Tujikumbushe habari za magazeti ya Zamani

Kiresua

JF-Expert Member
May 13, 2009
1,184
259
Source (Yona Maro)

Wazee waombwa kumsaidia Mwinyi


MZALENDO, Jumapili, Novemba 3, 1985.


RAIS Nyerere amewaomba wazee nchini kumsaidia Rais mteule, Ndugu Ali
Hassan Mwinyi kama ambavyo walivyomsaidia yeye wakati wa kudai uhuru
na baada ya uhuru.

Mwalimu akizungumza na wazee wa mkoa wa Dar es Salaam katika sherehe
za kuagana nao zilizofanyika jana kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee,
mjini Dar es Salaam alisema mambo makubwa ya nchi ya kimaendeleo
yanayoanzishwa hayawezi kufanikiwa kama hayana baraka za wazee.

"Kama mlivyonisaidia mimi, msaidieni na mwenzangu. Anaihtaji sana
msaada wenu", alisema Mwalimu ambaye anastaafu Urais kesho kutwa
wakati Ndugu Mwinyi atakapoapishwa kuwa Rais wa Pili wa Jamhuri ya
Muungano.

Mwalimu ambaye katika hotuba yake alizungumzia kwa kirefu misaada
mbalimbali aliyopewa na wazee nchini wakati wa kudai uhuru, alieleza
kuwa pamoja na kuwa misingi mizuri imejengwa nchini, matazamio ya
wananchi ni makubwa jambo ambalo alisema linamfanya Ndugu Mwinyi awe
na kazi kubwa mbele yake.

Aliwashukuru kwa msaada, imani na kuelewa kwao mambo na ushirikiano
mzuri waliompa katika miaka 24 ya uhuru wa taifa na pia katika
harakati za kuutafuta. "Kila nilipotembea nchini wakati wa kudai uhuru
watu wa kwanza walionielewa walikuwa wazee", alisema.

Mwalimu aliwataka vijana nchini kuiga mfano wa wazee hao na pia
kufanya kazi za kujitolea ili kuliwezesha taifa kufikia hatua kubwa
zaidi ya kimaendeleo.

Akigusia mchango uliotolewa na vijana enzi za kudai uhuru ambao wengi
wao hivi sasa ni wazee, Mwalimu alisema Tanzania haiwezi kufanya
maendeleo makubwa bila vijana kufanya kazi za kujitolea.

Alisema vijana ndio wengi nchini ni wasomi na wana nguvu na kwamba
bila wao kutumiwa kwa kufanya kazi za kujitolea, maendeleo makubwa
hayawezi kufikiwa.

Mwalimu aliwakumbusha baadhi ya michango ya vijana wa zamani ya
kujitolewa iliyosaidia kupatikana kwa uhuru. "Kazi za vijana wa zamani
ilikuwa kufanya kazi za hiari kwa ajili ya TANU na kuimba, alisema.

Aliwataka vijana kuchagua kazi ambazo wanaweza kuzifanya kwa kujitolea
ili kusaidia taifa kufikia maendeleo makubwa zaidi.

Katika risala yao kwa Mwalimu, wazee hao walimpongeza Mwalimu kwa
uamuzi wake wa kustaafu na kumtaka wakati akiwa Mwenyekiti wa Chama
kufanya kila analoweza kukiimarisha Chama. "Chama ndicho
kilichotukomboa ... Chama ndicho kilichotukomboa... Chama ni baba na
mama", walisema wazee hao.

Miongoni mwa zawadi walizompa Mwalimu katika sherehe hizo ni baiskeli,
jembe, panga, kiti na mkongojo.

Leo Mwalimu atapokea maandamano makubwa ya walimu wa mkoa wa Dar es
Salaam yatakayoanzia Arnautoglu hadi Ikulu ambako ataagana nao.

Mapema jana Rais Nyerere alikabidhiwa rasmi "nishani ya Mkuu wa nchi"
kutoka Chama cha Kimataifa cha Klabu ya Misaada za Lions kutokana na
chama hicho kutambua mchango wa Mwalimu katika kuwasaidia binadamu.

Katika sherehe iliyofanyika nyumbani kwake Msasani, mjini Dar es
Salaam asubuhi, Mwalimu pia alikabidhiwa shilingi laki moja
atakazozitumia kwa ajili ya mradi wowote wa maendeleo jinsi
atakavyoona yeye katika eneo lolote nchini.

CHIPAKA AJIBU:
'Mtemvu toka wewe mimi sitaki'


Mwafrika, Alhamisi Juni 22, 1961


BWANA Lifa Chipaka alisema jana kwamba bado anaendelea na cheo chake
cha Mwenyekiti wa African National Congress. Ripoti iliyotolewa na
chama hicho juzi kusema Chipaka hatakiwi kwahiyo ajiuzulu aliita kuwa
ni ya uongo mtupu, wala haitambui.

Bwana Chipaka alidai kuwa hiyo Districk Committee iliyosemwa kuwa
imemfukuza kazi yeye haifahamu, wala hata kama iko yeye anafikiri kuwa
haiwezi kumtoa kazi Mwenyekiti wa chama cha Tanganyika nzima.

