Tujifunze kutoka India: Serikali yazuia Wanafunzi kupewa 'homework' na kubebeshwa mabegi mazito

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
1,608
2,000
Nimekua nikijiuliza maswali mengi yasiyo na majibu kuhusu elimu ya sasa, nashindwa kuelewa elimu imebadilika tofauti na niliyosoma mimi au waalimu wetu ndio walikua hawafundishi.

Siku hizi unakutana na mtoto wa darasa la pili amebeba begi zito hadi mgongo unataka kupinda, hasa hizi zinazoitwa english medium schools. Nakumbuka enzi nasoma darasa la pili tulikua na masomo 2 tu, kusoma na kuandika. Leo mtoto wa darasa la pili ana masomo karibu 9 alafu hakuna ratiba ya kesho atasoma somo lipi hivyo inamlazimu kuchukua kwenye begi lake madaftari yote 9 na vitabu vyake maana haijulikani mwalimu gani ataingia.

Huko India serikali imepiga marufuku homework kwa watoto wadogo ili kuwalinda na athari za kupimda migongo kutokana na walimu kuwarundikia kazi.

Hizi shule za english medium zitaua watoto.
IMG_20190212_114056.jpg
 
Chikwuemeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
12,325
2,000
Nadhani ni wazazi kutokujua ratiba ya vipindi lakini ukifuatilia mtoto hawezi kubeba mzigo kama kruta
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
12,570
2,000
Kazi ya watoto ni kusoma; hakuna kingine. Kuna vishule fulani utakuta viwanafuzi vyao vinaenda shift za mchana na daftari moja kalikunja kama chapati liko mfukoni - sketi, kaptula, au suruali. Wakiondoka nyumbani saa nne wanafika shuleni saa nane au sometimes (mara nyingi) hawafiki kabisa! Nadhani unatamani hizo English Medium zifuate utaratibu wa vishule hivyo.
 
spinderella

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
1,137
2,000
Shule ingejenga sehemu maalumu ya makabata ya wanafunzi (lockers) kila mwanafunzi angekuwa na loka lake anaweka madaftari humo ya darasa Yale homework na vitabu anaweza rudi navyo nyumbani mzigo ungepungua

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli mkuu, solution ni kuwa na lockers nyuma ya kila darasa kwa idadi ya wanafunzi wa hilo darasa. Maktaba palitakiwa pawe na text books ambazo watoto wanatumia wakiwa shule then text books anazo nunua mzazi zinabaki nyumbani kwa ajili ya reference wakati wa kufanya homework....na homework zisizidi mbili kwa siku zenye maswali yasiozidi 10 kila moja tena ni mambo aliyofundishwa. Eti mtoto anapewa maswali ambayo hajafundishwa akafanye research....kwa nani???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
isajorsergio

Platinum Member
Apr 22, 2018
2,928

Haswaa, maana research zenyewe hata wanaowapa maswali hawana uhakika nazo.
 
Lucas philipo

JF-Expert Member
Sep 1, 2017
1,393
2,000
Kweli mkuu, solution ni kuwa na lockers nyuma ya kila darasa kwa idadi ya wanafunzi wa hilo darasa. Maktaba palitakiwa pawe na text books ambazo watoto wanatumia wakiwa shule then text books anazo nunua mzazi zinabaki nyumbani kwa ajili ya reference wakati wa kufanya homework....na homework zisizidi mbili kwa siku zenye maswali yasiozidi 10 kila moja tena ni mambo aliyofundishwa. Eti mtoto anapewa maswali ambayo hajafundishwa akafanye research....kwa nani???

Sent using Jamii Forums mobile app
Safi mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Omusolopogasi

JF-Expert Member
Aug 31, 2017
3,633
2,000
Heading iko sahihi. Hizi shule eti wanataka mtoto aweze kusoma akiwa na miaka 2-3. Wapi na wapi hiyo? Huo ni umri wa mtoto kucheza na wenzie. Halafu siyo wao wa kumfundisha. Wanataka mzazi eti ndiye amfundishe mtoto nyumbani. Kuna siku nimegombana nao...
Mods rekebisheni heading..
 
mrsleo

JF-Expert Member
Jan 13, 2014
2,445
2,000
Shule ingejenga sehemu maalumu ya makabata ya wanafunzi (lockers) kila mwanafunzi angekuwa na loka lake anaweka madaftari humo ya darasa Yale homework na vitabu anaweza rudi navyo nyumbani mzigo ungepungua

Sent using Jamii Forums mobile app
Huu ushauri wa kujenga hizo locker ni kwa shule za serikali au english medium?
 
Mpyena Blazze

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
759
1,000
Mbona shule nyingi wanaacha madaftari shuleni,
Wazazi zungumzeni na uongozi watoto waache madaftari ya darasani shuleni,
Wabebe ya homework tu.
Daftari zikiachwa shule huko nyumbani mtoto atajisomea nini!? mwanafunzi anatakiwa afanye review ya kile alichojifunza shuleni. Wizara ya elimu iingilie kati na ije na mkakati wa kupunguza masoma mashuleni.
 
spinderella

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
1,137
2,000
Heading iko sahihi. Hizi shule eti wanataka mtoto aweze kusoma akiwa na miaka 2-3. Wapi na wapi hiyo? Huo ni umri wa mtoto kucheza na wenzie. Halafu siyo wao wa kumfundisha. Wanataka mzazi eti ndiye amfundishe mtoto nyumbani. Kuna siku nimegombana nao...
Wanatufanya misukule, ada tunalipa na kufundisha tunafundusha wenyewe. Halafu text books wanazo recommend ni poor in content, mtoto anatafuta jibu mpaka basi mpaka wewe mzazi uingilie kati kwa ku google au kujikanyaga kanyaga, maana mtoto asipopata jibu anakosa amani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Manton

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
796
1,000
Elimu ya 'prestige' ndivyo ilivyo watu wanapambana kulinda vitengo vyao, visije kupigwa, kikumbo kama vile vya sayansi kilimo, sayansi kimu(maarifa ya nyumbani), ufundi stadi, muziki na kadhalika: waoneeni huruma wenye vitengo vyao wanazo familia zinazo wahitaji sana kiuchumi, kupitia kipato hicho hicho, cha kubebesha watoto mizigo, au mwataka yule waziri wa maarifa ya jamii afufuke tena. Suala kuvunjika mgongo litatatuliwa na madaktari bingwa, litakapojitokeza.
 
Kaveli

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
3,851
2,000
Shule ya 'medium' ndiyo kitu gani?
Unajiita 'hakimu mfawidhi' halafu unaandika semantically vague sentence?!!

-Kaveli-
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom