Kiswahili: Methali, Vitendawili, nahau, Misemo n.k

Asiyejua maana haambiwi maana.

Kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi

kusema ukweli vinanichanganya kati ya nahau, methali na misemo.

Fuata nyuki ule asali

tembea uone

NDIO HAPO SASA!
Methali ni proverbs au?
na Nahau ni idiomatic expressions..au mnasemaje wajuzi wa lugha?
 
Nimeamini kuwa ni kweli mimi sijui kiswahili wala kiingereza. Na lugha ya kwetu milimani nayo haipandi.
Aibu tupu!
asante mkuu, yani mie ndio kiazi wa both.... nimejua rasmi kwamba ujanja wangu ni kuunga-unga sentensi tu... nothing more!!!

kuna hii inasema "mwenda tezi na omo... marejeo ngamani" ina maana gani?
 
Tuendelee na nahau mpya...na tutofautishe na methali
Labda tuangalie idioms ili tuone kwenye kiswahili kuna nini...

to kick the bucket = to die = kukata kamba = kufa ( Hapa tunaona kuwa haihusiani na kamba wala ndoo)
can of worms = trouble = kuleta kasheshe = matatizo ( Hakuna cha kopo wala minyoo/wadudu japo vimetumika)
Being up in arms =to be very angry in protest -=kupandisha munkari/hasira
A bone of contention = source/locus of argument - mtanange = kinachopambaniwa

Haya tuendelee kwa mifano zaidi
 
Wakuu nisaidieni kujua maana ya methali&nbsp;<br>1. KOKO HAIDARI MAI&nbsp;<br>2. HAKUNA KAPA ISIYOKUWA NA USUBI<br>3. MCHAMA AGO HANYELI HWENDA AKAUYA PAPO<br>4. USIACHE MBACHAO KWA MSALA UPITAO&nbsp;<br>5. ANGA KAANGA TU CHINI YA GAE
 
Wakuu nisaidieni kujua maana ya methali&amp;nbsp;&lt;br&gt;1. KOKO HAIDARI MAI&amp;nbsp;&lt;br&gt;2. HAKUNA KAPA ISIYOKUWA NA USUBI&lt;br&gt;3. MCHAMA AGO HANYELI HWENDA AKAUYA PAPO&lt;br&gt;4. USIACHE MBACHAO KWA MSALA UPITAO&amp;nbsp;&lt;br&gt;5. ANGA KAANGA TU CHINI YA GAE
 
3. Mchama ago hanyeli huenda akawia papo.

Mchama = kuchama (mtu)=kuhama (mtu)

Ago= (?)

hanyeli= hanyi (halinyei)

akawia= kuwia= kurejea

Papo= hapo hapo

Anaehama pahala hatakiwi apanyee kwa kuwa inawezekana akarudi hapo hapo. Au kwa kiswahili cha siku hizi ni kuwa usipaharie pahala kwa sababu unahama kwa kuwa unaweza ukarejea hapo hapo :)
 
4. Usiache mbachao kwa msala upitao

Usiache= usiache
Mbacha= kipande cha mkeka mkongwe, mkuu-kuu, chakavu,
-o = wako
Msala= kipande cha mkeka chenye hadhi nzuri, usafi
Upitao= unaopita

Usiache mkeka wako mkongwe kwa msala usiokuwa wako wa kudumu. Kwa kiswahili cha siku hizi usitupe bigG kwa karanga za kuomba au Usijipe ufaghari kwa wali wa matangani

Usidharau chako kwa kitu kinachopita tu japo kama ni kizuri zaidi ya kile chako
 
3. Mchama ago hanyeli huenda akawia papo.

Mchama = kuchama (mtu)=kuhama (mtu)

Ago= (?)

hanyeli= hanyi (halinyei)

akawia= kuwia= kurejea

Papo= hapo hapo

Anaehama pahala hatakiwi apanyee kwa kuwa inawezekana akarudi hapo hapo. Au kwa kiswahili cha siku hizi ni kuwa usipaharie pahala kwa sababu unahama kwa kuwa unaweza ukarejea hapo hapo :)
Ah!, hii imekaa vyema! nashukuru mkufunzi!
 
