Uchaguzi 2020 Tujikumbushe kuelekea uchaguzi mkuu tarehe 28 Oktoba, 2020

desmond JJ

Member
Jul 6, 2012
55
26
TUJIKUMBUSHE MAMBO MBALIMBALI KWA MUJIBU WA MIONGOZO YA NEC

  1. Wajibu wa Vyama vya siasa wakati huu wa kampeni ni kunadi sera kwa kuzingatia Sheria za Uchaguzi,Kanuni na Maadili ya Uchaguzi. Kama inavyoelekezwa katika kifungu cha 51 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na kifungu cha 53 (1) (b) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292.
  2. Jukumu la kuendesha kampeni za uchaguzi ni la Mgombea, Wakala wa mgombea au chama chenyewe.
  3. Kila Mgombea kipindi hiki cha Kampeni anapaswa kuzingatia Maadili ya Uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuheshimiana, kuelimisha wanachama wake na wananchi kwa ujumla waweze kuelewa sera za chama husika, kutojenga chuki na kuhakikisha kuwa kampeni zinafanyika kwa amani na utulivu.
  4. Kila chama chenye mgombea kina haki ya kuteua mawakala na kuwasilisha majina ya mawakala hao ngazi stahiki za usimamizi wa uchaguzi, siku saba (7) kabla ya siku ya uchaguzi (kwa maana nyingine kabla ya tarehe 21/10/2020 majina ya mawakala yanapaswa kuwa yamekwisha wasilishwa). Aidha mawakala hawa watakuwa na jukumu la kushirikiana na Wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha zoezi zima la upigaji kura linafuata sheria na taratibu zilizowekwa.
  5. Baada ya kukamilika kwa zoezi la upigaji kura, wakala wa upigaji ndiye atakuwa wakala wa kuhesabu kura. Hivyo atatakiwa kukiwakilisha chama chake kwenye zoezi la kuhesabu kura.
  6. Mawakala wote wa upigaji kura na uhesabuji kura wanatakiwa kuapa kiapo cha kutunza siri mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi au Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi siku saba (7) kabla ya Siku ya Uchaguzi kwa kutumia Fomu Na. 6. Hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 50 (4) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge ya mwaka 2020 na kanuni ya 43 (4) ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2020.
  7. Ni muhimu vyama vya siasa viwafundishe Mawakala na Wagombea wao taratibu mbalimbali zinazopaswa kufuatwa wakati wa Mchakato mzima wa upigaji kura.
  8. Nakala ya fomu ya Matokeo inapaswa kubandikwa nje mahala pa wazi katika eneo la kuhesabia Kura mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo.
ONGEZA MENGINE UNAYOYAFAHAMU HAPA
 
Tunashukuru sana. Haya ndio mambo ambayo watanzania tunayahitaji kwa wakati huu tunapokwenda katika Uchaguzi Oktoba 28,2020. Sio kuja na malalamiko tuuuuuu tena mengine mfano Malalamiko ya jambo kalitenda Twitter unamlaumu Jamii Forums. Safi sana
 
Back
Top Bottom