Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 18,657
- 22,254
Mwishoni mwa miaka ya 50 Mwalimu Nyerere alishitakiwa na wakoloni na akafikishwa mahakamani, siku za kusikilizwa kesi watanganyika walijaa nje ya mahakama kushuhudia tukio hilo muhimu la kiongozi wao kusurubiwa na mkoloni. Enzi hizo jeshi la polisi lilikuwa chini ya malkia wa uingereza na lilikuwa likipokea amri toka huko, cha ajabu hawakuonekana polisi wakipiga jalamba wala kuwabughuzi raia waliofika mahakamani! Hata Mwalimu aliposhinda kesi na alipotoka nje ya mahakama alibebwa mbele ya polisi waliokuwepo na hawakuwabughuzi wananchi hao licha ya enzi hizo kuwa za ubaguzi.