Tujifunze Kutoka Cuba........

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,194
1,355
Cuba ilikuwa inapata mafuta kutoka Soviet Union, baada ya Soviet Union Kuanguka Kukawa hakuna njia ya kupata mafuta. Hapo ikabidi Cuba itafute njia mbadala.

Kuhusu shida ya Usafiri mabasi makubwa yaliandaliwa kusafirisha watu.... ambapo watu ilibidi wasubili mpaka masaa manne kungoja usafiri, waliagiza baiskeli 1.2 milioni kutoka China na nusu milioni kutengenezwa ndani ya nchi ili kupigana na ugumu wa usafiri. Pia usafiri wa Punda ulikuwa ni jambo la kawaida.....

Sisemi kwamba tuanze kutembelea punda na baiskeli kama Cuba walivyofanya ila kwanini tusijifunze kuishi na tulichonacho..... Kwanini tusifufue viwanda vyetu wenyewe viwanda vya viatu, nguo n.k. (ikowapi Bora, Mwatex n.k.) kwanini uniform za wanafunzi wanajeshi na wafanyakazi wa serikali visingekuwa vinatengenezewa nchini, kwahiyo kukuza ajira.

Kwanini Tununue maziwa kutoka Kenya na Uganda wakati n'gombe tunao na kusindika maziwa na kuyapack hakuitaji fedha za kigeni....

Lets learn to utilize our own things na hii sio kwa serikali tu hata wananchi inabidi tuwe patriotic, inabidi tuone sifa kuvaa nguo ya kitenge, batiki na kiatu cha katambuga sababu kinatengenezwa Tanzania (Hence tunakuza uchumi wetu) na sio Gucci, Versace, CK, Nike Adidas Just because vinatoka nje.
 
Wazo zuri lakini kwanza jiulize hivyo viwanda nani kaviua! Je tukivifufua tutakuwa tumejifunza nini?
Uzoefu unaonyesha waafrika ni wagumu kujifunza!
 
Wazo zuri lakini kwanza jiulize hivyo viwanda nani kaviua! Je tukivifufua tutakuwa tumejifunza nini?
Uzoefu unaonyesha waafrika ni wagumu kujifunza!

Okay hata wakati bado hatujafufua viwanda.... tupende kununua vitu kutoka saccos... na kwa wajasiliamali wadogo wadogo.... sio mpaka tunue sausage kutoka south africa... Hata Arusha Meat pia wanazo...... Wenzetu wachina ndio walivyofanya walinunua bidhaa za ndani hence rasilimali watu ikasaidia kukuza uchumi...... Kuhusu kuuwawa kwa viwanda its because there is no accountability na kuwajibika this needs to be checked as well
 
Ivi tunaitaji kuimport tooth pick kweli.
Kuna vitu ni kupiga marufuku tuu then tutatia akili
 
In today's world, true freedom will come from people that use their brain to find solutions to the common problems surrounding them. Sisi solution ya kila tatizo letu ni kuomba msaada au kutafuta wawekezaji.
 
In today's world, true freedom will come from people that use their brain to find solutions to the common problems surrounding them. Sisi solution ya kila tatizo letu ni kuomba msaada au kutafuta wawekezaji.
Bora hata hiyo misaada tungekuwa tunaiona... Mimi kwakweli sijui hata hiyo misaada inanisaidie mimi kivipi... zaidi ya kunipa image ya omba omba kwa washikaji zangu wa huko abroad.......
 
Ivi tunaitaji kuimport tooth pick kweli.
Kuna vitu ni kupiga marufuku tuu then tutatia akili
We need to build from the bottom up.... Kwanza kuwawezesha wajasiliamali ili hata quality ya bidhaa zao ziwe na quality nzuri pia baada ya hapo ni kuongeza import taxes ya hizi bidhaa ambazo zipo nchini ili kuweza ku compete na bei
 
Nimeanza kuwa patriotic nimenunua betri za National kutumia kwenye radio yangu wanapochakachua umeme...... Lakini Du.. Kiwango Chake? hivi TBS wanafanya kazi kweli.......
 
Back
Top Bottom