Wakuu nisaidieni kujua maana ya methali
1. KOKO HAIDARI MAI
2. HAKUNA KAPA ISIYOKUWA NA USUBI
3. MCHAMA AGO HANYELI HWENDA AKAUYA PAPO
4. USIACHE MBACHAO KWA MSALA UPITAO
5. ANGA KAANGA TU CHINI YA GAE

Nitajaribu namba nne na tano;
4)Mbachao ni mkeka kuukuu . ambao unautumia kwa shida naraha,lakini huo
msala ulioazima kwa jirani yako utautumia muda mfupi tu kwani mwenyewe atauhitaji baadaye
hivyo itabidi uurudishe. ina maana thamini kilicho chako ingawa kibovu.
methali nyingine zianzofanana nayo:
Chako ni chako usitegemee cha mwingine.
Thamini chako.
Ukipata Chungu kipya usitupe cha zamani. kitakufaa mbele ya safari.

5)Kwa wale wa vijijini wanaotumia jiko la kuni lenye mafiga matatu wataelewa vizuri mfano huu
wewe unapika mfano chakula kwenye hilo jiko la kuni, umewasha moto umetoka kidogo
kwenda anakuja mtu nyuma anazima moto na anatoa kuni., hivyo unachopika hakitaiva.
hii inaonya kwamba kuna fitina nyingi katika jamii zetu, watu hatutakiani mema.
 
Nitajaribu namba nne na tano;
4)Mbachao ni mkeka kuukuu . ambao unautumia kwa shida naraha,lakini huo
msala ulioazima kwa jirani yako utautumia muda mfupi tu kwani mwenyewe atauhitaji baadaye
hivyo itabidi uurudishe.

5)Kwa wale wa vijijini wanaotumia jiko la kuni lenye mafiga matatu wataelewa vizuri mfano huu
wewe unapika mfano chakula kwenye hilo jiko la kuni, umewasha moto umetoka kidogo
kwenda anakuja mtu nyuma anazima moto na anatoa kuni., hivyo unachopika hakitaiva.
hii inaonya kwamba kuna fitina nyingi katika jamii zetu, watu hatutakiani mema.

msala nayo maana yake nini!?? au ni mkeka mpya?

5. Please hebu dadavua zaidi kiasi, mimi nimeshatumia jiko la kuni ila bado sijakunyaka vizuri mkuu!
 
1. KOKO HAIDARI MAI
Hiki ni Kiswahili cha Lamu, Koko ni aina ya mti unaoota kwenye maji (Mikoko), kwa kiswahili chepesi unaweza kusema hivi "Mkoko haupati maji".

Methali hii ina maana kuwa: Japokuwa mikoko inaota kwenye maji lakini matawi yake yapo juu na hayaguswi na maji. Ikimaanisha kuwa binadamu unaweza kuzaliwa na kuishi kwenye mazingira ya watu wenye tabia mbaya lakini wewe tabia yako ikawa ni nzuri kuliko hao walio kuzunguka.

2. HAKUNA KAPA ISIYOKUWA NA USUBI (Hapana kapa isiyokuwa na usubi)
Hakuna kanzu (mikono mifupi) itakayo kukinga na mbu. Maana yake ni kuwa hakuna mtu aliye mkamilifu.

Kapa ni aina ya kanzu isio na mikono
Usubi ni aina ya wadudu wadogo wanafanana na mbu pia uuma.

3. MCHAMA AGO HANYELI HWENDA AKAUYA PAPO (Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo)
Msafiri anyei kambi aifikiayo, huwenda siku moja anaweza kurudi tena.

Ikimaanisha kuwa usimfanyie fujo au kumtukana mtu usiye mjua anaweza kuja kukusaidia siku za mbele. Ni sawa na kusema usimdharau usiye mjua.

4. USIACHE MBACHAO KWA MSALA UPITAO
Kamwe usiwache (Kudharau) chako cha zamani kwa ajili ya mkeka (kusalia) cha kuazima.

Thamini zaidi kilicho chako, kuliko kuthamini kitu cha kuazima cha mwenzako hata kama kinaonekana kuwa bora kuliko chako.

5. ANGA KAANGA TU CHINI YA GAE
Hata ukiKaanga sisi tupo chini ya kikaangio... Tutajuwa tu kilichopo kwenye kikaangio

Ikimaanisha kuwa hata ukificha siri za ndani, lakini kuna siku kuna mtu atakuja juwa siri yako.
 
1. KOKO HAIDARI MAIHiki ni Kiswahili cha Lamu, Koko ni aina ya mti unaoota kwenye maji (Mikoko), kwa kiswahili chepesi unaweza kusema hivi "Mkoko haupati maji". Methali hii ina maana kuwa: Japokuwa mikoko inaota kwenye maji lakini matawi yake yapo juu na hayaguswi na maji. Ikimaanisha kuwa binadamu unaweza kuzaliwa na kuishi kwenye mazingira ya watu wenye tabia mbaya lakini wewe tabia yako ikawa ni nzuri kuliko hao walio kuzunguka.2. HAKUNA KAPA ISIYOKUWA NA USUBI (Hapana kapa isiyokuwa na usubi)Hakuna kanzu (mikono mifupi) itakayo kukinga na mbu. Maana yake ni kuwa hakuna mtu aliye mkamilifu.Kapa ni aina ya kanzu isio na mikonoUsubi ni aina ya wadudu wadogo wanafanana na mbu pia uuma. 3. MCHAMA AGO HANYELI HWENDA AKAUYA PAPO (Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo)Msafiri anyei kambi aifikiayo, huwenda siku moja anaweza kurudi tena.Ikimaanisha kuwa usimfanyie fujo au kumtukana mtu usiye mjua anaweza kuja kukusaidia siku za mbele. Ni sawa na kusema usimdharau usiye mjua.4. USIACHE MBACHAO KWA MSALA UPITAOKamwe usiwache (Kudharau) chako cha zamani kwa ajili ya mkeka (kusalia) cha kuazima.Thamini zaidi kilicho chako, kuliko kuthamini kitu cha kuazima cha mwenzako hata kama kinaonekana kuwa bora kuliko chako.5. ANGA KAANGA TU CHINI YA GAEHata ukiKaanga sisi tupo chini ya kikaangio... Tutajuwa tu kilichopo kwenye kikaangioIkimaanisha kuwa hata ukificha siri za ndani, lakini kuna siku kuna mtu atakuja juwa siri yako.
asante
 
Duh Bwana X-paster..sijui nikushukuruje...UMENIFUNGUA MACHO sana!
Ubarikiwe bwana...
 
1. KOKO HAIDARI MAI
Hiki ni Kiswahili cha Lamu, Koko ni aina ya mti unaoota kwenye maji (Mikoko), kwa kiswahili chepesi unaweza kusema hivi "Mkoko haupati maji".

Methali hii ina maana kuwa: Japokuwa mikoko inaota kwenye maji lakini matawi yake yapo juu na hayaguswi na maji. Ikimaanisha kuwa binadamu unaweza kuzaliwa na kuishi kwenye mazingira ya watu wenye tabia mbaya lakini wewe tabia yako ikawa ni nzuri kuliko hao walio kuzunguka.

2. HAKUNA KAPA ISIYOKUWA NA USUBI (Hapana kapa isiyokuwa na usubi)
Hakuna kanzu (mikono mifupi) itakayo kukinga na mbu. Maana yake ni kuwa hakuna mtu aliye mkamilifu.

Kapa ni aina ya kanzu isio na mikono
Usubi ni aina ya wadudu wadogo wanafanana na mbu pia uuma.

3. MCHAMA AGO HANYELI HWENDA AKAUYA PAPO (Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo)
Msafiri anyei kambi aifikiayo, huwenda siku moja anaweza kurudi tena.

Ikimaanisha kuwa usimfanyie fujo au kumtukana mtu usiye mjua anaweza kuja kukusaidia siku za mbele. Ni sawa na kusema usimdharau usiye mjua.

