Tujikumbushe: CUF Walipoamua Kumtambua Karume

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
Marekani waipa pongezi kwa mabadiliko ya kisiasa Z'bar



Tuesday, 10 November 2009 07:07



SERIKALI ya Marekani imesema kuwa imefurahishwa na uamuzi wa CUF kuachana na msimamo wake mkali wa muda mrefu na kutangaza rasmi kumtambua rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.

Ingawa uamuzi huo haujapokelewa vizuri na wafuasi wa CUF, ambacho ni chama kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar, taarifa ya ubalozi wa Marekani iliyotolewa jana imefurahishwa na hatua hiyo iliyofikiwa baada ya Karume na Seif Sharrif Hamad kukutana na kujadili mustakabali wa visiwa hivyo.

Katika mkutano wa hadhara uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, Maalim Seif, ambaye ni katibu mkuu wa CUF, aliwaambia wafuasi wa chama hicho kuwa wameamua kumtambua Karume kama rais wa Zanzibar kuwa vitendo vya chama hicho vinaonyesha dhahiri kuutambua utawala wake.

Alitoa kauli hiyo siku chache baada ya kutembelea Ikulu ya Zanzibar na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake. Hata hivyo, Maalim Seif alijikuta akizomewa na wafuasi waliohudhuria mkutano huo walioonekana kuwa na hasira.

Katika taarifa ya ubalozi huo, Marekani imesema kuwa kwa muda mrefu imekuwa ikitoa wito kwa viongozi wa kisiasa wa Zanzibar kutetea na kusimamia siasa za maendeleo, amani na haki ili kusiwe na Mzanzibari yeyote anayetengwa.

Iliongeza kuwa Marekani ilitaka kuona kila raia wa Zanzibar anakuwa na sauti kuhusu uendeshaji wa serikali yake na kusiwe na Mzanzibari yeyote anayekuwa na hofu ya kudhuriwa kutokana na msimamo wake wa kisiasa.

“Ni matarajio yetu kuwa kama sehemu ya kuendeleza nia njema ya mkutano huu, viongozi wa Zanzibar watachukua hatua mahsusi za kujenga mazingira mazuri ya kisiasa visiwani Zanzibar yatakayowezesha kukua kwa utawala bora na maendeleo ya kiuchumi kwa wote,” inasema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa hatua ya kwanza itakuwa ni kwa viongozi kuwaelekeza wanachama wao kujizuia dhidi ya vitendo vyote vya utumiaji nguvu na kuvunjika kwa amani.

Tunaunga mkono maoni ya viongozi hawa wawili (Maalim Seif na Karume) kwamba iwapo Zanzibar inaweza kutatua tatizo la mgawanyiko wa kisiasa lililodumu kwa miongo kadhaa, basi ubunifu, ujasiri na moyo wa kujituma wa watu wa Zanzibar utajidhihirisha wazi kwa manufaa ya Wazanzibari wote, inasema taarifa hiyo.

Iliongeza kuwa Zanzibar imetoa mchango mkubwa katika utamaduni wa dunia hivyo huu ni wakati muafaka kwa Wazanzibari wakaidhihirishia dunia kile wanachoweza kufanya na kukifikia.

Wakati huohuo, mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema mazungumzo yaliyoanzishwa baina ya Rais Karume na Maalim Seif si muendelezo wa mazungumzo ya mwafaka yaliyozimika ghafla.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu akiwa mkoani Tanga jana, Profesa Lipumba alisema mazungumzo hayo mapya ni ya Wazanzibari wenyewe yanayolenga kutafuta maridhiano na maelewano ya kisiasa baina ya pande mbili hizo.

Baada ya kuona kuwa mazungumzo mbalimbali ya mwafaka yaliyofanyika baina ya CCM na CUF na kusimamiwa na wasiokuwa Wazanzibari kutokuwa na mafanikio, Wazanzibari wenyewe wakaamua kuanzisha mazungumzo kwa lengo la kutafuta maelewano na maridhiano ya kisiasa kwa mustakabali wa maendeleo yao, alisema Profesa Lipumba.

Mwafaka wa kwanza ulisimamiwa na Jumuiya ya Madola (1999), wa pili ukasimamiwa na rais mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa (2001-2005) na wa tatu ukasimamiwa na Rais Jakaya Kikwete (2005), lakini yote hayakufanikiwa, sasa wenyewe wameamua kuanzisha mazungumzo yao.

Akijenga hoja kutetea uamuzi wa kumtambua Rais Karume, Maalim Seif alifafanua kuwa Baraza Kuu la Uongozi la CUF lilikaa na kukubaliana kuwa kutomtambua ni nadharia zaidi kuliko uhalisia.

Alisema chama hakimtambui, lakini wawakilishi wanaendelea kuhudhuria vikao vya Baraza la Wawakilishi, kitu kinachomaanisha kuwa wanaitambua serikali yake.

Source: http://www.tzlivenews.com

My Take:

CUF Wakae kimya sasa. wasijifanye wao ni washauri wazuri sana kwa CHADEMA na wanaojua siasa zaidi ya kujawa na unafiki na maslahi binafsi.

Waelewe kuwa siasa za bara na Zanzibar ni tofauti. Kule ni Upemba na Uunguja zaidi. Hata hao wawakilishi wao bungeni, majority wanatoka Pemba. Ukumbukwe kuwa Pemba ni sawa na wilaya moja tu ya DSM.

Isiwe tabu. Tunapigania maslahi ya Nchi yetu na watoto wetu. Na wimbo wa Amani na Utulivu usitumiwe kama kisingizio cha kudhulumu haki za raia.

QED.
 
Inasikitisha kuona kuwa sasa hivi CUF wako more concerned na mikakati ya CHADEMA kuliko CCM. Why?
 
Superman

na vile vile kwa chadema wamejikita kuponda na kuponda tena cuf wakati ccm inachekelea. Vimegeuka vita vya panzi.

Hasara kwa mwananchi.
 
Haya yote yanatokana na na siasa za chuki tukubuke Zanzibar kila uchaguzi hutokea mauaji na husababishwa na Serekali sasa kuepusha hayo na sasa walivyo kubaliana ni lipi bora tuipongeze CUF kwa ujasiri wao wa kuepusha madhila na maonevu.Hakuna aliye watetea wakati wanapopata madhila hayo :Adui yako mfanye Rafiki yako.
 
Superman

na vile vile kwa chadema wamejikita kuponda na kuponda tena cuf wakati ccm inachekelea. Vimegeuka vita vya panzi.

Hasara kwa mwananchi.

Maadui wameongezeka wamekuwa wengi. Sidhani kama Chadema wanawaponda CUF pekee tumeona leo wamemsusa rais kwa hiyo ilikuwa ni zamu ya CCM. Mwisho wa siku mwananchi atanufaika kwa kupata haki yake.
 
Superman,

Nadhani upo sahihi kabisa, my take is only for CUF, kukaa kimya na kuiacha CDM iendelee na mapinduzi ya haki za za watanzania. Ikiwa kama kwao CUF haki zako ilikuwa ni kupata madaraka, basi waelewe kuwa CDM si kupata madaraka bali kumkomboa mtanzania. Nadhani CUF inabidi wawe na busara kidogo ktk suala hili, wao wanajua hali ikichafuka inakuaje zaidi hata yetu huku Bara. Waangalie historia itawahukumu.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom