Tujifunze Nini kwa Hawa Viongozi wanaotembelea Tanzania

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,372
6,078
Leo Waziri mkuu wa Ethiopia ameanza ziara ya kutembelea Tanzania. Nchi hii ina rekodi mbaya sana katika masuala ya Demokrasi, upinzani ni marufuku, viongozi wengi wa upinzani wapo jela, waandamanaji wanapigwa risasi.

Rais wa Uturuki alitembelea Tanzania na huyu kiongozi hataki upinzani nchini mwake wapinzani wengi wamefungwa na kwasasa ana mpango wa kubadilisha katiba ili atawale mpaka mwaka 2030.

Rais wa Rwanda alitembelea Tanzania na huyu kiongozi hakubali demokrasia ndani ya nchi yake wapinzani wengi wameuawa na wengine kufungwa.

Rais Museveni alitembekea Tanzania, ni kiongozi aliyetawala kimabavu kwa muda wa zaidi ya miaka 30 chaguzi zote zinazofanyika nchini humo yeye hutangazwa mshindi, wapinzani huwa wanafungwa mara kwa mara.

Je Tanzania tutajifunza nini kutoka kwa hawa viongozi wanapofanya ziara hapa nchini.
 
Ni waz kuwa Tz inaelekea kwenye utawala wa kiimla, kana kwamba uongozi uliopo madarakani haupo tyr kuachia ngazi! Hiyo n ishara tosha kuwa huenda wakawa wanapewa mbinu mbdala za kuweza kuzorotesha upinzani!
 
Leo Waziri mkuu wa Ethiopia ameanza ziara ya kutembelea Tanzania. Nchi hii ina rekodi mbaya sana katika masuala ya Demokrasi, upinzani ni marufuku, viongozi wengi wa upinzani wapo jela, waandamanaji wanapigwa risasi.
Rais wa Uturuki alitembelea Tanzania na huyu kiongozi hataki upinzani nchini mwake wapinzani wengi wamefungwa na kwasasa ana mpango wa kubadilisha katiba ili atawale mpaka mwaka 2030.
Rais wa Rwanda alitembelea Tanzania na huyu kiongozi hakubali demokrasia ndani ya nchi yake wapinzani wengi wameuawa na wengine kufungwa.
Rais Museveni alitembekea Tanzania, ni kiongozi aliyetawala kimabavu kwa muda wa zaidi ya miaka 30 chaguzi zote zinazofanyika nchini humo yeye hutangazwa mshindi, wapinzani huwa wanafungwa mara kwa mara.
Je Tanzania tutajifunza nini kutoka kwa hawa viongozi wanapofanya ziara hapa nchini.
  • Naona umeamua ku limit thread yako katika negative side, fahamu kuwa mazuri ya kujifunza yapo, tena ni mengi kuliko hayo maovu machache
 
Tunakoelekea ni kule kule!!!

Huyu wa hapa amebadili katiba ya chama ili mwaka 2020 agombee pekee yake!!!

Mwaka 2020 akirudi Magogoni atafanya attempt ya kubadili Katiba ya Jamhuri ili agombee tena 2025 kama alivyofanya Swahiba wake PK na Mu7!!!

Na amini amini nawaambia; huyu mtu asipodhibitiwa; atakaa madarakani hadi 2050...!!!
 
Naona umeamua ku limit thread yako katika negative side, fahamu kuwa mazuri ya kujifunza yapo, tena ni mengi kuliko hayo maovu machache
Hebu kwanza tutajie hapa mazuri kutoka kwa Museven na Kagame!!!
 
  • Naona umeamua ku limit thread yako katika negative side, fahamu kuwa mazuri ya kujifunza yapo, tena ni mengi kuliko hayo maovu machache
Nakubaliana na wewe kweli mengi mazuri wamefanya ambayo tunapaswa kuiiga lakini msingi wa nchi yeyote ni kuwa na demokrsia ya kweli na kuchunga haki za binadamu.
 
Back
Top Bottom