Tujikite kumaliza miradi mikubwa iliyopo; madeni yaliyopo yanatosha. Haraka ya nini Bagamoyo?

MSHINO

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,067
709
Ndugu watanzania wenzangu urefu wa pwani kutoka Tanga mpaka Mtwara ni 591.12km, kutoka Tanga mpaka Dar es salaam ni 195.07 na Dar es salaam kwenda Mtwara 397.39 km.​

Kwa kuwa umbali kutoka Tanga na Dar es salaam ni karibu sana yaani km 195.07, huku umbali wa kutoka Tanga mpaka Bagamoyo ni km 154.24 km. Je, kuna haja ya kuwa na bandari ya tatu kati ya Dar es salaam na Tanga? Kwa kuwa Bandari ya Mtwara ina kirefu zadi kwanini mradi wa Bandari ya Bagamoyo usihamishiwe kuboresha bandari za MTWARA na TANGA? Ili mizigo ya kwenda Nchi za Zambia, Malawi na DRC Congo-Kusini ipite Mtwara, huku Bandari ya Tanga ijengewe miundombinu ya kuwa bandari ya kushusha mafuta ukizingatia kuna mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda.

Pia kwa sasa ma- tang ya mafuta kule kigamboni siyo salama tena siku ikitokea dharula ya moto au vita Dar es salaama itakuwa katika kaburi la moto. Bandari ya Dar es salaam imeongezwa kina ili kuingiza meli kubwa zaidi hivyo ni swala la kuiboresha kidogo kwa sababu miundo mbinu ya SGR ipo tayari ipo ni rahisi. Hapa nguvu kubwa utumike kujenga bandari ya nchi kavu kule Ruvu.

Mwisho: Kwa sasa nchi yetu ina miradi mikubwa inayohitaji pesa nyingi na uwekezaji mkubwa kama SGR (Dar-Mwanza-Kgm), Mwl Nyerere Hydro power, Daraja la Busisi, ujenzi wa meli na kufufua shirika la ndege la ATC, sioni haraka ya kuwa na mradi huu kwa sasa.

Kama tukijikita kufungua nchi Jirani kama Rwanda, Burundi, Condo, Zambia na Malawi kwa kuunganisha na miundombinu ya SGR itakuwa na tija kubwa sana kuliko ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Kama ni ule mradi wa viwanda pale Bagamoyo basi wawekezaji wapewe eneo bandari ya Tanga, Mtwara au karibu na bandari kavu Ruvu, kwani mizigo itasafirishwa kwa SGR kuelekea bandarini.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom