Tujikumbushe kuhusu Lugha yetu

PEVU HALISI

JF-Expert Member
Dec 19, 2018
207
85
Salamu kwenu waungwana, tujikumbushe kidogo.

Toa maana mbili ya maneno yafuatayo:-
1. Mbuzi
2.Tenga
3. Kaa
4. Taa
 
Salamu kwenu waungwana, tujikumbushe kidogo.

Toa maana mbili ya maneno yafuatayo:-
1. Mbuzi
2.Tenga
3. Kaa
4. Taa

1)¡. Kifaa kinachotumika kwa kukunia nazi.
¡¡. Pia mbuzi mnyama.

2) ¡. Kugawa/kuchanganua vitu vilivyopamoja na kuvifanya zaidi ya sehemu moja.
¡¡. Kifaa kinachotumika kwa kuwekea vitu na sifa yake kubwa inakuwa na matundu kutokana na utengenezwaji wake.
Zipo zaidi.

3.¡. Kitendo mfano kaa kitako/chini.
¡¡. Pia ni aina fulani ya kitoweo kinachopatikana baharini anaejulikana kwa jina hilo lá kaa.

4.¡. Ni kifaa kinachotumika kwa ajili ya upatikanaji WA mwanga mfano balbu,kandili n.k.
¡¡. Pia ni jamii ya samaki anaepatikan baharini.

Nimejaribu ikiwa kunamakoseo naomba kukosolewa ili nijifunze zaiid.
 
Back
Top Bottom