Tujifunze: Niliuza simu na kuanzisha biashara

Mr Mikazo

JF-Expert Member
May 26, 2016
1,586
794
Habari wakuu,

Kutokana na ugumu wa maisha na ajira ndo hatuelewi kama zitakuja lini nilipata wazo la kuuza simu yangu pendwa Tecno W3 kwa laki moja na kuamua kufanya hivi;
672caaba08585eec183c0594f7474fbe.jpg

1d6d44d89cc7a41e16a162c54a8667dd.jpg

Kama muonavyo hapo juu, nilinunua Yebo aina na rangi mbalimbali, mifuko ya sulfate(kipindi cha mavuno hiki), chumvi, viberiti na sukari.

Nazunguka mitaa na meneo ya jirani napanga mizigo yangu kama muonavyo hapo juu nachopata kidogo Mungu anasaidia.

Nimeona nilete kwenu ili tuweze kupeana fursa zingine na mawazo mbadala, pia lazima tujue laki moja pia ni mtaji tosha tu tatizo ni uthubutu.

NB: Simu hii nimeazima na huwa naazima mara moja moja kwa wife kuangalia labda email imepotea njia huko.

Nawasilisha, matusi dharau ni mwiko
 
Hongera sana mkuu!!! Ni ujasiri ulioje!!!
Yaani mie natamani niiuze simu hii ata leo ili niingize pesa kwenye biashara.... Sema simu yenyewe ya kuazimwa Nimependa kweli wazo lako
Mkuu tatizo wengi wetu tunatamaa ya kufanya bizness kubwa kubwa, Ila huyu Mr Mikazo akikomaa usijekushangaa baadae anakuja kumiliki kiwanda kikubwa cha kuyeyusha na kuunda plastic materials.
 
Mtaji wako ni ulichonacho wewe mwenyewe usitegemee chakupewa na ndugu pamoja na masimango, maadam una afya Mungu atakusaidia utatoka tu.
 
Ni nzuri,umethubutu,
Ushauri,ongeza tu vyombo vya ndani eg sufuria,bakuli,ndoo za plastic nk ,kwa mazingira ya vijijini utapata wateja,
Kuna vijiji pia,watu hubadilisha bidhaa kwa bidhaa,jaribu nahiyo pia,eg sufuria ya kilo 2,kwa kilo kumi za nafaka nk,.au viroba kumi kwa debe 1,la kilo 20,
 
Japo mleta mada anaweza kuwa si mhusika mkuu, ila ni mawazo mazuri pia ushauri kwa vijana ambao unakuta simu ya laki 3 wakati soli ya viatu vyake imeisha kwa kutembeza bahasha ya kaki kuomba ajira wakati hiyo pesa ni mtaji tosha..
 
Back
Top Bottom