Kiswahili: Methali, Vitendawili, nahau, Misemo n.k

Haba na haba hujaza kibaba
Adhabu ya kaburi aijuaye maiti
Ganda la mua la jana chungu kaona kivuno
Heri kufa macho kuliko kufa moyo
Mwamba ngoma ,ngozi huivuta kwake
Kutoa ni moyo usambe ni utajiri
Hii ganda la mua la jana chungu kaona kivuno mimi sjui inamaanisha nini,naomba mnifasirie sababu nimeiona na kuisika muda mrefu lakini sijui chungu ninani na kivuno ninini,sawa na ridhiki mafungu saba,mi nafuatisha semi tu kakini sjui maana.Nisaidieni jamani!
 
Nyingine hizi hapa:
  1. Papo kwa papo, kamba hukata jiwe
  2. Ndugu chungu, jirani mkungu
  3. Mwenye njaa hana miiko
  4. Mume wa mama ni baba
  5. Mtembezi hula miguu yake
  6. Mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba
  7. Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe
  8. Mjinga akierevuka mwerevu yupo mashakani
  9. Mchama ago hanyeli,huenda akauya papo
  10. Jino la pembe si dawa ya pengo

Nimeipenda sana hiyo iliyo na red color.
 
Hizi ni za Kinyamwezi. Sijui kama nazo twaziandika.

1. Kilichouwa kazi nachenyewe ni kazi (methali ya kivivu).
2. Simba na simba hawaumani.
3. Kupangusa (vimchuzi kwenye chungu) si sawa na kula mkavu.
4. Amulikaye (kurunzi) huanzia miguuni kwake.
5. Kula kwa mtoto wa mbwa, kuko miguuni.
6. Ukimfunda (mtoto) aliyefundika, utajisifu ufundaji.
7. Uzuri wa Nkuwa (tunda) ndani kuna mdudu.

Hii ni ya KIGOGO:
1. Myujiyuji, mti wa lulengo si wa kukata zengo (Myujiyuji, ni mti mzuri sana ila haufai kujengea).
 
Sidhani kama hiyo ndio maana ya msemo huo.

Wataalam wengine wameeleza msemo huo kumaanisha chagua moja, kujisafisha sana au nusu nusu uondoke na uchafu. Na sio ``uchafu ni uchafu tu,`` hata ukifanya usafi hausafishiki, la hasha. Sugua kadri uwezavyo.


mimi najua kuchamba kwingi mwisho utatoka na mavi maana yake unachokono saaana mambo ambao huyaju ukiyajua yanaweza kukutapisha bora usiyachokonoe jua kile unachopashwa kujua tu.

ukiumchunguza bata anachokula hutamla.

au usilolijua ni kama usiku wa giza.

aisifuye mvua imemyea; pole pole ndio.................
 
Kiswahili chaenda kikipanuka na kukua kila siku.... hivi kuna nahau gani mpya isije ikawa tuna zilezile za zamani tu ...pia tutofautishe nahau na methali...........tujuzeni wajuzi wa kiswahili.
Asanteni
 
mh, mada ngumu!! kiswahili kwa wengi enzi za O level kilikua chanzo cha penati kwenye divisions

kuna semi, nahau, methali na hapo ndio mtihani unaanza... let alone tanakali, takriri, tashtiti na mengineyo

mwe!
 
mh, mada ngumu!! kiswahili kwa wengi enzi za O level kilikua chanzo cha penati kwenye divisions

kuna semi, nahau, methali na hapo ndio mtihani unaanza... let alone tanakali, takriri, tashtiti na mengineyo

mwe!

kuna ngeli za majina, vihisishi, mofimu, misimu, viwakilishi, viunganishi, duh kweli kiswahili kiboko....
 
kuna ngeli za majina, vihisishi, mofimu, misimu, viwakilishi, viunganishi, duh kweli kiswahili kiboko....
gademu... Umenikumbusha mbali sana preta... Merci! Arusha yenu mvua tupu na tope kiatu kimekua raizoni
 
gademu... Umenikumbusha mbali sana preta... Merci! Arusha yenu mvua tupu na tope kiatu kimekua raizoni

ha ha ha...pole na karibu sana...hii mvua imetukatili lakini tunafurahi kwa kupata neema hii....karibu utembelee na huku Yaeda...nyanyi wameongezeka sana msimu huu
 
ha ha ha...pole na karibu sana...hii mvua imetukatili lakini tunafurahi kwa kupata neema hii....karibu utembelee na huku Yaeda...nyanyi wameongezeka sana msimu huu
Na'as desi... But t'laau
 
Kwa wale ambao wanajiuliza nahau ni nini...nahau kwa Kiingereza ni idiomatic expression....
 
Nimeanza kusahau haya mambo hebu mwageni somo tujifunze kwa upya elimu haina mwisho
 
Asiyejua maana haambiwi maana.

Kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi

kusema ukweli vinanichanganya kati ya nahau, methali na misemo.

Fuata nyuki ule asali

tembea uone
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom