Tujikumbushe ahadi za CCM kupitia Kwa Kikwete

Arushaone

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2012
Messages
14,816
Points
2,000

Arushaone

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2012
14,816 2,000
Ahadi za JK kwenye kampeni za kusakaurais 2010
============================

1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora

2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini

3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria- Igunga

4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga

5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma

6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini

7. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma

8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera

9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi- Kagera

10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba- Bukoba Mjini

11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini

12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera

13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera

14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu- Kagera

15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya

16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba- Kagera

17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali

18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika- Mwanza

19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza

20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita

21. Kulinda muungano kwa nguvu zote- Pemba

22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro

23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa- Mbeya mjini

24. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa

25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea

26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya

27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga

28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa

29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro

30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini

31. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora

32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu

33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini

34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)- Hydom Manyara

35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa-Musoma

36. Kulinda haki za walemavu- Makete

37. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini

38. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha

39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini

40. Kujenga barabara ya lami Manyoni- Kigoma– Kaliua,Tabora

41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi- Arusha Mjini

42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma

43. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido

44.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga

45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini

46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo- Busekera, Wilaya ya Musoma, .

47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido

48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro

49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara

50. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini

51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa

52. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa

53. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania- Iringa

54. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda

55. kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara

56. kuwapa wanawake nafasi zaidi- Kilolo ,Iringa

57. ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar

58. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa- Kabandamaiti mjini Zanzibar

59. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti

60. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma

61. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma

62. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma

61. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma

62. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam

63. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara

64. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha

65. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa- Kibaha

66. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha

👉CCM KUAHIDI NI JADI YAO
👉KUTEKELEZA NI NDOTO. 👉HAKUNA JIPYA ktk ILANI hii ya 2015.
👉MAGUFULI hana JIPYA
👉AHADI zile zile WATU walewale

Hata John Magufuli akitoa ahadi kwa kuwa yuko cha kile kile hataweza kuzitekeleza kamwe.

Wenye nia njema na nchi hii achaneni na CCM kwa kuwapigia kura wagombea kutoka vyama vinavyounda UKAWA Tanzania bara na visiwani.

Piga vita ahadi hewa kokote ulipo. Mfumo hautampa nafasi Magufuli atekeleze ahadi zake shtukeni watanzania wenzangu.

Cha kuelewa ni kuwa JP Magufuli lazima atekeleze matakwa ya JK atakayomwambia afanye.

Chaguo lako liwe UKAWA.

Edward Lowassa Tosha!!!
 
Arushaone

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2012
Messages
14,816
Points
2,000

Arushaone

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2012
14,816 2,000
Utachaguliwaje huna sera wala dira ya kuwaeleza watanzania?

Hii imetoka kwa mwanagamba mwenzio pale Lumumba.
* CCM RASMI TAASISI YA JK

* MIRAJI KIKWETE APEWA TENDA YA KU-PRINT T-SHIRTS ZA CCM ZA KAMPENI.

* MVUTANO MKALI WAIBUKA BAINA YAO.

* UVCCM WANYIMWA PESA WALIYOOMBA KWA AJIRI YA MATANGAZO.

* RUGE MUTAHABA AKABIDHIWA RASMI FUNGU KUFANIKISHA KAMPENI YA CCM.

Hakika kifo kikikaribia hakuna wa kukizuia, hali si shwari sana ndani ya Chama chetu Cha Mapumbavu yaliyokithiri (CCM) baada ya kuibuka hali inayoelezewa kuwa huenda ikasababisha chama hicho kukimbiwa na baadhi ya Viongozi wake kwa kile kilichoelezwa kuwa ni Mwenyekiti wa CCM Taifa kutumia nafasi yake ndani ya chama kwa manufaa yake binafsi na kwa ajili ya Masilahi ya Familia yake.

Katika ofisi za CCM Lumumba Jijini Dar es Salaam yalizuka majibizano hayo ambayo mtoaji taarifa wetu anasema kuwa

"Hapa lumumba kuna mvutano mkubwa juu ya issues mbili

1. JK amempa kijana wake aitwaye Miraji tenda ya kuprint tshirt zote za kampeni, na hii imesababisha mvutano mkubwa wa kimaslahi kati ya Vigogo ndani ya Ccm ambao walitegemea wangepewa tenda hiyo ambayo imegarimu mamilioni ya shilingi.

Walipotaka kujua kwa nini tenda hiyo apewe mtoto wa JK majibu hayakuwa ya kuridhisha sana na kufikia Viongozi wakubwa wa chama hicho kutamka kutishiriki katika kampeni ambazo zimezinduliwa tarehe 23/08/2015".

Ishu nyingine ni hii ya UVCC, iko hivi,
2.UVCCM waliomba milioni 500 kwa ajili ya media coverage kipindi chote cha kampeni,badala yake Akina Nape na Mangula wameipa kazi hiyo clouds ambayo ndio wanaofanya matangazo ya yote ya CCM huku mwakilishi na Mkurugenzi wake Bwana Ruge Mutahaba akiwa amepokea fungu hilo kwa ajili ya kuendesha matangazo."

Kitendo hicho kimewauma sana UVCC ambao wamesikika wakilalamika kutumia muda na nguvu zao kuhakikisha ushindi lakini chama kinageuzwa kuwa cha familia na watu binafsi.
UVCCM wamesikika wakisema kuwa kama mambo ndio hayo basi ni bora wakae pembeni na waangalie mwisho wa mchezo huo na ushiriki wao hautakuwa na maana tena.

Mwenyekiti wa CCM Taifa ana haha na amewaita Wakuu wa Mikoa, Walaya na Wakuu wa vyombo vya usalama ili wahakikishe ushindi wa Ccm unapatikana.

by Mpumbavu na Lofa mwenzao wa CCM mtaa wa Lumumba.
 
masopakyindi

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2011
Messages
14,640
Points
2,000

masopakyindi

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2011
14,640 2,000

Hayo wahadithie wanywa viroba na watakuimbia piiiipoooozzzz!
Huku siye twapiga mbele kwa mbele, na safari ya matumaini itaishia Fire.
 
Arushaone

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2012
Messages
14,816
Points
2,000

Arushaone

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2012
14,816 2,000
Hayo wahadithie wanywa viroba na watakuimbia piiiipoooozzzz!
Huku siye twapiga mbele kwa mbele, na safari ya matumaini itaishia Fire.

Una akili kama za Mkapa wewe. CCM imewafanyia nini watanzania? Hao familia wenye CCM wamekupa hisa au tenda?

Tukutane 25 October machinjioni.
 
Forum statistics

Threads 1,344,386
Members 515,452
Posts 32,819,014
Top