Akafyatuka, "Mtemvu lazima atoke yeye katika Congress maana ameharibu
jina la chama, alipokuwa akisafiri huko na huko ulimwenguni. Alipokuwa
China Mtemvu alijiita Waziri Mkuu wa Tanganyika", alisema Bwana
Chipaka. Hapo hapo akatoa bahasha ya barua kutoka China aliyoletewa
Mtemvu kwa cheo cha Waziri Mkuu wa Tanganyika.

Aliendelea, "Mimi nilikubaliana na Bwana Mtemvu kuwa niende Unguja,
mwenyewe akanipa barua nikampelekea Bwana Ali Muhsin. Nilifanikiwa
sana, ndiyo maana sasa Mtemvu ananionea gele.

"Nilipokuwa Unguja nilikuwa kama Mfalme, na sasa Mtemvu hapandezwi na
kufanikiwa kwangu huko na Mtemvu anashirikiana na Marijani ili
kuniangusha. Wala sipendelei Marijani awe Katibu wa Mtemvu.

Chipaka aliongeza, " Mtemvu alipokwenda nchi za Mashariki,
hakufanikiwa kama vile nilivyofanikiwa mimi Unguja. Alipewa vitu vingi
lakini aliporudi huku alijifanya kwamba vilikuwa zawadi alizopewa yeye
mwenyewe wala hazikutolewa kwa Congress.

Halmshauri Kuu ya chama ilikuwa ikikutana tangu Jumamosi ikimfikiria
Bwana Mtemvu, alisema Bwana Chipaka.

Akazidi kueleza, "Nilipokwenda Unguja nilimweleza Bwana Muhsin kuwa
sikuwa na kitu, akanipa senti fulani, lakini sasa wakina Mtemvu na
Omido wanavitaka hata visenti nilivyopewa Unguja nivitoe kwenye chama.
Lakini Mtemvu mwenyewe hakurudi na hata senti moja kutoka nchi za
Mashariki.

"Hawawezi kunitoa katika Congress kwa sababu wanachama wote wako
upande wangu nami nina kila ushahidi wa haya ninayosema. Hafai

Aliendelea, "Mtemvu hafai kwa uongozi, ndio maana Sanga aliacha chama
cha Congress. Katika barua yake ya kuacha kazi Sanga mwenyewe alisema
wazi kwamba yeye hawezi kuwa Katibu na Mtemvu kuwa Rais wa Congress,
aliona kwamba hawawezi kufanya kazi pamoja".

Naye Bwana Omido Katibu Mwenezi wa Congress alisema kwamba mashitaka
ya Bwana Chipaka hayana msingi wowote. Alisema kwamba jana usiku
habari ya Bwana Chipaka ilikuwa ikifikiriwa na Halmashauri Kuu ya
Congress.


Makaburu wadhibiti habari
Mzalendo, Jumapili, Novemba 3, 1985


JOHANNESBURG, Afrika Kusini


UTAWALA wa makaburu wa Afrika Kusini jana ulipiga marufuku vyombo vya
habari kupiga picha na kutangaza habari za ghasia za Wazalendo ambazo
zimeikumba Afrika Kusini kwa muda wa mwaka mmoja na miezi minane na
kutangazwa katika magazeti ya dunia nzima pamoja na kwenye
televisheni.

Waziri wa sheria wa makaburu Louis Le Grange alisema kuwa wapiga picha
hawaruhusiwi kupiga picha za mapambano na migomo katika maeneo ambayo
yamewekwa chini ya amri ya hali ya hatari isipokuwa tu kwa kibali
maalum kutoka kwa polisi na kwamba waandishi wa habari hawaruhusiwi
kuandika habari katika maeneo hayo. Hayo yalitangazwa katika gazeti la
serikali lililotolewa jana.

Rais Peter Botha, ambaye serikali yake inavilaumu vyombo vya habari
kwa kuandika habari zinazohusu ghasia nchini Afrika Kusini ambazo
zimeifanya Afrika Kusini ishutumiwe na dunia nzima, Alhamisi iliyopita
alivionya vyombo vya habari vya nchi za nje visiandike mabaya tu
kuhusu Afrika Kusini.

Hatua hiyo ya Afrika Kusini ambayo itainyima dunia kufahamu unyama
unaofanywa na polisi kwa wazalendo imechukuliwa wakati askari wa
makaburu wamesambaa kwenye mitaa ya Johannesburg baada ya kuwepo na
ghasia katika siku za hivi karibuni.

Waandishi wa habari kutoka nje ambao wamekuwa wakiandika habari kuhusu
ghasia ambapo zaidi ya watu 800 wamekufa, wameshutumiwa na serikali ya
Afrika Kusini kwa kile inachokiita upendeleo wakati wanapoandika
habari zao.

Zaidi ya waandishi wa habari 170 kutoka nje wako Afrika Kusini wakati
ambapo wengine zaidi wanazidi kuja kwa madhumuni ya kuandika habari za
wimbi la mapambano nchini Afrika Kusini.


Mafisadi wa Marekani wafukuzwa Guinea


Uhuru, Alhamisi, Novemba 10, 1966


RAIS Ahmed Sekou Toure wa Guinea ametoa amri ya kuwafukuza Wamarekani
wote waliokwenda nchini huko kwa kazi za kujitolea (Peace Corps) na
kuamuru waondoke nchini Guinea katika muda wa siku nane.

Amri hiyo aliitoa juzi alasiri kwenye mkutano wa hadhara baada ya
kugunduliwa kuwa Wamarekani hao walihusika na vitendo vya kifisadi
vilivyosababisha kukamatwa na kuzuiliwa kwa wajumbe 19 wa Guinea
nchini Ghana, wakiwa safarini kuelekea Addis Ababa kwenye mkutano wa
mawaziri wa nchi za kigeni.

Kufuatana na habari zilizotangazwa mjini Washington, Amerika
inasemekana kuwa Rais Toure alisema alipokuwa akitoa amri hiyo kwamba
Wamarekani 64 wa kujitolea waliopo mjini Conakry (mji mkuu wa Guinea)
pamoja na wengine wengi ambao wametawanyika katika vijiji na miji
mbalimbali ya Guinea, pamoja na jamii nane za Kimarekani ni lazima
waondoke nchini humo katika muda wa siku nane.

Katika siku chache zilizopita, baada ya tu ya kukamatwa na kuzuiliwa
kwa wajumbe wa Guinea nchini Ghana, serikali ya Guinea iliweka amri ya
kuwazuia Wamarekani hao wa kujitolea wasitembee ovyo kama wanavyotaka
nchini humo, lakini baadaye amri hiyo iliondolewa, imeelezwa kutoka
Washington.

Msemaji mmoja wa Marekani wa kujitolea alisema baada ya kutolewa kwa
amri hiyo kwamba inaelekea kuwa serikali ya Guinea itaizingatia amri
hiyo ya Rais Toure, jambo ambalo Marekani hao hawatakuwa na la kusema.

Akaongeza "ikiwa kama ni hivyo basi sisi hatutakuwa na kipingamizi
chochote na tutaweza kuondoka katika muda wa wiki moja".

Msemaji mmoja wa serikali ya Amerika mjini Washington alidai kwamba
kufukuzwa kwa Wamarekani hao wa kujitolea kumefanyika kutokana na
kukamatwa kwa wajumbe wa Guinea nchini Ghana baada ya kuteremshwa kwa
nguvu kutoka katika ndege ya Kimarekani ambapo serikali ya Kimarekani
haikuchukua hatua yoyote kuwatetea wajumbe hao.



China na Urusi zalaumiana

Uhuru, Alhamisi, Agosti 14, 1969


HONG KONG, Jumatano

CHINA imedai kwamba majeshi ya Urusi yakiwa na vifaru, magari yenye
silaha na helikopta yalishambulia sehemu ya China, yakaua na kujeruhu
wanajeshi kadhaa wa Kichina.

Serikali ya China, katika taarifa kali ya malalamiko iliyotangazwa na
Redio Peking imesema kwamba mapigano hayo ya mpakani yalitokea katika
jimbo la Sikiang ambako China imefanya majaribio ya mabomu ya atomik.

Taarifa hiyo imetaka kuondoka haraka kwa majeshi yote ya Kirusi na
ikasema kuwa ndiyo yenye dhamana ya matokeo ya kile ilichokieleza kuwa
ni "uchokozi wa dhahiri".

Taarifa hiyo iliyotolewa na Balozi wa Urusi mjini Peking pia ilisema
kwamba majeshi ya China yalipigana ili kujihami.

Pia iliilaumu Urusi kwa kupeleka vifaru vingi na majeshi "katika
juhudi ya kutaka kusababisha vita zaidi".

Wakati huo huo, huko Moscow serikali ya Urusi ilitangaza leo kwamba
mejshi mengi ya Kichina yenye silaha yalivuka mpaka wa Mashariki
kutoka jimbo la Sikiang wakaingia katika sehemu ya Urusi lakini
wakarudishwa nyuma na majeshi ya Urusi.

Shirika la Habari la Tass limesema kwamba serikali ya Urusi imetoa
malalamiko kwa China kuhusu "uchokozi huu mpya" na imerudia maonyo ya
kwanza kwamba "uingiliaji wowote katika ardhi ya Urusi utajibiwa
vikali".

Tass limesema kwamba mapigano yalikuwa katika sehemu ya Kazakhstan,
sehemu iliyokuwa na mapigano wakati wa mkutano wa vyama vya
Kikomunisti mwezi Juni.

Shirika la Habari la Tass limesema kwamba maafisa wa Kichina wametiwa
nguvuni katika ardhi ya Urusi. Lilisema kwamba kumetokea vifo na
majeruhi katika mapigano hayo lakini halikutoa maelezo kamili.


Congress itawafukuza wageni Lejiko - Mtemvu

Mwafrika Jumanne Septemba 25, 1962


"AMRI kali kali zinakuja katika serikali ya TANU ya Jamhuri, kwa hiyo
ukipigia kura TANU, unajipalia Makaa ya moto yakuunguze kichwani; pia
unakaribisha taabu".

Haya yalisemwa na Bw. Mtemvu, Rais wa Congress katika mkutano wa
hadhara juzi mjini Dar es Salaam huko Magomeni.

Akasema: Wapiga kura wakiichagua Congress (wala si Mtemvu labda
mnayechukiana), bali hutamwona tena Mzungu au Mhindi ndani ya Baraza
la Taifa.

Pia watemi watarudishwa katika utemi wao; sheria za wafanya kazi za
kugoma iwapo hawafanywi haki zitarejeshwa; na hata marejinoli kamishna
na maarea kamishna ambao hivi sasa ni watumishi wa serikali bali ni
macheameni wa TANU wataachishwa kazi hizo.

Ukoloni wa ndani

Kuhusu habari za ukoloni wa kisirisiri uliomo serikali na kuitwa
Afrikanaizesheni, Bw. Mtemvu alisema katika kila ofisi ya Waziri, yupo
Mzungu anayeitwa 'Staff Officer". Je, kazi ya Mzungu huyo ni nini?
Kama si kupeleka habari za siri zenu kwao London? (bomoa!!!!!)

Akasema kwamba TANU haiwezi kuondoa mseto kwa sababu uhuru huu
usingepatikana ila kwa sababu TANU imeahidiana na Uingereza mseto
uwepo.

Vile vile TANU inaona ugumu kuvunja ahadi zake na ndiyo sababu Wazungu
chungu nzima pamoja na Wahindi wamejiandikisha kuwa raia wa
Tanganyika. Je, watawezaje kuwabagua ndani ya Baraza la Taifa?
aliuliza Bwana Mtemvu.

Kamishna aeleza mafanikio ya mkoa

Mwafrika Alhamisi Machi 12, 1964

REGIONAL Commissioner wa Mkoa wa Pwani Bwana Suleiman Kitundu
alipokuwa akihutubia mkutano wa Halmashauri ya maendeleo ya mkoa wa
Pwani uliofanyika mjini Dar es Salaam majuzi, Kamishna huyo aliieleza
komiti hiyo mipango mbalimbali ambayo ilipangwa mwaka jana na
imefanikiwa.

Akianza kueleza kwa sehemu mbalimbali alisema kwamba sehemu ya
Kisarawe barabara tatu, shule tano za Lower, Primary, nyumba nne,
dispensary moja, barabara nane zenye urefu wa maili sabini na tatu na
soko moja.

Makadirio ya majengo haya yanakadiriwa kuwa shilingi 47,410 msaAda wa
kupata vitu vilivyojengea ni shilingi 9,400.50 na akiba imekuwa
shilingi 38,009.

Katika sehemu ya Mzizima shule mbili za Upper Primary, kisima kimoja,
madaraja matatu, nyumba mbili za kukaa watu, stoo moja ya ofisi na
mabarabara manne yenye urefu wa maili kumi na nne. Fedha za akiba
zilifikia shilingi 43,577.88.

Sehemu ya Mafia ni dispensari moja tu ndio ambayo imemalizika na
gharama yake ni shilingi 5,110.32 msaada ulitolewa ni shilingi
1,720.92 na akiba imefikia shilingi 3,390.

Bwana Kitundu aliuambia mkutano kwamba sehemu ya Bagamoyo na Rufiji ni
lazima ziongeze juhudi zao na kama hazikufanya hivyo ni wazi
ziTarudisha maendeleo yao ya uchumi wa mkoa huu.

Regional Commissioner aliwashukuru vijana wa National Service kwa
kusaidia kujenga daraja la Mbwamaji na pia alitoa shukrani zake kwa
chama cha Dar es Salaam Football Association kukubali kuchezesha
michezo ya mpira ambayo imewezekana shilingi 700 kupatikana.

Mpaka sasa mfuko huo wa maendeleo umefikia shilingi 6,000 ambazo
zitatumika kwa mipango mbalimbali.

MafunGu mawili ya misaada yametolewa kwa sehemu ya makao mapya ya
Mafia na Mbwamaji. Mafia imepokea shilingi 500 na Mbwamaji shilingi
722 kutoka mfuko huo.

Aliyempiga mfumaniwa kaachiwa
Mwafrika Jumanne Agosti 28, 1962

OMARI bin Musa, kabila Mpogoro aliyekuwa ameshitakiwa kortini huko
Magomeni mjini Dar es Salaam kwa sababu ya kumjeruhi vibaya sana Bwana
mmoja wa Kihaya aitwaye Dotratios Karema, aliAchiliwa huru jana na
Hakimu Bw. Balozi Rehani, kwamba mshitakiwa huyo alikuwa na sababu ya
kutosha ya kumwumiza bwana huyo baada ya kumfumania na mkewe.

Hakimu alitamka kuwa mtu yeyote angekasirika na kuchukua hatua
aliyofanya mshitakiwa ya kupigana, kama angemkuta mtu mwingine akizini
na mkewe.

Alimwonya mshitaki ajihadhari na tabia ya kutembea na wake za wenzake;
alimwonya asiwe na makuu ya kujifanya hajui Kiswahili, kumbe wakati
wote alipokuwa akizungumza na bibi huyo alitumia Kiswahili.

Bakwata yafungua ofisi 'uhamishoni'

Mfanyakazi 08/01/1992

Na Yassin Sadik

VIONGOZI wa Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA
juzi walianza kufanyia kazi zao 'uhamishoni' katika eneo la Upanga
Magharibi nyumbani kwa mkubwa mmoja wa baraza hilo ili kupanga
mashambulizi ya kukomboa ofisi zao zilizowekwa chini ya ulinzi siku ya
Jumamosi na Waislamu wanaopendelea mageuzi ndani ya BAKWATA.

Uchunguzi uliofanywa na waandishi wa habari jana utokana na tukio hili
la aina yake hapa nchini, umeonyesha kuwa zaidi ya Masheikh 20 na
viongozi wa BAKWATA wa mikoa yote ya Tanzania bara ambao walikuwa
mjini Dar es Salaam kusubiri jawabu la kuonana na Rais Ali Hassan
Mwinyi baada ya mkutano wa Morogoro juu ya kusakamwa BAKWATA,
walionekana kufadhaika na wengine wakijadili majaliwa ya uongozi wa
Waislamu.

Huko Kinondoni yaliko makao makuu, waandishi wa habari walikuta kundi
kubwa la Waislamu wanaendelea kuchunga milango yote ya ofisi na
majengo mengine, ikiwemo nyumba ya Sheikh Mkuu huku magari yakiwaletea
vyakula na huduma zinazostahiki.

Ulinzi wa aina hiyo umewekwa pia katika ofisi ya BAKWATA mkoa wa Dar
es Salaam iliyoko kona ya mtaa wa Agrey na Lumumba, na pia Alharamain
ambako huko palikuwa panalindwa kwa doria kali.

Baadhi ya waliokuwa wanadhibiti ulinzi wa shule hiyo ni kati ya walimu
14 waliofukuzwa shuleni hapo mwezi Oktoba mwaka jana kwa kile
kilichoelezwa kuwa hawakuelewana na Mkuu wa Chuo kuhusu maslahi na
mikataba ya kazi.

Mmoja wa maofisa walioonekana kusimamia mipango ya kuchukua uendeshaji
wa ofisi za BAKWATA aliwaeleza waandishi wa habari jana hiyo kuwa
watakuwa tayari kulegeza msimamo wao ikiwa viongozi wawili wa makao
makuu watatangaza kujiuzulu wenyewe. Viongozi hao aliwataja kuwa ni
Alhaj Suleiman Hegga ambaye ni Kaimu Makamu Mwenyekiti na Alhaj Mahami
Rajabu Kundya ambaye ni Kaimu Katibu Mkuu.

Kwa mujibu wa ofisa huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini
viongozi hao inadaiwa wanaendesha chombo cha Waislamu kama kampuni ya
mtu binafsi au kambi ya jeshi.

Alipoulizwa kuhusu hatua waliyochukua baada ya kukamata maofisi ya
BAKWATA, msemaji huyo alieleza kuwa "vinginevyo tumeshaiomba serikali
iwaondoshe watu hao wawili kwa ajili ya usalama na amani ya Taifa
hili, isimamishe katiba ya BAKWATA ya 1984 na hapo hapo Sheikh Mkuu
awajibike kwa kufumbia macho maovu, dhulma, dharau na madhambi
yanayofanywa na watendaji wake dhidi ya Waislamu wa nchi hii kwa zaidi
ya miaka 15 sasa.

Juhudi za kumpata Sheikh Mkuu Hemed bin Jumaa bin Hemed zilishindikana
jana ili kupata maelezo yake juu ya mgogoro huu maana inasemekana kuwa
siku moja kabla ya tukio hilo alihamisha familia yake iliyokuwa
inaishi karibu na Makao Makuu ya BAKWATA na hivyo kila akitafutwa
huambiwa "yuko Tanga".

Mwenyekiti wa jumuiya hizo za Kiislamu ambazo inadaiwa zimeungana
kuchukua nafasi ya BAKWATA Sheikh Salum Khamis alieleza kuwa katiba ya
kuendesha baraza hilo jipya imepitishwa Jumamosi walipokutana Waislamu
wa nchi nzima, na tayari imeshawasilishwa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani
ili kuchukuliwa hatua zinazostahili.

Alipoulizwa juu ya kuvamia ofisi za watu, ofisa mwingine ambaye naye
aliomba asitajwe jina alidai kuwa "hata hao wakubwa wawili (Hegga na
Kundya) wanaong'ang'ania uongozi hawakukabidhiwa baraza hilo bali
walifanya hila na ujanja kwa siri na kutangaza ghafla kuwa wametwaa
madaraka, na makabidhiano (kama yapo) yalifanyika baada ya kuwatimua
wenzao maofisini.

Mpaka sasa ni miezi 18 Waislamu hatujaitwa kuelezwa walikabidhiwa
nini, kitu gani kimepungua au kuongezeka, makosa gani yaliyowapelekea
kuwaondosha wenzao na maendeleo gani yamepatikana, hivyo tumechoka
kutapeliwa na watu ambao hata serikali iliwatimua kwa kujifanya
maarufu kumbe wabadhilifu", alieleza huku akionyesha uchungu.

Mpaka sasa kila upande unadai kuwa umepeleka taarifa zake Ikulu na
kuomba maamuzi ya Rais Mwinyi juu ya purukushani za uongozi imara wa
Waislamu.

Wakati gazeti hili linakwenda mitamboni polisi waliendelea kufanya
doria kwenye maeneo hayo ili kuhakikisha usalama wa wananchi. Hata
hivyo wafanyakazi wa makao makuu na mkoa wa Dar es Salaam walionekana
nje ya ofisi zao wakisubiri hatima ya patashika za ukubwa.

