Chimbekeha
JF-Expert Member
- Dec 1, 2018
- 1,193
- 2,163
KUONYESHA na KUONESHA ni maneno ya kiswahili fasaha, maneno haya yamekuwa yakitumiwa tofauti katika mazungumzo yetu ya kila siku...
Nini mzizi wa maneno haya? Swali hili litaweza kutupatia majibu sahihi kama ifuatavyo hapo chini;
KUONYESHA linatokana na mzizi wa neno ONYA, mzizi huo una maana ya KUTAHADHARISHA au KUKARIPIA jambo,kitu, hali au tabia fulani unaweza ukanyumbua mzizi huo ukapata hali tofauti... Mfano; ONYWA, ONYEKA, ONYESHA, ONYESHANA, ONYEWA nk..
KUONESHA linatokana na mzizi wa neno ONA, mzizi huo una maana ya kupepesa macho juu ya kitu au mtu fulani..
unaweza ukanyumbua mzizi huo wa neno na kupata hali tofauti, mfano; ONWA,ONEKANA ONEKA,ONESHA nk.
MFANO WA SENTENSI kutokana na maneno tajwa hapo juu;
- TUNU atakuonyesha popote pale mtakapokutana.
Sentensi hii inamaana ya kuwa TUNU anatarajia kutoa tahadhari kwa mtu ambaye atakutanana nae ila ukisema
- TUNU atakuonesha popote pale mtakapokutana.
Sentensi hii ina maana ya kwamba; TUNU anatarajia kumfanya mtu atakae kutana nae apepese macho yake juu ya jambo, kitu au mtu fulani.
Karibu kukosoa, kuuliza, kupongeza au kurekebisha pale ambapo unahisi panastahili.