Tujikumbushe : Jaji Warioba alivyomueleza Profesa Shivji waziwazi kuwa si mkweli na ni kugeugeu na mpotoshaji

Mwendawazimu peke yake ndiye hawezi kuona umhimu wa katiba mpya, watu kama akina shivj na kabudi niwa kupuuzwa Sana.
Mateso ya jasho na damu tuliyo pitia awamu ya tano ni kipimo tosha kuwa tuna ulazima wa katiba mpya kwa mstakabali wa Tanzania yetu

Mateso gani mkuu. Wewe na Nani? Ni Wale kumi waliofanya sherehe au mamilioni waliolia na kusaga meno?
 
Linapokuja swala la Muungano basi inshu ya katiba mpya inakuwa ngumu sana.kwa iyo ni bora wanasiasa wetu waachane na hii inshu ya Muungano.
 
Na huo ndio ukawa mwanzo wa kunyanyuka kwa Bashite, kuwa mkuu wa wilaya!

Dunia ina mambo kweli!

Msidanganyike, Bashite alitumwa na genge la Kikwete na Samuel Sitta kumvuruga jaji Warioba!! Laana hiyo haitamuacha salama mpaka kaburini!!!
Baada ya Sitta kufa nae Bashite akamgeuka Kikwete kwa kumuorodhesha mwanae kama muuza Ngada!!!!
 
Tusimlaumu Prof shvji Labda uzee nao unachangia......

Sidhani kama ni uzee bali huyo mzee anatumika. Nakumbuka wakati wa mchakato wa katiba mpya 2012-2015 kuna wakati Prof. Shivji aliandaliwa vipindi kwenye redio na TV na serikali, mada alizokuwa anaziendesha zilikuwa na mwenendo wa upotoshaji kuonyesha katiba mpya sio muhimu, bali iliyopo ni ya kupigwa viraka tu. Vipindi hivi vilienda tofauti kabisa na misimamo yake ya awali ya katiba mpya ya wananchi, na kuacha mshangao kwa wengi waliokuwa na imani kwake. Walichofanya serikali ya JK wakati huo ni kumtumia yeye kufifisha suala la katiba mpya, kwani yeye ni mmoja ya watu walioaminika na watanzania kuhusu mchakato huo. Walichofanya system iliyokuwa chini ya JK ni kile waswahili wasemacho "mchawi mpe mwana amlee" Na kwa kiwango fulani walifanikiwa. Na isingekuwa kuwa hitaji la hii katiba mpya ni la wakati, basi wangeweza kubadili kabisa mitazamo ya wananchi walio wengi.
 
Source: Warioba amshukia Prof Shivji | Mwananchi

Dar es Salaam. Mjadala wa Mabadiliko ya Katiba jana ulihamia nje ya Bunge wakati Jaji Joseph Warioba alipomchambua mhadhiri maarufu nchini, Profesa Issa Shivji akimueleza kuwa si mkweli bali mpotoshaji wa Rasimu ya Katiba.

Jaji Warioba, ambaye ni mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, pia amemtuhumu Profesa Shivji kuwa ndiye mwanzilishi wa chokochoko za Zanzibar za kudai serikali tatu, jambo ambalo sasa analigeuka kutokana na kuona hali imekuwa mbaya.

Kauli ya Warioba imekuja baada ya Profesa Shivji kuichambua Rasimu ya Katiba jana asubuhi kwenye Kongamano la Vijana lililoandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo lililokuwa na dhima ya Vijana Katika Kuimarisha na Kuendeleza Muungano Baada ya Miaka 50. Tamasha hilo lilifanyika kwenye hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Plaza jijini Dar es salaam.

Akiwasilisha mada kwenye kongamano hilo, Profesa Shivji alisema katika kujadili Muungano, wananchi hawana budi kuzingatia mambo mawili ambayo ni nchi zinazozungumziwa kwenye Rasimu kuwa ni Zanzibar, Tanganyika au Tanzania, ambayo alisema haina mamlaka katika pande hizo mbili za Muungano.