4. USIACHE MBACHAO KWA MSALA UPITAO
Kamwe usiwache (Kudharau) chako cha zamani kwa ajili ya mkeka (kusalia) cha kuazima.

Thamini zaidi kilicho chako, kuliko kuthamini kitu cha kuazima cha mwenzako hata kama kinaonekana kuwa bora kuliko chako.

5. ANGA KAANGA TU CHINI YA GAE
Hata ukiKaanga sisi tupo chini ya kikaangio... Tutajuwa tu kilichopo kwenye kikaangio

Ikimaanisha kuwa hata ukificha siri za ndani, lakini kuna siku kuna mtu atakuja juwa siri yako.

Asante sana kwa ufafanuzi. Nimekuelewa vyema sana mkuu
 
msala nayo maana yake nini!?? au ni mkeka mpya?

5. Please hebu dadavua zaidi kiasi, mimi nimeshatumia jiko la kuni ila bado sijakunyaka vizuri mkuu!

Mkuu Mentor
Ni Mkeka mpya . Lakini nafikiri mkuu X -Paster ni mtaalamu zaidi , naye kafafanua mambo vizuri. Thanks.
 
1. KOKO HAIDARI MAI
Hiki ni Kiswahili cha Lamu, Koko ni aina ya mti unaoota kwenye maji (Mikoko), kwa kiswahili chepesi unaweza kusema hivi "Mkoko haupati maji".

Methali hii ina maana kuwa: Japokuwa mikoko inaota kwenye maji lakini matawi yake yapo juu na hayaguswi na maji. Ikimaanisha kuwa binadamu unaweza kuzaliwa na kuishi kwenye mazingira ya watu wenye tabia mbaya lakini wewe tabia yako ikawa ni nzuri kuliko hao walio kuzunguka.

2. HAKUNA KAPA ISIYOKUWA NA USUBI (Hapana kapa isiyokuwa na usubi)
Hakuna kanzu (mikono mifupi) itakayo kukinga na mbu. Maana yake ni kuwa hakuna mtu aliye mkamilifu.

Kapa ni aina ya kanzu isio na mikono
Usubi ni aina ya wadudu wadogo wanafanana na mbu pia uuma.

3. MCHAMA AGO HANYELI HWENDA AKAUYA PAPO (Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo)
Msafiri anyei kambi aifikiayo, huwenda siku moja anaweza kurudi tena.

Ikimaanisha kuwa usimfanyie fujo au kumtukana mtu usiye mjua anaweza kuja kukusaidia siku za mbele. Ni sawa na kusema usimdharau usiye mjua.

4. USIACHE MBACHAO KWA MSALA UPITAO
Kamwe usiwache (Kudharau) chako cha zamani kwa ajili ya mkeka (kusalia) cha kuazima.

Thamini zaidi kilicho chako, kuliko kuthamini kitu cha kuazima cha mwenzako hata kama kinaonekana kuwa bora kuliko chako.

5. ANGA KAANGA TU CHINI YA GAE
Hata ukiKaanga sisi tupo chini ya kikaangio... Tutajuwa tu kilichopo kwenye kikaangio

Ikimaanisha kuwa hata ukificha siri za ndani, lakini kuna siku kuna mtu atakuja juwa siri yako.
Shukran sana Mkuu
 
