ya elimu ipialiyoongeza wakati wadogo zetu wameshindwa kama nini. MWAKA HUU NI CHADEMA 2 HATA KAMA CCM WATAIBA, LAKINI TUTAKUWA HATUJAWACHAGUA, BALI WAMEJIPA MADARAKA WENYEWE. Ni sawa na nyumbani baba unapokosa heshima kwa watoto na mama yao, halafu ukatumia ubabe kwa kuwa tu wewe ni baba, haipendezi hata kidogo.
   
Loading...