Pia alisema suala la maadili kwa viongozi halina budi kuangalia kuwa linazungumzia maadili ya viongozi wa Zanzibar, Tanganyika au Tanzania na kwamba rasimu inazungumzia viongozi wa Tanzania ambao hawana mamlaka kwa Tanganyika na Zanzibar.

Katika majumuisho yake, Profesa Shivji, ambaye aliikosoa Rasimu kuwa haiwakilishi matakwa ya Watanzania kwa kuangalia sampuli zilizotumika, alisema kwamba wajumbe wa Tume ya Jaji Warioba walikuwa na nia njema.

Lakini Shivji akaenda mbali zaidi kwa kusema “the road to hell is paved in good intention,” akimaanisha kuwa njia ya kuzimu imetengenezwa kwa nia njema.

Akijibu hoja hizo, Jaji Warioba alisema Profesa Shivji amegeuka maandishi yake yaliyokuwa yanachochea utaifa wa Zanzibar na sasa anaona Tanganyika ndiyo hatari kwa Muungano.

“Shivji ni msomi na mimi najua anaelewa matumizi ya takwimu,” alisema Jaji Warioba, ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wakati alipozungumza na gazeti hili nyumbani kwake jana jioni. “Nasema hapa, Shivji akiwa msomi, amekuwa intellectually dishonest (si mkweli kiusomi). Anapotosha kwa makusudi.”

Jaji warioba alisema Shivji ndiye amekuwa chanzo cha uchochezi wa kitaifa Zanzibar kupitia maandishi yake. Alisema waliokuwa wanadai serikali tatu kwa muda mrefu walikuwa wananchi wa Zanzibar.

“Shivji alikuwa anasema Tanganyika imejificha kwenye Muungano ili inufaike. Kwa hiyo anasema Tanganyika iwe wazi isijifiche,” alisema Jaji Warioba.

“Na Shivji amechochea hilo… wote wale waliokuwa wanamnukuu walikuwa wanatoa hayo kwenye maandishi yake na kwamba mpaka leo hii kuna watu wa Zanzibar wanaamini Muungano huu si halali kisheria kutokana na Shivji ambaye alisema Baraza la Mapinduzi halikuridhia articles (ibara) za Muungano.”

Alipoulizwa jana usiku kuhusu tuhuma hizo za uchochezi na chanzo cha hisia za utaifa wa Uzanzibari na Utanganyika, Profesa Shivji alisema hawezi kujibu tuhuma hizo kwa kuwa hajamsikia Jaji Warioba akizungumzia hilo.

“Hey, amezungumza lini?” alihoji. “Siwezi kujibu kwa kuwa sijamsikiliza mwenyewe.”
Lakini Jaji Warioba alisema watu walitumia msingi huo kudai utaifa wa Zanzibar na kusisitiza kuwa Shivji amesababisha hisia za utaifa na kwamba haya yanayoendelea sasa yanatokana uchochezi huo.

“Hata kabla ya sisi kuanza mchakato huu, Shivji alikwenda Zanzibar akazungumza na Baraza la Wawakilishi na akawaambia issue kwa Zanzibar ni self determination (kujitambua), Sasa leo anaona kama hatari ni Tanganyika, lakini yeye ndio amechochea nationalism (utaifa),” alisema Jaji Warioba.

Kuhusu takwimu, Jaji Warioba alisema mara ya kwanza Profesa Shivji alizungumzia takwimu za Zanzibar kuhusu muundo wa Muungano akisema kuwa waliozungumzia suala hilo walikuwa 47,000, huku watu 27,000 wakitoka Tanzania Bara na 19,000 kutoka Zanzibar.

“Safari hii ametaja zile za Tanzania Bara na kusema hiyo ni figure (namba) ndogo sana ukilinganisha na watu 300,000 waliotoa maoni,” alisema Warioba.

Alisema Tume ilitumia takwimu zinatokana na watu waliozungumzia suala ambalo wameliwekea asilimia na si kwa ujumla na ndio maana anaona Profesa Shivji anataka kupotosha kwa makusudi.

Warioba alimuelezea Profesa Shivji kuwa sasa ameamua kueneza propaganda za serikali mbili kwa kuponda Rasimu ya Katiba ambayo inaonyesha kuwa muundo wa serikali tatu ndio unaoifaa Tanzani kwa sasa. Aidha, Warioba alisema msimamo wa Profesa Shivji ni kwamba Zanzibar haikukosea kubadilisha Katiba mwaka 2010.

“ Nimeshangazwa na Shivji kusema kwamba kitendo cha Zanzibar kubadili Katiba yao kuwa ‘Zanzibar ni Nchi’ halikuwa jambo la ajabu,” alisema Warioba.

Alisema Shivji ni msomi ambaye anafahamu kitendo cha kubadilisha Katiba kilikuwa na madhara makubwa katika muundo wa Muungano.

“Nadhani mnakumbuka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipoulizwa Bungeni kama Zanzibar ni nchi au siyo nchi, alijibu kuwa Zanzibar siyo nchi, vurugu zake mnakumbuka,” alisema.

Alisema lakini msomi kama Shivji haoni kama suala hilo la ‘Zanzibar ni nchi’ lina madhara makubwa katika mstakabali wa taifa letu.
Jaji Warioba alisema kama serikali tatu hazitakiwi, basi kinachotakiwa kufanywa ni kwa Zanzibar kubadili Katiba yake ili iseme kwamba Zanzibar ni sehemu ya Muungano, vinginevyo haiwezekani.

“Maana kama ni kusahihisha, ni lazima kwanza Katiba ya Zanzibar itumie maneno yale yale yaliyo kwenye Katiba ya Muungano. Yaani Zanzibar iwe sehemu ya nchi. Zanzibar wakubali hilo,” alisema.

“Zanzibar wakubali Rais wa Muungano ana madaraka nchi nzima maana mabadiliko ya 2010 yamemuondolea Rais wa Jamhuri ya Muungano madaraka yake.”

Akitoa mfano wa mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, Jaji Warioba alisema amekuwa akidai takwimu hazionyeshi uhalisia wa maoni ya wananchi.

“Kwa mfano, Jimbo la Simanjiro linakuwa na watu 100,000 lakini waliojiandikisha kupiga kura ni watu 20,000 na waliopiga kura ni watu 15,000. Hii ina maana ushindi wake utakuwa katika watu waliopiga kura na siyo idadi ya watu wa Simanjiro,” alisema Warioba
Shivji ni miongoni mwa wazee wanailipwa kwa minajiri ya kuendeleza usaliti ktk taifa hili. Group lake na wengine kazi zao ni kupinga misingi ya maendeleo kwa kufeva mabwana zao. Wanatumia umaarufu wao ku whitewash uozo wa serikali na chama.
 
Huo ndio ukweli japo unakera. Nenda hata kwenye jamii ya Kiasia ukweli huu utauona. Mfano mrahisi kama utakuwa huongozwi na unafiki, waasia wanazaliwa na kukulia hapa hapa nchini, umeona wakioona na wabantu? Unadhani jambo hilo ni bahati mbaya?
Kweli. Hata wale waliopo tangu kabla ya uhuru huoni wakufanya hivyo. Wahindi jamani khaa! wanashindwa na wazungu
 
Kabudi anatetea meza kulingana na sahani yake ya chakula iko meza gani kwa wakati huo. .

Alipokuwa mjumbe wa tume ya katiba alikuwa anatetea katiba kwa nguvu. Leo ni waziri wa katiba na sheria anaipinga katiba.

Huyu ni mnafiki, siyo mtu wa kumchukulia serious.

Ni wa kupuuzwa
 
Kweli. Hata wale waliopo tangu kabla ya uhuru huoni wakufanya hivyo. Wahindi jamani khaa! wanashindwa na wazungu

Kabisa, tena wangalau wanaume wao huweza kuzaa na wanawake wa kibantu na sio kwa mapenzi au ndoa, bali bahati mbaya kutokana na hamu za mwili. Lakini hakuna uwezekano binti wa Kiasia kuzaa na mbantu, hilo halipo kabisa. Wazungu hawana tatizo bali huzaa na yoyote.
 
