Tujikumbushe Babu wa Loliondo (ili tujifunze)

Mu-Israeli

JF-Expert Member
Mar 21, 2012
2,454
975
Toka mwanzoni kabisa huyo babu alionekana kabisa kuwa yuko zaidi ki-jasiriamali.
Hapa namaanisha huyo babu alikuwa mfanyabiashara wa kawaida tu aliyebuni biashara ya kuuza 'juice' ya mizizi, na kudai kuwa ni 'dawa' ya magonjwa sugu ('dawa' aliyooteshwa na mungu !).
Kilichonishangaza mimi ni kuwa watu wengi sana (wasomi na wasio wasomi) walimuamini kupita kiasi, bila ya kujiuliza maswali madogo tu.

  • Babu alidai anatibu kwa nguvu za mungu (ila hakutaja mungu gani !!!)
  • Babu alikuwa anafanya maombi kabla ya kuanza kugawa 'dawa' yake (hakuwahi kusema anamuomba mungu gani !!!)
  • Watu waliotumia 'dawa' yake wakaaanza kupata matatizo zaidi na kufa (akaingiza swala la imani baada ya kuona wagonjwa hawaponi !!!)
  • Babu akasema 'dawa' yake inafanya kazi ikitumika ndani ya eneo la Loliondo tu !! (watu bado hawakushtukia dili !!)
  • Babu akasema mtu aliruka foleni na kunywa 'dawa', 'dawa' haitafanya kazi !!! (watu bado wakushtuka kuwa wanaingizwa mjini !!!)
  • Kila kona ya nchi yetu kukazuka watu wanaotibu kwa 'kikombe' !!! (watu bado hawakushtukia utapeli !!!)

Sasa hivi huyo babu na watoa 'kikombe' woote hasikiki tena. Babu kishajichumia shs. billion zake kadhaa, katulia kimya......

Serikali na wale woote waliokuwa wanautetea kuwa anatibu kwa nguvu za mungu, hawaonekani kabisa....Maana nakumbuka vichwa vya habari kwenye magazeti megi vikisema:- "dawa ya babu salama..", "babu's kikombe gets intial nod..", nk.

Nawahurumia sana waliokunywa hiyo 'dawa'. Wajiulize maswali yafuatayo:-

  • Walikunywa nini? ('dawa', juice, sumu, ....)??
  • Side-effect za hicho walichokunywa ni nini? (especially long term side-effects)
  • Kama hiyo 'dawa' ilikuwa kweli ni dawa, mbona imeishia ghafla (au wagonjwa wameisha)?

Watanzania tujifunze na tusikubali kudanganyika next time.
 
Mwache babu apumzike!
Wewe unasema wee, babu anakula umeme wa jua, anachajisha simu, nyumba nzuri ya kisasa, na usafiri umepaki nje!...!
U r wasting time broda!..tafuta mada zenye mashiko!
\ babu loliondo.jpg
 
Hahahaha nilijua tu PJ lazima uje kumtetea Mwasapile
 
Mwache babu apumzike!
Wewe unasema wee, babu anakula umeme wa jua, anachajisha simu, nyumba nzuri ya kisasa, na usafiri umepaki nje!...!
U r wasting time broda!..tafuta mada zenye mashiko!
\View attachment 50366
PJ umenikumbusha kuna siku ttulipanga kwenda kwa Babu ili tuweze kurusha LIVE....hivi ilikuwaje tukaacha kwenda maana mimi nakumbuka nisha muaga na wife kabisa akaniambia vipi unao.....hahahahaha
 
PJ umenikumbusha kuna siku ttulipanga kwenda kwa Babu ili tuweze kurusha LIVE....hivi ilikuwaje tukaacha kwenda maana mimi nakumbuka nisha muaga na wife kabisa akaniambia vipi unao.....hahahahaha
Si unakumbuka wakati tukiwa hatua za mwisho za kuchukua Landcruiser 4WD ndo foleni za kukaa kwa wiki zikawa zimeanza?...tukachanganya na zetu, maana waajiri wetu wengine ni jamii ya Miss Judith!
 
Babu ni mjasilia mali wa ukweli hapa Arusha aliwatoa vijana sana maana ilifika wakati wazungu hawakuwa issue tena maana Land cruiser ilikuwa ina beba watu 12x150,000 kuna bar iko pale karibu na Kimahama Bookshop machalii walikuwa wanakesha wakinywa.....
 
Unaonekana ni mmoja wa walio ingia king kwa babu arifu
Hapana!
Mi nawalaumu watu wanaompinga babu kumbe shida yao ni IMANI HABA!...
Waliopona ni wengi mno kiasi naona ni upuuzi kumdharau babu!
 
Si unakumbuka wakati tukiwa hatua za mwisho za kuchukua Landcruiser 4WD ndo foleni za kukaa kwa wiki zikawa zimeanza?...tukachanganya na zetu, maana waajiri wetu wengine ni jamii ya Miss Judith!

hahahahaha......kuna watu wana kushutumu kuwa wewe una mtetea sana huyu babu je kuna ukweli hapo? au unamtetea kwasababu alitoa ajira kwa vijana kazi ambayo CCM wameishindwa.............
 
Hapana!
Mi nawalaumu watu wanaompinga babu kumbe shida yao ni IMANI HABA!...
Waliopona ni wengi mno kiasi naona ni upuuzi kumdharau babu!
Duu labda ndugu zangu hawana bahati nina dungu zangu 11 walienda na matatizo mbalimbali hakuna hata mmoja aliepona...Je unaamini walio pona ni kwa dawa alizokuwa anatoa au walipona kwa imani tu maana kuna magonjwa mengine unaweza kupona kwa imani mkuu....
 
Mwache babu apumzike!
Wewe unasema wee, babu anakula umeme wa jua, anachajisha simu, nyumba nzuri ya kisasa, na usafiri umepaki nje!...!
U r wasting time broda!..tafuta mada zenye mashiko!
\

Hapo kweli umenena!
Babu kapumzika kwenye nyumba saafi kabisa na usafiri mzuri anao.

Lakini gharama yake ikoje?? Iko kama ifuatavyo:-
  • Maisha ya watu wengi sana yamepotea kwa sababu ya uwongo wake.
  • Maisha ya watu wengi sana yamepotea kwa sababu ya serikali na vyombo vya habari kuunga mkono uongo wake.
  • Maisha ya watu wengi sana yamepotea kwa sababu ya watu waliotoa ushuhuda wa uongo kuwa wamepona, na hivyo kudanganya watu zaidi.

Ni kweli kuwa sote tunatafuta pesa ili tuwe na maisha mazuri, lakini sion kwa gharama ya kutoa uhai wa watu wengine ili tu babu wa loliondo na wengineo wapate nyumba, gari na solar panel.
Hiyo nyumba na gari, n.k. anavyomiliki babu unayemtetea vimejengwa na kununuliwa kwa pesa iliyopatikana baada ya kuua watu wengi sana.
Wewe, babu wa loliondo na watu wote tunajua fika kuwa 'dawa' hiyo haikuwa ya kweli, na imeua watu wengi sana kwa makusudi kabisa ili tu babu (na wengineo) wapate hizo nyumba, magari, solar panels, n.k.

Finally, Thread hii ina mashiko sana maana inatukumbusha kuwa makini na matepeli kama hawa, ili tusipoteze maisha ya wapendwa wetu wengi kama ilivyotokea.
 
uMEENDA SAWA KOTE, KASORO HAPO KWENYE NYEKUNDU!
Hakuna chinjachinja aliyetoa roho ya mtu...tafadhali rekebisha kauli yako kama si kuifuta!
Mkuu,
Chukua mlinganyo rahisi tu...ni kwamba waliokwenda kule wote walikuwa wagonjwa, so probability ya kutokea vifo vingi toka kwennye kundi hilo ilikuwa kubwa!
Tusilaumu kwa intuition tu!
 
Mambo makubwa ya maisha hayataki papara....yanataka kujipa muda wa kutafakari na kuangalia mwelekeo na hatimaye matokeo. We still have time to know which is which kuhusu babu.
 
wengi walioenda kwa babu walikuwa wameshakata tamaa hivyo hawakuwa na cha kupoteza wala option nyingine hawakuiona walikuwa tayari kwa lolote.

hata ungwewaambia yule mwizi wasingeelewa.matatizo mchezo
 
mwacheni babu hakuna mtu alimlazzimisha kwenda . na hii tiba ni ya kiimani zaidi . HUTAKI UNAACHA.
 
uMEENDA SAWA KOTE, KASORO HAPO KWENYE NYEKUNDU!
Hakuna chinjachinja aliyetoa roho ya mtu...tafadhali rekebisha kauli yako kama si kuifuta!
Mkuu,
Chukua mlinganyo rahisi tu...ni kwamba waliokwenda kule wote walikuwa wagonjwa, so probability ya kutokea vifo vingi toka kwennye kundi hilo ilikuwa kubwa!
Tusilaumu kwa intuition tu!

Napenda kurudia tena na tena, babu wa loliondo alitoa uhai wa watu kwa makusudi ili apate pesa za hiyo nyumba uliyoionyesha, na gari, solar panels, nk.

Alitoa uhai wa watu wengi sana kama ifuatavyo:-
  • Alisema ameoteshwa 'dawa' inayotibu magonjwa sugu, na kwamba ukitumia tu, baada ya wiki moja utakuwa umepona kabisa. Alisema haya huku akijua fuka kuwa ni uwongo, na akijua fika kuwa watu wataamini na hatimaye watakufa tu.
  • Alitengeneza 'dawa' kwa kutumia mizizi ya mti ambao ni sumu kali, huku akijua fika kuwa hiyo ni sumu na wala sio dawa.
  • Alipoona kuwa watu hawaponi na malalamiko yameanza, alileta kizezo cha 'imani'. Kwamba usipokuwa na imani huponi, huku akijua fika kuwa anachofanya ni utapeli tu. (swala la imani hakulisema mwanzoni alipoanza kutoa 'dawa' yake).
  • Baada ya kuona malalamiko yanazidi, na vifo vimeongezeka sana, akazusha swala la 'watu wasiache kutumia madawa yao ya hospitali'. (swala hili hakulisema mwanzoni alipoanza kutoa hiyo 'dawa' yake).
  • Alijua kuwa hiyo 'dawa' yake ni ya uongo na pia ni sumu, hivyo akatumia jina la mungu ili kuvuta imani ya watu kwenye 'dawa' yake kwa makusudi kabisa.
  • Wewe na watu wote mnajua fika kuwa mgonjwa wa pumu, ukimwi, kusukari, n.k hapewi sumu, ila anapewa dawa, lakini hoyu babu kwa makusudi kabisa aliamua kuwapa sumu ili tu apate mradi wake wa kujenga nyumba, kununua gari na kununua solar panels.
Huyo babu wa loliondo alikuwa mchungaji wa kanisa la kilutheri, na anajua kabisa kuwa uponyaji wowote unaohusisha nguvu za Mungu hautakiwi kulipiwa ada yoyote ile, yaani unatolewa BURE. Lakini yeye kwa makusudi kabisa alitoza watu ada za matibabu - maana alijua hiyo tiba yake haitokani na Mungu, ila ni uongo mkubwa ambao utasababisha watu wenga sana kupoteza maisha.
Narudia tena, watanzania tujifunze, tusiangukie tena kwenye janga kama hili.
 
Back
Top Bottom