Tujikumbushe ahadi za Mwana-TANU na tulipo sasa hivi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Tanu.jpg
 
Kijana umenikumbusha enzi zile nilipokuwa tanga, Nakumbuka wakati najiunga rasmi na TANU nilikula kiapo cha kutoenenda kinyume na chama zikiwemo hizo ahadi! Hivyo nilikuwa mwaminifu sana na Mpaka sasa, sijajua sasa hivi kama vyama hivi vingine vinaapisha wanachama wake ili kupata wanachama wenye nia ya dhati kabisaa na wasioyumbishwa na tamaa ya madaraka. Ahsante sana
 
Wadau
Tujikumbushe kidogo ahadi kuu za Mwana CCM
1. Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.
2. Nitasema kweli daima fitna kwangu mwiko
3. Rushwa ni adui wa haki sitapokea wala kutoa rushwa.
4.Daima nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote.
5.Cheo ni dhamana sitakitumia cheo change au cha mtu mwingine kwa faida yangu.
6. Nitashirikiana na wenzangu wote kuijenga nchi yangu.
7. Nitakuwa mtiifu na mwaminifu kwa Rais wa Tanzania.
8. Nitakuwa mwanachama mwaminifu kwa chama changu, raia mwema wa Tanzania na Afrika.
Karibuni
 
CCM ishakufa kitambo, tafteni jukwaa la kujadili mambo yenu. CCM ndio mdudu gani hbanaa?
 
Wadau
Tujikumbushe kidogo ahadi kuu za Mwana CCM
1. Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.
2. Nitasema kweli daima fitna kwangu mwiko
3. Rushwa ni adui wa haki sitapokea wala kutoa rushwa.
4.Daima nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote.
5.Cheo ni dhamana sitakitumia cheo change au cha mtu mwingine kwa faida yangu.
6. Nitashirikiana na wenzangu wote kuijenga nchi yangu.
7. Nitakuwa mtiifu na mwaminifu kwa Rais wa Tanzania.
8. Nitakuwa mwanachama mwaminifu kwa chama changu, raia mwema wa Tanzania na Afrika.
Karibuni

Ahadi hizo ni kama hadithi za kutunga tu,hazijawahi kutekelezwa popote.Kama kiongozi aliyeapa kuilinda na kuitetea katiba,anaivunja hadharani kwa kupiga marufuku utekelezwaji wa haki za kikatiba kama vile Uhuru wa mawazo na mikusanyiko,ahadi hizo ni takataka tu.

Unasema binadamu wote ni sawa wakati binadamu haohao chini ya serikali ya chama chenye ahadi ya usawa wanauwawa na kupigwa risasi mchana wa jua kali?Usawa upo wapi kama Taifa limeasisi kundi la wauwaji kwa lengo la kuuwa,kuteka na kutesa yeyote atakayeikosoa serikali?

Kiongozi anahimiza matumizi ya takwimu sahihi wakati yeye kila siku anatoa data na taarifa feki!Hivi ni kweli alikamata vichwa vya treni na magari yasiyo na mwenyewe pale bandarini?Ni kweli 2015 alipoingia madarakani sukari ilikuwa inauzwa sh.5000/Kg?Ni kweli amekamata UsDollar bilioni 1 hapo JKNIA?Ni kweli kuwa kuna mtu alikuwa anahamisha sh.8,000,000/ kila dakika na walimkamata na kumweka mikono salama?

Eti nchi yenye usawa na haki inaendesha maigizo ya uchaguzi huku mkuu wa nchi akiwaonya makada aliowapa mamlaka ya kusimamia uchaguzi kutomtangaza mshindi halali aliyetokana na matakwa ya wapigakura.Eti mteule wa rais anaandika barua ya kuomba radhi baada ya eneo lake la uchaguzi kushindwa kupora ushindi halali wa mgombea!

Eti rushwa ni adui wa haki huku mnaendesha serikali inayohonga hadi kiongozi waache vyama vyao na kujitangaza eti wanaunga mkono Juhudi za kudumisha na kuendeleza rushwa!

Upumbavu ni kipaji na tunu ambayo si kila mtu anayo,hongera sana,ccm hoyeee!
 
Back
Top Bottom