Hawa wanazuoni waliotoka pale UDSM wametuharibia taswira nzima ya usomi; Mwakyembe, Shivji, Bashiru, Kitila, Kabudi, Uforo nk.
Kuna haja ya kuja kugeuza makaburi yao kuwa sehemu ya watu kwenda kujisaidia haja ndogo.
 
Kosa linakuja kwa wasomi wetu kuwa wanasiasa.hapa ndipo wanashindwa kutofautisha siasa na usomi
 
Sidhani kama ni uzee bali huyo mzee anatumika. Nakumbuka wakati wa mchakato wa katiba mpya 2012-2015 kuna wakati Prof. Shivji aliandaliwa vipindi kwenye redio na TV na serikali, mada alizokuwa anaziendesha zilikuwa na mwenendo wa upotoshaji kuonyesha katiba mpya sio muhimu, bali iliyopo ni ya kupigwa viraka tu. Vipindi hivi vilienda tofauti kabisa na misimamo yake ya awali ya katiba mpya ya wananchi, na kuacha mshangao kwa wengi waliokuwa na imani kwake. Walichofanya serikali ya JK wakati huo ni kumtumia yeye kufifisha suala la katiba mpya, kwani yeye ni mmoja ya watu walioaminika na watanzania kuhusu mchakato huo. Walichofanya system iliyokuwa chini ya JK ni kile waswahili wasemacho "mchawi mpe mwana amlee" Na kwa kiwango fulani walifanikiwa. Na isingekuwa kuwa hitaji la hii katiba mpya ni la wakati, basi wangeweza kubadili kabisa mitazamo ya wananchi walio wengi.
Tatizo ni kuwa tumeandaliwa hivi karibuni kutukana tusiopenda mawazo yao badala ya kuyaheshimu lakini tukajenga hoja bila kuchoka kuwapinga kistaarabu. Na sisi tunaoitaka katiba mpya tunachelewa kwa kutukana wapinzani wetu badala ya kumwaga hoja popote ili hoja zetu zitawale hadi watawala wazichukue. Kwangu mimi kwa ufupi sana mada muhimu ni mbili. Kubwa kabisa ni kuwa na katiba mpya. Inayofuata ni madaraka ya serikali ya muungano na vishawishi kwa serikali zingine yanayohakikisha kutovunjika kwa muungano. Mjadala wa serikali mbili au tatu haulingani na hayo mawili kwa umuhimu. Akina Warioba walifanya kazi nzuri, lakini waliiharibu kwa kuifanya serikali ya tatu, yaani ya muungano, kuwa dhaifu sana kwenye rasimu yao. Hilo tu. Katiba ya sasa ni mbaya sana kwa jambo lililo wazi, ni ya madikteta! Tuwashukuru viongozi wa awamu nne za kwanza kuwa walituhurumia huku wakiwa na mfumo wa kidikiteta. Sasa tumeshajua ubaya wa kutegemea huruma ya kiongozi. Tutengeneze katiba isiyo na udikiteta!
 
Shivji ni miongoni mwa wazee wanailipwa kwa minajiri ya kuendeleza usaliti ktk taifa hili. Group lake na wengine kazi zao ni kupinga misingi ya maendeleo kwa kufeva mabwana zao. Wanatumia umaarufu wao ku whitewash uozo wa serikali na chama.
asanteni kwa kumuanika hadharani
 
Nooooooo
Hiki kizee cha kihindi hiki kishenzi Sana. Kwanza kirudi kwao kule kwao kule India kulikojaa umaskini na taka kibao.

Wengi walikishangaa kugalauka galauka. Kimechapisha machaposho mengi sana kikielezea ubovu wa katiba na uharamu wa muungano wetu huku kikipigia chapuo serikali tatu. Lkn kinaongea utopolo.
!Usianzishe hayo!
 
Back
Top Bottom