Mkapa awasili Sudan

Uhuru Jumanne Mei 15, 1979


WAZIRI wa Mambo ya Nchi za Nje Ndugu Benjamin Mkapa aliwasili mjini
Khartoum jana akiwa na salamu kutOka kwa Rais Nyerere kwenda kwa Rais
Jaafar Nimeiri wa Sudan, Shirika la Habari la Sudan (SUNA) limeeleza.

Shirika hilo limesema kwamba, salamu hizo zitaimarisha uhusiano wa
nchi hizi mbili, pia zitafafanua hali ya hivi sasa katika Afrika
Mashariki, lakini halikutoa maelezo zaidi.

>
> Harakati za kuhamasisha umma 1954-1961
>
> * Zuhra * Gazeti la Kwanza kueleza Sera za TANU
>
> LAKINI kile ambacho TANU ilimudu kuwapiku Waingereza katika mazingira
> ya kisaikolojia kupitia hotuba za viongozi wake na propaganda
> nyinginezo ilikipoteza kwa kukosa gazeti la kuandika mafanikio hayo.
> Chini ya ukoloni usambazaji wa habari kwa njia ya uchapishaji pamoja
> na njia nyingine za upashanaji habari zilikuwa chini ya ukiritimba wa
> serikali na wamishionari.
>
> Kwa namna hii serikali ya kikoloni iliweza kudhibiti habari, ikitoa
> habari zile ambazo ilifikiria muhimu kwa maslahi yake yenyewe na hivyo
> zinafaa kusomwa na raia. Idara ya Maendeleo ya Jamii ilikuwa
> ikichapisha magazeti ya Kiswahili - Mambo Leo, Tazama, Mwangaza na
> Baragumu.
>
> Wamishonari walikuwa wakichapisha Kiongozi na Lengo, magazeti haya
> yakimilikiwa na Wakatoliki na Walutheri. Madhehebu ya Ahmadiyya
> ilikuwa na gazeti lao - Mapenzi ya Mungu lakini gazeti hili halikuwa
> maarufu na nakala chache sana ndizo zilizokuwa zikiuzwa. Kwa kuwa
> Waislamu wa madhehebu ya Sunni ndiyo wengi Tanganyika, watu
> walijiepusha na gazeti hilo wakiliona kama kama chombo cha kufru.
>
> Wakati magazeti ya serikali yakijishughulisha zaidi na kampeni za
> kufuta ujinga kwa kuchapisha porojo na visa kuwahimiza watu kusoma,
> Wamishionari walijikita zaidi katika kueneza Biblia na propaganda za
> kupinga Ukomunisti. Kwa kushirikiana katika nyanja ya vyombo vya
> habari serikali na Wamishonari waliweza kuyalinda maslahi yao kwa
> pamoja.
>
> Ramadhani Mashado Plantan alivunja ukiritimba huu baina ya serikali na
> Wamishionari. Akifuata nyayo za Erika Fiah, Mwafrika wa kwanza
> kuchapisha gazeti katika Tanganyika, Mashado alianzisha gazeti lake
> Zuhra.
>
> Mashado alizaliwa mwaka 1900 huko Lourenco Marquis (sasa Maputo) na
> alikuja Tanganyika akiwa mtoto mdogo mwaka 1905 wakati nchi ipo katika
> vita vya Maji Maji dhidi ya Wajerumani.
>
> Mwaka 1924 alirudi Msumbiji na alisafiri kwenda Lisbon kwa pasi ya
> Kireno. Wale waliomfahamu wanasema kwa kiwango cha miaka ya 1950,
> Mashado Plantan alikuwa mtu mjuzi wa mambo. Alikuwa miongoni mwa
> wanachama wa mwanzoni wa African Association ilipoanzishwa mwaka 1929
> na miongoni mwa wanchama wa awali kujiunga na TANU pale ilipoasisiwa
> mwaka 1954.
>
> Msimamo wa Zuhra ulikuwa kuwazindua na kuwashirikisha Waafrika
> kupambana na ukoloni pamoja na ubeberu. Katika tahariri zake nyingi,
> Mashado alimwonyesha Mwingereza kama mgeni ambae baada ya kukaribishwa
> sasa anambughudhi mwenyeji wake. Lakini juu ya yote Zuhra lilikuwa
> gazeti la Kiislamu, likipendwa na halaiki ya watu. Lakini gazeti hilo
> halikuwa likithaminiwa na wasomi ambao walilidharau na kuliona kama
> gazeti la Kiswahili tu, lisilokuwa na ujuzi wowote, lililokusudiwa
> hasa msomaji wa chini asiye na elimu na asiyejua kusoma Kiingereza.
> Mashado alikuwa akichapisha tafsiri ya Qur'an154 ndani ya gazeti lake.
> Zuhra kwa ajili hii halikuwavutia sana wasomi kwa kuwa kurasa zake
> zilitangaza Uislamu.
>
> Mashado, kwa kupitia safu za Zuhra, alikuwa ndiye msemaji wa African
> Association na kupitia tahariri zake alitangaza na kudhihirisha
> msimamo wa chama.
>
> Mwaka wa 1955 Mashado alikuwa na umri wa miaka 55. Mtu mzima na
