Tujifunze toka Botswana na South Africa kuhusu Madini, hizi porojo hazitatusaidia. ..!!

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,697
9,048
Kuna nchi 2 katika Afrika ambazo ni Botswana na South Africa ambazo Uchumi wako uko vizuri na Imara sana kutokana na Biashara ya madini.

Nchi hizi zina mahusianao mazuri tu na Tanzania tangu enzo za Baba wa Taifa lakini jambo la kushangaza hakuna hata kiongozi mmoja wa nchi hii alishawahi kufikiri kwenda kupata utaalamu au ushauri katika uwekezaji wenye tija kwenye madini.

Tangu ugenishaji wa Raslimali za Tanzania uanzishwe na Rais wa Awamu ya 3 Mzee Nkapa hakuna tija yoyote ambayo Watanzania wameipata tokana na madini. Mikataba yote iliyosainiwa tokea awamu ya 3 chini ya Mkapa, ikaja awamu ya 4 chini ya Kikwete imekuwa ni ya kifisadi na yenye kunufaisha matumbo ya Viongozi wa CCM, ndugu, jamaa na marafiki zao.

Leo hii katika Awamu hii ya 5 CCM wanakumbuka shuka asubuhi kumeshakucha...!! Ukisikiliza hizi porojo na propaganda zinazotangazwa mubashara kwa mbwembwe nyingi utafikiri kichaa kaokota dodo chini ya mnazi. CCM wanasahau kwamba watu hawahawa wanaolaumiwa, kutukanwa na kuitwa wasaliti ndiyo waliokuwa wakipiga kelele kuhusu wizi wa madini ulikuwa ukifanywa na wawekezaji uchwara ambao Srarikali hii hii ya CCM iliinhia mikataba nao ili watunyonye Watanzania lakini Viomngozi wanufaike na upuuzi huo.

Wananchi hatuoni hatua stahiki zinachukuliwa kwa hawa Mafisadi waliosaini Mikataba na Sheria za Madini badala yake wanaondolewa nyadhifa tu huku wakiendelea kufaidi fedha waliyovuna toka kwenye mikataba hiyo ya kifisadi. Kama JPM ni Rais mpeda haki basi tunaomba hao walioliingiza Taifa kwenye mikataba hiyo nao wahukumiwe...maana hawa ndio wasaliti namba moja!!!
 
Back
Top Bottom