Kaveli
JF-Expert Member
- Dec 4, 2012
- 5,415
- 8,819
Ukiachilia mbali mzee Nyerere baba wa Taifa, nilikuwaga 'likizo ndefu' sana ya kutosikiliza kabsa Hotuba za marais wa Tanzania.
Sababu kuu ya mimi 'kuchukulia poa' hotuba hizo, ni baada ya kugundua kwamba hotuba hizo zilikuwa ni 'mboyoyo' tu za kutuhadaa watanzania na kutuahidi nchi ya asali na maziwa. Nyuso za wazungumzaji zikiwa hazioneshi kabsa 'image' yoyote ya uhalisia wa kile wanachokizungumza na kukiahidi. Niligundua kabsa kuwa tayari Nchi ishawekwa bondi, then kabobo na utemi kwa wingi ili kumaintaini political mileage ya kibabe, huku wananchi wanyonge wakiendelea 'kulamba reli'.
Nakumbuka siku moja miaka hiyo. Ilikuwa mishale ya saa 3 hivi usiku if my memory serves me well. Nipo sebuleni nimechill kidogo baada ya kufika kutoka skonga upcountry. Tumemaliza kupiga 'menyu'. Nimekaa sebuleni ili kusubiri baba mwenye mji alale ndo niwashe luninga nichungulie ulimwenguni. TV inawashwa baba akishalala, hii ilikuwa miongoni mwa 'sharia' za kaya hiyo. Hahahaahaa kuishi kwa 'watu baki' unajifunza mengi sana kwakweli, ebu tuyaache haya maana nikiyakumbuka sana yatanitoa nje ya chaki sasaivi !!!!
Nikawasha 'kioo'. Nakutana na Hotuba ya mkulu wa nchi. Nilikuwa nishasikia kwamba mkulu huyo kajiwekea ratiba ya kuzungumza na wananchi kila mwisho wa mwezi kupitia luninga. Basi nami siku hiyo kwa mara ya kwanza ndo 'nikaifumania' hotuba ya mkulu. Najiandaa kuifinya remote, nikasita. Nikasema aaarg ngonja nimsikilize ata kwa sekunde kadhaa, pengine labda kuna 'chakula cha ubongo' nitapata.
Ghafula dogo akaja pale sebuleni. Ni mtoto-damu wa familia. Kavizia wazazi weshaangusha, nae ndo kaibuka pale sebuleni. Sikujua anachotaka.
Ukimya ukatanda kati yetu kwa dakika mbili hivi, kisha dogo akaanza kunihoji, maongezi yetu yakawa hivi:
Dogo: Kaka kwani unatizama kipindi gani hicho ?
Mimi : Ina maana wewe humfahamu Rais wako wa nchi eeh? Anazungumza na wananchi.
Dogo: Namfahamu ndiyo. Kwani anasemaje ?
Mimi : 'Mwenye nchi' huyu bhana mdogo wangu. Anaahidi 'maisha bora' kwa kila 'mwananchi'.
Dogo: Aaargh, kaka unamuelewa?
Mimi : (kimya)
Dogo: Kaka, au weka mieleka. Leo John Cena anamuaharibia mtu.
Hahaha ndo nikagundua kilichomleta dogo pale sebuleni. Nikakaa kimya kwa dakika moja hivi nikiwa naitafakari hiyo 'busara' ya dogo kwamba kuliko kusikiliza ile hotuba, bora tuwatch mieleka! Fasta nikaanza kuifinya remote kumsaka John Cena. Ila channel husika ikawa full chenga, kipindi hiko bado analogy inatamba. Nikatamka: mdogo wangu ebu nenda nje kazungushe antenna, ielekezee Tandale! Basi tukaendelea kuwatch kioo kimya kimya hapo sebuleni tukimshangilia John Cena a.k.a the battle Babylon !
LAKINI leo hii ni awamu ya tano ya 'utawala' (sio 'uongozi'). Nimekuwa nikifuatilia Hotuba zote, top-to-bottom, za Mheshimiwa sana Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Tanzania.
I am non-partisan, ila jamani let the truth prevail... Huyu jamaa ni kichwa! Magufuli ni miongoni mwa marais bora kabisa Africa. Tangu ile hotuba yake ya kulifungua Bunge, nimekuwa na morali kubwa sana ya kusikiliza hotuba zake. Ni Rais ambaye hachoshi kumsikiliza. Ni Rais ambaye hasomi 'written paper' iliyoandaliwa, bali anatema 'madini' tupu toka kichwani at most of the time!
Jana alizungumza na 'wazee' wa Darisalama. Hakika kusema ukweli, ametoa hotuba iliyotukuka. Hotuba ile ilipoisha tu, nikajikuta natamka ''Tawile baba''. Hotuba zake zinatia matumaini.
Binafsi nikiri kuwa navutiwa sana na hotuba za huyu mzalendo. The guy talks potentials for the community. Wakati akiwa anazungumza, his face tells it all kwamba anamaanisha anachozungumza na kuna uhalisia mkubwa ndani ya maneno yake. Angalau sasa, awamu hii, mambo ni tofauti sana kwenye maudhui ya hotuba za mkulu wa nchi.
Rais Magufuli ana nia njema kabsa kwenye nchi hii iliogota for decades kama behewa la Itigi. Wananchi wote (bila kujali itikadi zetu) tuweni supportive kwake, hususani ktk kutumbua majibu! Ni tumaini la watanzania wengi kuwa 'mkemia' huyu atatuvusha na kutupeleka mbele. Tukimuombea, na asipohujumiwa, I am sure kabsa V.I.P huyu atacheza kama Pele !
Sasa wapigaji na mafisadi wapo matumbo joto, hasa yule fisadi papa!
'Mjanja wa Mzizima kawa mshamba wa Darsalaama'
UKWELI UTATUWEKA HURU.
- Kaveli -