> mwanasiasa mwenye uzoefu kwa kiwango chochote kile. Mafanikio ya
> Nyerere katika Umoja wa Mataifa na ile hamasa ya umma katika kudai
> uhuru kulizua tatizo ambalo halikutarajiwa.
>
> Mafanikio ya TANU yalikuja kwa haraka na hivyo kuwastaajabisha watu
> wengi. Watu wachache walitambua wakati ule kuwa African Association
> ilikuwa imepigana vita vile kwa niaba ya TANU kwa hiyo njia ya TANU
> ilikuwa imekwishasafishwa kiasi cha kufanya kazi iliyobaki iwe ndogo
> sana. Kwa ajili hiyo sasa ilikuwa rahisi kuwashirikisha watu chini ya
> TANU kudai uhuru. Baadhi ya vijana katika TANU wakawa hawana subira na
> wakapumbazwa na mafanikio ya haraka ya harakati. Mashado alikuwa
> anapokea taarifa nyingi za kukaidi serikali wananchi wakidai kuitambua
> TANU kama ni mamlaka pekee yenye uwezo wa kutoa haki sawa kwa raia.
> Mashado aliliona tatizo hili na hatari yake.
>
> Alitumia fursa hiyo kudhibiti hali hiyo ya hatari ambayo kama
> ingeachiwa kuendelea ingesababisha vurugu na watu kuiasi serikali.
> Aliandika tahariri muafaka moja katika nyingi, akiwakumbusha
> Watanganyika hususan wanachama wa TANU kuwa chama hakijachukua
> majukumu na kazi za serikali. Alisisitiza kwa watu wote kuwa
> Waingereza walikuwa bado ndiyo watawala na wanahusika na kutunza amani
> ya nchi. Machafuko miongoni mwa wanachama wa TANU yaliepukwa kabla
> mambo hayajaharibika.
>
> Mashado alijenga taswira ya TANU na haiba ya Nyerere kama kiongozi wa
> harakati za kudai uhuru wa Mtanganyika. Kupitia Zuhra Mashado
> aliwafahamisha wananchi kuhusu masuala mengi ya kisiasa ya siku zile
> na aliwahimiza wasomaji wake kuyajadili masuala hayo katika kurasa za
> gazeti lake.
>
> Mafanikio ya TANU katika kuuhamasisha umma yaliathiri serikali ya
> kikoloni. Mnamo Novemba, 1955 serikali baada ya kuona hali ya hewa na
> uhasama uliokuwa ukioneshwa na wananchi dhidi ya utawala wa kikoloni,
> serikali ilirekebisha sheria iliyokuwa ikitumia kujilinda na kile
> kilichoitwa 'uchochezi', ikawa ni kosa 'kuchapisha na kuuza au katika
> mkutano wowote wa watu kutoa maelezo yoyote ambayo yataelekea kuzusha
> chuki na manung'uniko miongoni mwa wakazi wowote nchini'.
>
> Serikali ilifanya marekebisho hayo huku ikiwa na watu kama Mashado na
> Nyerere katika fikra yake. Kabla ya kuibuka kwa harakati za kudai
> uhuru, washairi nchini Tanganyika walitunga beti za kuwasifu Wafalme
> na Malkia wa Uingereza kutoka ukoo wa Windsor pamoja na nasaba yao.
> Ghafla baada ya kuundwa kwa TANU palitokea mageuzi ya maudhui katika
> tungo za mashairi na tenzi. Washairi waliacha kumsifu na kumtukuza
> Mfalme na Malkia wa Uingereza. Wakiongozwa na Saadani Abdu Kandoro
> walianza kutunga mashairi yenye ujumbe wa kizalendo wakimsifu Nyerere
> na TANU.
>
> Mara tu baada ya marekebisho hayo ya sheria Mohamed Suleiman, mshairi
> hodari akijulikana sana kwa jina lake la ushairi la - 'Mtu Chake',
> alikamatwa, akatiwa ndani na kuhojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi,
> Dar es Salaam kilichokuwa na sifa mbaya ya ukatili. Mtu Chake alikuwa
> ametunga mashairi ya kuvutia sana kuhusu Nyerere, TANU, utaifa,
> mshikamano, udugu, upendo na wakati huo huo kuwakejeli Waingereza.
> Baada ya kuhojiwa Mtu Chake aliachiwa huru bila kufunguliwa mashtaka
> yoyote. Lengo la kumtia mbaroni lilikuwa kumtisha tu na kumtia
> msukosuko.
>
> Mashado Plantan aliifanyia kampeni TANU hadi chama kilipoweza
> kuanzisha gazeti lake lenyewe, Sauti ya TANU mwaka 1956.
>
> Kuanzia hapo Zuhra lilisaidiana na Sauti ya TANU katika juhudi za
> kuwahamasisha wananchi dhidi ya propaganda za kikoloni. Mashado
> alimuunga mkono Nyerere hadi mwaka 1958. Baada ya kura tatu na baada
> ndipo baada ya kuhisi kuwako kwa uroho na tamaa kubwa ya kujinufaisha
> binafsi na baada ya kuona dalili za kupiga vita Uislam kulikoanza
> kujitokeza katika uongozi mpya wa TANU ulioibuka, Mashado alijitoa
> katika chama na kuanzisha chama kipya, All Muslim National Union of
> Tanganyika (AMNUT). Tutakuja kuona hapo baadae jinsi Mashado
> alivyotupana mkono na Nyerere.
>
> Wana-propaganda * Bantu Group, 1955
>
> TANU ilipoanza juhudi zake za kuushirikisha umma katika harakati za
> kudai uhuru, hasa baada ya hotuba ya Nyerere mbele ya Baraza la
> Udhamini la Umoja wa Mataifa, chama hakikuwa na chombo chake chenyewe
> cha propaganda. TANU ilitambua umuhimu wa kuwa na chombo maalum cha
> propaganda ili kukabiliana na hila za kikoloni.
>
> Katika mwaka 1955, kikundi cha TANU Bantu kiliundwa mahsusi
> kukabiliana na tatizo la udini kutokana na hisia za baadhi ya Waislam
> ndani ya TANU. Tangu kuundwa kwa TANU, kulikuwa na hisia ya kupinga
> Ukristo ndani ya chama.
>
> Tatizo hili la udini lilikuwa likichemka pole pole na chini kwa chini
> ndani ya TANU. Ilikuwa kazi ya kikundi cha TANU Bantu kuwafichua na
> kuwapiga vita wanachama wa TANU waliokuwa na hisia kama hizo.
>
> Bantu ilifanikiwa sana katika katika hili hadi kudiriki kupiga
> marufuku mamkuzi ya Waislamu ya Asalaam Alaikum (Amani iwe juu yako)
> baina ya Waislamu kwa msingi kuwa ilikuwa inawabagua Wakristo na hivyo
> inawatenga. Mamkuzi hayo yalipigwa marufuku kwa sababu kwa mujibu wa
> Uislamu ni Mwislamu tu ndiyo mwenye haki ya kusalimu na kusalimiwa kwa
> namna hiyo. Hii ni kwa sababu maamkuzi hayo yanachukuliwa kama dua; na
> kwa mujibu wa mafundisho ya Waislam ni Mwislam tu ndiyo anaweza
> kumtolea salam hiyo Mwislam mwingine. Mamkuzi yale ya Kiislamu
> yalionekana kama yanakwenda kinyume na imani ya TANU na ilishauriwa
> kuwa 'salaam aleikum' ipigwe marafuku isitumike. Ikiwa mathalan kwa
> kusahau Muislam mmoja atatoa salaam kwa Muislam mwenzake, kwa kawaida
> angejibiwa 'Alaikum salaam' maana yake 'Amani iwe juu yako pia'.
> Badala ya majibu haya mazuri, majibu yaliyobuniwa na Bantu yalikuwa -
> 'Ahlan tabu' maana yake
>
> On Sep 26, 8:17 pm, Yona F Maro <oldmo...@gmail.com> wrote:
> > Kikao cha Bunge chaahirishwa kwa siku moja
>
> > NIPASHE, Ijumaa Julai 21, 1995
>
> > MKUTANO Mkuu maalum wa Chama Cha Mapinduzi utakaochagua jina la
> > mgombea wa kiti cha Urais wa JamhuriyaMuungano kupitia chama hicho
> > unaanza kesho mjini Dodoma.
>
> > Uchaguzi wa jina la mgombea Urais kwa tiketiyaCCM utafanywa kutoka
> > miongoni mwa wanachama watatu wa Chama hicho waliopendekezwa na Kamati
> > Kuu na baadaye Halmashauri KuuyaCCM kuwania nafasi hiyo.
>
> > Waliopendekezwa na vikao hivyo viwili vya juu vya CCM kuwania nafasi
> > hiyo ni pamoja na Waziri wa Fedha, Bw. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri
> > Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, Bw. Cleopa Msuya na Waziri wa
> > Sayansi, Teknolojia na ElimuyaJuu Bw. Ben
>
 
Duh! Kumbe zamani Wahindi walikuwa wanaitwa kwa jina lao hilo hilo 'Wahindi" na sio 'Watanzania wenye asili ya Kiasia' kama tunavyowaita siku hizi.
 
kama kuna mtu anaweza hata kuyascan magazeti aliyoluwa nayo ya long t itakuwa poa.
 
Tuwekee kabisa na zile katuni za Chakubanga

ch_ulevi01.gif
 
duh ujue wakati naendelea kusoma nikajua hamna comment so nikajua page zinaendelea ONGEZA kaka maana magazeti mengine ni wakati HATA DINGI YAnGU nA MAZA HAWAJAKUTANA, so nilikuwa sifikiriwi kabisa hata kuzaliwa, NIPELEKE SHULE ZAIDI
 
News Week Magazine july 27, 1711!

Msafaara wa watumwa umekamatwa Magindu leo hadhuhuri ukielekea Bagamoyo pwani, na Padre Madrios kchmedes!!....wqtumwa wote wameachiwa huru kujiunga na kanisa la st Peters Basirica!

watumwa weeengi wamekuwa waki kimbilia kanda ya ziwa, na pwani ya Bagamoyo ajili ya usalama wao!
 
Back
Top Bottom