Tujikumbushe ilikuwaje ulipopokea tokeo la form 4

dtj

JF-Expert Member
Nov 29, 2014
1,332
1,375
Wakuu... Tujikumbushe lini na wapi ulipokea tokeo lako na ilikuaje... Hehehe
Mimi nlipokea langu nkiwa nimelala jamaa akanivutia waya tokeo limetoka. kwenda kucheki kitu cha 3 ya naniiii basi roho kwatuuuuuu....... wewe ilikuaje??
 
Nilikuwa mitaani mama wakambo na mdingi hawakuamini ilibidi waende shuleni kabisa wakakuya mzigo wa 2 nilifurahi saana ukizingatia maisha niliyokuwa naishi yalikuwa magumu balaa,nikajiunga na Lutheran Junior Seminary,nihayo tu
 
Mie ilikuwa home na pacha angu na mshikaji wetu mmoja hivi Feb 2008 mama akatupa simu tuangalie..pacha angu na mshikaji wetu wote wakawa wamepiga 1:11 kazi ikawa kwangu ilibidi nikajifungie na simu ndani nilipoangalia kukuta 2 kidooogo roho ikapoa ingawa sifa zilimwagika kwa pacha angu na mshikaji wetu mpaka roho ikawa inaniuma
 
Ilikua muda wa saa mbili usiku, siku ya Jumapili mwaka 2009, shangazi yangu alinipigia simu akaniambia hongera sana umepata division one, nilifurahi sana nikawa na amani tele moyoni.
 
mimi nilikua nasaidia wazazi kufanya biashara kuna ndugu yangu tulikua tunasoma wote ila yeye alikua A Level so wakati toleo linatolewa yy alikua hapo skuli then alinipigia cm kunipa taarifa nimefaulu vizuri sana aise
 
Sikuwa na wasiwasi wala hofu coz tangu Form 3 mitihani ya shule shule mm ndo namba 1 wao..naenda kuangalia matokeo nimepata div 3 ya mwisho(25) wiki nzima nilikuwa nalia, bahati nzuri nilichaguliwa coz nilikuwa na credit..mpk nimemaliza chuo sina imani na mitihani wala test
 
mmmmmmh!!,yaani humu wote mnajifanya mlipasua wakati wengine nawajua kabisa mmerisiti zaidi ya mara nne ndo mkapata credit,kweli jf ni noma,kila mtu anajifanya kafaulu,duuu!!
 
Ha ha ha....nikikumbuka naona aibu mwenyewe maana nilifanya kituko
Ni pm,sitomwambia Mtu,ntaitunza hiyo siri...
the best people now are the ones who did mistakes in the Past,
They still learned,those people ambao hawajafanya makosa au ujinga,Bado hakuna walichojifunza.
Still your the winner today,its a lessons to Us now from You ...Tatty
 
Ni pm,sitomwambia Mtu,ntaitunza hiyo siri...
the best people now are the ones who did mistakes in the Past,
They still learned,those people ambao hawajafanya makosa au ujinga,Bado hakuna walichojifunza.
Still your the winner today,its a lessons to Us now from You ...Tatty
Sio siri..ni jinsi tu nilivyoyapokea hayo matokeo ndio kichekesho.
zamani kupata matokeo ilikuwa issue kidogo sio kama sasa hivi kuna mitandao.
niliposikia matokeo yametoka nikaongozana na mama yangu kwenda kuangalia..pale SUA. Kuna mama mmojq alikuwa nayo..basi akaanza kunisomea matokeo akawa ananitajia masomo na grades nilizopata..cha kushangaza akawa ananitajia masomo ambayo mimi sikuyasoma..basi acha nitoe kilio cha nguvu..tena ofisini kwa watu. Yaani kilio haswaaaa.
baadae ndo nikapata matokeo yangu sahihi..hayakuwa mabaya lakini hayakuwa matarajio yangu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom