Tujikumbushe kichekesho cha dunia: Yanga vs Ndanda FC 2016

njaakalihatari

JF-Expert Member
Feb 12, 2019
4,084
8,663
Tuesday , 10th May , 2016

Mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara kati ya wenyeji Ndanda FC na Yanga uliokuwa ufanyike Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara sasa utafanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi.

yanga-5.jpg

Afisa habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Alfred Lucas amesema, Bodi ya Ligi imeridhia maombi hayo mara baada ya Ndanda na Yanga kushawishiana na kufikia makubaliano ya mchezo huo ambao hapo awali ulitakiwa kuchezwa Mei 15 baadaye ukarudishwa mpaka Mei 14 na wakaamua tena uchezwe Mei 13 Uwanja wa Nang'wanda mjini Mtwara lakini hivi sasa rasmi utachezwa Mei 14 Uwanja wa Taifa.

Lucas amesema, makubaliano hayo yameafikiwa baada ya timu ya Yanga kuiomba Ndanda FC mechi ichezwe Dar es Salaam kwa sababu wanataka kuwahi Angola Mei 17 kucheza na wenyeji Sagrada Esperanca katika mchezo wa marudiano wa mchujo wa kuwania kwenda hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.

Lucas amesema, Ndanda wamekubali kucheza mechi zote mbili za msimu na Yanga ugenini, kwa sababu hawana cha kupoteza wala kupata zaidi katika Ligi Kuu ilipofikia ukingoni.

Katika mchezo huo, Yanga itakabidhiwa Kombe lake la ubingwa wa Ligi Kuu iliyojihakikishia Jumapili baada ya Simba SC kufungwa bao 1-0 na Mwadui FC katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa upande mwingine Lucas amesema, mechi za mwisho za kufunga dimba la Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara zilizotakiwa kupigwa Mei 21 mwaka huu zimesogezwa mbele kwa siku moja na zitachezwa Mei 22 mwaka huu ili kuipa Yanga nafasi ya kuweza kupumzika atakapotokea kutoka nchini Angola.

Lucas amesema, Yanga wanatarajia kukutana na Esperanca Mei 17 mwaka huu na Mei 21 ndio zilikuwa zichezwe mechi za kufunga pazia la Ligi ambapo Yanga ingetakiwa kusafiri mpaka Songea kucheza dhidi na Majimaji hivyo bodi ya Ligi ikaridhia kuwa michezo yote imalizike Mei 22 mwaka huu ili kuipa Yanga nafasi ya kuweza kupumzika.

Kanuni zinasemaje
baada ya tarehe 3 wakishahshushwa daraja kwa kugomea mechi ya simba watenda cas huko wataenda kutunishiana misuli na jamhuri ya muungano wa Tanzania watazijua kanuni vizuri..wao ndo mabingwa wa kanuni labda watatueleza hiyo kanuni ya kucheza mechi ya ndanda dsm ilikuwa ni nini?
 
Karia ashajua wazi hahitajiki pale, hata Yanga ikigoma, hana ubavu huo. Yanga ni zaidi ya unavyojua.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
baada ya tarehe 3 wakishahshushwa daraja kwa kugomea mechi ya simba watenda cas huko wataenda kutunishiana misuli na jamhuri ya muungano wa Tanzania watazijua kanuni vizuri..wao ndo mabingwa wa kanuni labda watatueleza hiyo kanuni ya kucheza mechi ya ndanda dsm ilikuwa ni nini?
Umesema wameridhiana kati ya Yanga na Ndanda kucheza mcheza mchezo wao Dsm.
Swali kwako je hao wamridhiano yalifanyika siku moja kabla ya mchezo ama ni siku kadhaa kabla ya tarehe ya mchezo?

Tukija kwenye Derby

Je mpaka sasa imetolewa sababu ipi ya kusogezwa ghafla mchezo wa derby tena kwa masaa machache mechi kuanza.

Nani aliyewajibishwa mpaka sasa kwa kitendo hicho cha kuvunja kanuni hiyo ya kutoa taarifa masaa 24 kabla ya tarehe ya mechi.
 
Back
Top Bottom