Tujifunze kuridhika kwenye mahusiano tuliyo nayo

Super human

JF-Expert Member
Feb 26, 2015
1,147
748
Naandika mawazo yangu haya kama ni yana kasoro sana naruhusu nyongeza na kurekebishwa, tulio kwenye mahusiano ya ndoa endapo hamna zile shida kubwa sana zinazotuharibu.

Tujitulize tu kwa sababu zifuatazo:

- Kila siku humu duniani wanazaliwa wazuri wengi wake kwa waume na hutawamaliza ewe mwanamke au mwanaume na mkishafanya yenu hutambandika usoni uende nae.

- Kila binadamu unaemuona ana kasoro zake ambazo mwanzoni utakua kipofu nazo. Pema ukipema si pema tena.

- Mali na vitu vingine ni matokeo tu kwenye maisha hakuna aliepangiwa kupata milele au kukosa milele unaemwona vizuri leo hujui kesho atakuaje.

- Usimfanyie mwenzio usichopenda kufanyiwa hebu jiulize ninalolifanya ingekua ni mimi?

Tujifunze kupenda UPENDO wa AGAPE kwenye ndoa kuna vitu hata vidogo vya kurekebishwa na kuvumiliana havitakiwi kuharibu ndoa.
 
Super human asante kwa wazo zuri sana binafsi nimeafikiana nawe....ila mapenzi na ndoa siku hizi ni fasheni tu watu wanaoana ilimradi tu wameoana .... Ni wapenzi ili tu watimiziane haja zao (sex, money ) kwa hali ya sasa usitegemee kuwa watu watabadilika tena kwa tulipofikia Ndio inatisha zaidi Mungu tusaidie
 
Umeandika kama vile umekata tamaa. Mapenzi ya kweli bado yapo, ni bahati mbaya kama haujakutana nayo bado.
 
Super human asante kwa wazo zuri sana binafsi nimeafikiana nawe....ila mapenzi na ndoa siku hizi ni fasheni tu watu wanaoana ilimradi tu wameoana .... Ni wapenzi ili tu watimiziane haja zao (sex, money ) kwa hali ya sasa usitegemee kuwa watu watabadilika tena kwa tulipofikia Ndio inatisha zaidi Mungu tusaidie
Go mi num ni Kuomba Mungu kk. ila impact za talaka zmekua kubwa mitaani
 
ila sasa tunafanyaje Mkuu? ili usiumie maana siku hizi movie ndo mpango mzma
Daa... Sahvi ni ngumu sana kutokuumizwa maana unaeza mpenda mtu kwa moyo wote kumbe yeye hakupendi anampenda bhoke na kuja kulijua hilo huchukua muda sana labda ushaumizwa ..... Kila aombae hupewa na naamini Mungu humjibu mtu kwa wakati wake tukimuomba kwa imani.... Tunaumizwa pale tunapojisahau Muombe sana Mungu akupe wa kufanana nae hutoumizwa
 
Sure Mkuu cku iz hakuna upendo wa kwel bali kuna kupenda Mali, elimu, muonekano n.k wakati moja ya alichotaka vinapoisha inakua ni shda tupu. so kuomba ni muhm sana kk
 
Back
Top Bottom