  1. Adhabu ya kaburi aijua maiti, The touture of the grave is only known by the corpse
  2. Akiba haiozi, A reserve will not decay
  3. Asifuye mvuwa imemnyea. He who praises rain has been rained on.
  4. Akili nyingi huondowa maarifa. Great wit drives away wisdom
  5. Asiye kubali kushindwa si mshindani.He who does not admit defeat is not a sportsman
  6. Atangaye na jua hujuwa. He wanders around by day a lot, learns a lot
  7. Asiye kuwapo na lake halipo.If you are absent you lose your share
  8. Avumaye baharini papa kumbe wengi wapo.Shark is the famous one in sea the but they many others
  9. Baada ya dhiki faraja.After hardship comes relief.
  10. Baniani mbaya kiatu chake dawa.An evil Indian but his bussiness is good.
  11. Bendera hufuata upepo. A flag follows the direction of the wind.
  12. Bilisi wa mtu ni mtu.The evil spirit of a man is a man.
  13. Chamlevi huliwa na mgema.The drunkard's money is being consumed by palm-wine trapper.
  14. Chanda chema huvikwa pete.A handsome finger gets the ring.
  15. Chombo cha kuzama hakina usukani. A sinking vessel needs no navigation.
  16. Chovya - chovya yamaliza buyu la asali. Constant dipping will empty goud of honey
  17. Dalili ya mvua mawingu. Clouds are the sign of rain
  18. Damu nzito kuliko maji.Blood is thicker than water
  19. Dawa ya moto ni moto. the remedy of fire is fire
  20. Dua la kuku halimpati mwewe.the curse of the fowl does not bother the kite.
  21. Fadhila ya punda ni mateke. Gratitude of a donkey is a kick.
  22. Fimbo ya mbali hayiuwi nyoka. A wepon which you don't have in hand wont kill a snake.
  23. Fuata nyuki ule asali.Follow bees and you will get honey
  24. Fumbo mfumbe mjinga mwerevu huligangua.Put a riddle to a fool a clever person will solve it
  25. Ganda la mua la jana chungu kaona kivuno.The skin of yesteday's sugarcane is a havest to an ant.
  26. Haba na haba hujaza kibaba.Little by little fills up the measure.
  27. Hapana marefu yasio na mwisho.They is no distance that has no end.
  28. Hakuna siri ya watu wawili.They is no secret between two people.
  29. Haraka haraka haina baraka.Hurry hurry has no blessings
  30. Hasira, hasara.Anger brings loss(Damage)
  31. Heri kufa macho kuliko kufa moyo.It is better to lose your eyes than to lose your heart.
  32. Heri kujikwa kidole kuliko ulimi.Better to stumble with toe than toungue.
  33. Hiari ya shinda utumwa.Voluntary is better than force.
  34. Hucheka kovu asiye kuwa na jeraha.He laughs at scar who has received no wound.
  35. Ihsani (hisani)haiozi.Kindness does not go rotten.
  36. Ikiwa hujui kufa,tazama kaburi.If you don't know death look at the grave.
  37. Jina jema hungara gizani.A good name shines in the dark.
  38. Jino la pembe si dawa ya pengo.An ivory tooth is not cure for the lost tooth.
  39. Jitihadi haiondoi kudura. Effort will not counter faith.
  40. Jogoo la shamba haliwiki mjini. The village cock does not crow in town.
  41. Kafiri akufaye si Isilamu asiyekufa.An infidel who does you good turn is not like a Muslim who does not
  42. Kamba hukatika pabovu. A rope parts where it is thinnest.
  43. Kanga hazai ugenini.A guine- fowl not lay eggs on strange places
  44. Kawaida ni kama sheria.Usage is like law
  45. Kawia ufike.Better delay and get there.
  46. Kazi mbaya siyo mchezo mwema.A bad job is not as wothless as a good game
  47. Kelele za mlango haziniwasi usingizi.The creaking of the door deprives me of no sleep.
  48. Kenda karibu na kumi.Nine is near ten.
  49. Kiburi si maungwana.Arrogance is not gentlemanly.
  50. Kichango kuchangizana.Everyone should contribute when collection is made.
 
  1. Kidole kimoja hakivunji chawa.One finger canot kill a louse.
  2. Kingiacho mjini si haramu.That is fashionable in town is never prohibited.
  3. Kikulacho ki nguoni mwako.That which eats you up is in your clothing.
  4. Kila chombo kwa wimblile.Every vessel has its own waves
  5. Kila mlango na ufunguwo wake.Every door with its own key
  6. Kila mtoto na koja lake.To every child his own neck ornament
  7. Kila mwamba ngoma ,ngozi huivuta kwake.Every who streches a skin on a drum,pulls the skin own his own side.
  8. Kila ndege huruka na mbawa zake.Every bird flies with its own wings.
  9. Kilio huanza mfiwa ndipo wa mbali wakaingia.The beareved begins the wailing latter others join.
  10. Kimya kingi kina mshindo mkubwa.Along silence followed by mighty noise.
  11. Kinga na kinga ndipo moto uwakapo.One fire brand after another keeps fire burning.
  12. Kinyozi hajinyoi.A barber does not shave himself.
  13. Kinywa ni jumba la maneno.Mouth is the home of words.
  14. Kipendacho moyo ni dawa.What the heart desires is medicine to it.
  15. Kipya kinyemi ingawa kidonda. A new thing is a souce of joy even if is sore.
  16. Kisebusebu na roho kipapo.Refusing and wanting at the same time.
  17. Kisokula mlimwengu,sera nale.what is not eaten by a man,let the devil eat it.
  18. Kitanda usicho kilala hujui kunguni wake.You canot know the bugs of a bed that you have not lain on.
  19. Kivuli cha fimbo hakimfichi mtu jua.Shadow of a stick canot protect one from the sun.
  20. Kiwi cha yule ni chema cha;hata ulimwengu uwishe. The blindnes of that one is his good fortune
  21. Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza.A good thing sells it self a bad one advertises it self
  22. Konzo ya maji haifumbatiki. A handfull of water can not be grasped.
  23. Kosa moja haliachi mke.One fault does not warrant divorce of a wife
  24. Kozi mwandada ,kulala na njaa kupenda.A goshawk is an egg child,if sleeps hungry its his own fault.
  25. Kuagiza kufyekeza. ie One eye of a master sees more than four of a servent.
  26. Kuambizana kuko kusikilizana hapana.Giving advice but no one listens.
  27. Kucha M'ngu si kilemba cheupe.The fear of God is not wearing a white turban.
  28. Kuchamba kwingi,kuondoka na mavi.Leave well alone! You wont improve matters by going on tinkering
  29. Kufa kufaana.Death has its advantages too ie it benifits those who inherit.
  30. Kufa kwa jamaa, harusi.The death of not a relative is a wedding.Compared to a death of a relative
  31. Kufa kwa mdomo,mate hutawanyika.When the head of the family dies,that family breaks up.
  32. Kuishi kwingi ni kuona mengi. To live long is to see much.
  33. Kujikwa si kuanguka,bali ni kwenda mbele.To stumble is not falling down but it is to go forward.
  34. Kukopa harusi kulipa matanga.Borrowing is like a wedding ,repaying is like mourning.
  35. Kuku havunji yai lake.A hen does not break her own eggs.
  36. Kuku mgeni hakosi kamba mguuni.A new fowl always has string around its legs.
  37. Kula kutamu ,kulima mavune.Eating is sweet ,digging is weariness.
  38. Kulea mimba si kazi kazi kulea mwana.It is not hard to nurse a pregnency,but it is hard to bring up a child.
  39. Kunako matanga kume kufa mtu.Where they is mourning someone has died.
  40. Kunguru mwoga hukimbiza mbawa zake.The timid crow withdraws his wings from harm.
  41. Kupanda mchongoma ,kushuka ngoma.You may climb a thorn tree,and be unable to come down.
  42. Kupoteya njia ndiyo kujua njia.To get lost is to learn the way.
  43. Kutoa ni moyo usambe ni utajiri.Charity is the matter of the heart not of the pocket.
  44. Kutu kuu ni la mgeni.Old rust is for the stranger.
  45. Kuzima koleo si mwisho wa uhunzi.Cooling the tongs is not end of forging.
  46. Kwa mwoga huenda kicheko na kwa shujaa huenda kilio.i.e.timidity often ends in a laugh, bravado in a lament.
  47. Kwenda mbio siyo kufika.To run is not neccessarily to arrive.
  48. Kwenye miti hakuna wajenzi.Where there trees,there are no builders.
  49. La kuvunda(kuvunja) halina rubani. A vessel running agroud has no captain.
  50. La kuvunda (kuvunja)halina ubani.They is no incence for something rotting.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom