Tujikumbushe AFCON 1980 Mambo Yalikuwa Vipi kwa Taifa Stars.

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Messages
1,883
Points
2,000

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2018
1,883 2,000
Historia huwa inajirudia:

Mechi ya kwanza:
Nigeria 2 Taifa Stars 1

Mechi ya pili:
Misri 2 Taifa Stars 1

Mechi ya Tatu:
Ivory Coast 0 Taifa Stars 0

Pia tukumbuke kipindi hiko ndio tuliwahi kuwa na kikosi bora kabisa kikiwa na wachezaji kama akina Juma Pondamali, Athumani Mambosasa, Leopard Mukebezi, pamoja na Mohamed Kajore (marehemu).

Wengine ni Leodgar Tenga, Jela Mkagwa, Juma Mkambi (marehemu), Omari Husein, bila kumsahau Hussein Ngurungu, Mohamed Salumu, vile vile Peter Tino.

Kabla ya kwenda kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1980 (Nigeria) Stars walienda kuweka kambi ya mwezi mmoja nchini Mexico na walicheza mechi kadha wa kadha za kirafiki ili kujiweka fiti tayari kabisa kwa vita.


Siku moja walienda kucheza mechi ya kirafiki katika mji maarufu wa starehe Uliopo nje kidogo ya makao makuu ya nchi ya Mexico (jina sikumbuki)”.


Katika mchezo huo mwamuzi aliwafanyia fitina Stars kwa kuwatoa wachezaji wetu watatu kwa kadi nyekundu na wakati huo tulikuwa nyuma kwa bao 2-1, kwa bahati nzuri Peter Tino alifanya kazi ya ziada akafanikiwa kuisawazishia Taifa Stars lile bao na ubao ukasomeka 2-2. Basi walianza kucheza rafu mbaya sana kwa wapinzani wao, waliwapiga buti hadi mwisho wa mchezo wachezaji wa Mexico walishukuru Mungu, kwa mchezo kuisha salama.


Sheria za soka zinasema mwamuzi haruhusiwi kutoa kadi nyekundu zaidi ya tatu kwa timu moja, baada ya kadi tatu nyekundu kinachofuata ni kuvunja pambano endapo timu hiyo itaendelea kufanya makosa. Stars walilijua hilo ndio maana waliamua kuwachezea rafu wapinzani wao.

Aluta Continua.
 

Forum statistics

Threads 1,363,978
Members 520,595
Posts 33,303,123
Top