tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,114
Katika dunia ya sasa hakuna kitu kinaweza kupotea ili mradi kimewahi kutamkwa mbele ya jamii. Lakn pia tunaweza kupoteza vitu admu pale tu tutakaposhindwa kuweka kumbukumbu kwa vizazi vijavyo na vya sasa. Kwa kipindi kirefu tumekua na nukuu za Baba wa Taifa mwalimu nyerere. Ni wakati mwafaka kuweka kumbumbuku ya maneno mazuri ya mheshimiwa Rais Magufuli.

Duniani tuna nukuu (quotes) zawa watu maarufu kama Martn Luther king, Jr. Abraham lincoln na wengine wengi. Kwa hapa kwetu tuna nukuu za baba wa taifa mwalim Nyerere.

Sasa ni wakati mwafaka kuweka nukuu zake kwenye uzi huu. Usihofu iwe mbaya masikio mwako au iwe nzuri wewe weka tu maana lolote analo litamka mkuu wa nchi linapaswa kutunzwa.

Naweka maneno mawili matatu kuanzisha ukurasa wa maneno ya mkuu wetu.



''Mimi ni Rais wa maskini. Waliozoea kuishi kama malaika wataishi kama mashetani''.



''Serikali yangu haitawapa chakula. Kila mtu atabeba msalaba wake. Njaa haijaletwa na serikali''.

Hakuna serikali iliyowahi kujenga nyumba za wahanga duniani pote. Na sisi hatujengi.

''Hakuna kufanya za siasa mpaka 2020''.

''Siwezi kuwashirikisha wapinzani kwenye serikali yangu. Nakushangaa Shein kuwaingiza wapinzani''.




''Sijawahi kutamka Katiba kwenye kampeni zangu za kuomba urais. Katiba sio kipaumbele changu. Kwa sasa nainyoosha nchi kwanza''.

''Polisi mkukita mtu anaendesha gari kwenye njia ya mwendo kasi, ng'oa tairi uzeni''.

''Watoto watasomeshwa bure kwenye utawala wangu hivyo fyatueni watoto wengi maana watasoma bure''.




Haya ni machache kati ya mengi aliyowahi kuyaongea. Ni wakati mwafaka kuweka maneno yake hapa.
=========

TAZAMA VIDEOS ZA SPEECHES MBALIMBALI ZA RAIS MAGUFULI

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom