Tujikumbushe kijarida cha TANU NA RAIA kilichoandikwa na Nyerere 1962 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujikumbushe kijarida cha TANU NA RAIA kilichoandikwa na Nyerere 1962

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpaka Kieleweke, May 31, 2012.

 1. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2012
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Katika utangulizi wake kuna maneno yanasema "Binadamu wanapofanya umoja wa aina yo yote huwa wanayo shabahaya kuunda umoja huo.Pengine ni umoja wa kujipatia elimu , au wa kufanya biashara,au wa kucheza ngoma,au kuimba nyimbo,au kwenda kumzika jirani ,n.k .Vitendo vyao vyote huwa vina shabaha ile moja ,yaani kusudi la kuunda umoja huo vitendo vyao vizuri ni vile vinavyosaidia kuitimiza shabaha yao na vibaya ni vile ambavyo vinapinga kutimizwa kwa shabaha yao havihusiani kabisa na kutimizwa kwa shabaha hiyo"

  anaendelea kusema kuwa " sisi tulipounda TANU shabaha yetu kubwa ilikuwa kuondoa serikali ya kikoloni katika nchi yetu , vitendo vyetu vilikuwa vikisaidia kutimiza shabaha yetu ya UHURU........'


  Nilipokuwa nasoma hapa nikajiuliza ,hivi shabaha ya CCM ni nini?
  vitendo vyao vinalenga kuifikia shabaha hiyo?
  Kuna mtu anaijua shabaha ya CCM leo?
  Umoja wao upo?Umeunganika ama viungo vingine vimekufa ? Na kama viungo vimekufa wana haja ya kuwepo ? ama watazikwa lini? Nani wa kuwazika hawa?

  Tutafakari pamoja ...
   
 2. M

  Mr.Busta JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 672
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  baada ya shabaha ya kumwondo mkoloni kufanikiwa hawakuka chini kutengeneza shabaha nyingine ndio maana hawajielewi hadi kusababisha ufisadi n.k
   
 3. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  prof shivji anakuambia kuwa ccm iliitwa chukua chako mapema toka ilipoundwa 1977.
  maanqa yake ni kuwa ilionekana haina shabaha.
   
 4. b

  bdo JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,712
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  shabaha yao ya sasa ni kuiachia NGUVU YA UMMA itawale,
   
 5. m

  matawi JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Aise wewe kweli umetafakari hawa jamaa hawana mbele wala nyuma
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Imani ya Tanu

  SIASA YA TANU NI KUJENGA NCHI YA UJAMAA, MISINGI YA UJAMAA
  IMETAJWA KATIKA KATIBA YA TANU, NAYO NI HII


  Kwa kuwa TANU inaamini:-

  (a) Kwamba binadamu wote ni sawa;
  (b) Kwamba kila mtu anastahili heshima;
  (c) Kwamba kila raia ni sehemu ya Taifa na anayo haki ya
  kushiriki sawa na wengine katika Serikali tangu ya Mitaa, ya
  Mikoa hadi Serikali Kuu;
  (d) Kwamba kila raia anayo haki ya uhuru wa kutoa mawazo
  yake, ya kwenda anakotaka, wa kuamini dini anayotaka na
  wa kukutana na watu mradi havunji Sheria;
  (e) Kwamba kila mtu anayo haki ya kupata kutoka katika jamii
  hifadhi ya maisha yake na ya mal i yake aliyonayo kwa
  mujibu wa Sheria;2
  (f) Kwamba kila mtu anayo haki ya kupata malipo ya haki
  kutokana na kazi yake
  (g) Kwamba raia wote kwa pamoja wanamiliki utajiri wa asili
  wanamiliki utajiri wa asili wa nchi hii ukiwa kama dhamana
  kwa vizazi vyao;
  (h) Kwamba ili kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unakwenda
  sawa Serikali lazima iwe na mamlaka kamili juu ya njia
  muhimu za kuukuza uchumi; na
  (i) Kwamba ni wajibu wa Serikali, ambayo ni watu wenyewe,
  kuingilia kati kwa vitendo maisha ya uchumi ya Taifa ili
  kuhakikisha usitawi wa raia wote na kuzuia mtu kumnyonya
  mtu mwingine au kikundi kimoja kunyonya kikundi kingine
  na kuzuia limbikizo la utajiri kufikia kiasi ambacho hakipatani
  na siasa ya watu wote kuwa sawa.
  MADHUMUNI YA TANU
  Kwa hiyo basi, makusudi na madhumuni ya TANU yatakuwa kama
  hivi yafuatavyo:-
  (a) Kuudumisha uhuru wa nchi yetu na raia wake;3
  (b) Kuweka heshima ya mwanadamu kwa kufuata barabara
  kanuni za Tangazo la Ulimwengu la Haki za Binadamu.
  (c) Kuhakikisha kwamba nchi yetu inatawaliwa na Serikali ya
  watu ya kidemokrasia na ya kisoshalist;
  (d) Kushirikiana na vyama vyote vya siasa katika Afrika
  vinavyopigania uhuru wa bara lote la Afrika;
  (e) Kuona kwamba Serikali inatumia mali yote ya nchi yetu kwa
  kuondoshea umaskini; ujinga na maradhi;
  (f) Kuona kwamba Serikali inasaidia kwa vitendo kuunda na
  kudumisha vyama vya ushirika;
  (g) Kuona kwamba kila iwezekanapo Serikali inashiriki hasa
  katika maendeleo ya uchumi wa nchi yetu;
  (h) Kuona kwamba Serikali inatoa nafasi zilizo sawa kwa wote,
  wake kwa waume, bila kujali rangi, kabila, dini au hali;
  (i) Kuona kwamba Serikali inaondoa kila namna ya dhuluma,
  vitisho, ubaguzi, rushwa na upotofu;4
  (j) Kuona kwamba Serikali ya nchi yetu inasimamia barabara
  njia kuu za kuzalisha mali na inafuata siasa ambayo
  itarahisisha njia ya kumiliki kwa jumla mali za nchi yetu;
  (k) Kuona kwamba Serikali inashirikiana na dola nyingine katika
  Afrika katika kuleta Umoja wa Afrika.
  (l) Kuona kwamba Serikali inajitahidi kuleta amani na salama
  ulimwenguni kwa njia ya Chama cha Umoja wa Mataifa.5
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mpaka Kieleweke, unaweza kutuwekea hapa hicho kijarida? Shukran
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...