Tujifunze aina mbalimbali za ' Unafiki ' zinazopatikana kwa wingi sana katika ardhi ya Tanzania hasa ya sasa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,871
" Serikali ya awamu ya Tano kupitia Waziri wake wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi imesema kwamba kuanzia sasa ( namaanisha leo hii na usiku huu ) hadi pale Yesu Kristo au Mtume Mohammed watakapokuja kutukomboa Wanadamu haitabomoa tena Nyumba za Wananchi waliojenga maeneo ya Makazi yasiyo rasmi badala yake itarasimisha Makazi holela ".

Chanzo taarifa: UVCCM Tanzania

Naomba Kukumbushwa hivi kuna matukio gani muhimu ambayo yatahitaji mno ' huruma ' ya Wananchi ( Watanzania ) Masikini hasa kwa mwaka huu wa 2019 na ule ujao wa 2020? Nitashukuru kama nitakumbushwa katika hili kwani Mimi nimeshasahau.

Nawasilisha.
 
kwani yeye ataikalia hio nafasi hadi akina yesu watakaporudi? ache kudanganya watu, sheria zenyewe zinabadilishwa kila siku, ukiona hivyo ujue kuna muswada wanataka kuupeleka kwa subwoofer ili wakafanye yao!
 
Lini utakuja kutujulisha unafiki wa watutsi kujitekenya wenyewe halafu kuja kujichekesha?

Taratibu Mkuu mchezo huu hauhitaji hasira. Ya ' Ututsi ' na ' Unyarwanda ' hapa yameingiaje? Watanzania wa leo wana akili kuliko hata nyie wachache mnaodhani mna akili, mbinu na ujanja. Hivi hilo wazo la Waziri lingekuja kabla ya ' Bomoa Bomoa ' kadhaa zilizopita CCM isingepata ' Credits ' za kutosha na kuzidi ' Kuzikonga ' nyoyo za Watanzania wengi badala ya Kauli hiyo kutolewa hivi sasa wakati tayari kuna Watanzania wengi wana ' Vidonda ' kama siyo ' Majeraha ' mioyoni mwao huku kukiwa hata kuna wengine ambao ama Wamepoteza maisha kwa ' Mshtuko ' na Ndugu zao wamepoteza hayo maisha? Halafu mkiambiwa ukweli na Mtu anayewapenda na kuwatakieni mema mnaanza kuleta masuala ya ' Ututsi ' na ' Unyarwanda ' hapa. Ipo Siku mtanielewa tu ila kama ni ' Unafiki ' basi huu wa sasa ' umetukuka ' kabisa.

Nasubiri kuambiwa GENTAMYCINE ni Mpinzani na hasa hasa mwana CHADEMA kwa huu ' Ukweli Mchungu ' niliowapeni hapa.
 
Hapo ni kutokuelewa tuu kauli ya Mh. Waziri au hujafafanua vizuri aliongea hivyo kwa muktadha upi, kwani sheria zipo wazi na Mh. Rais alishasema toka akiwa waziri wa ujenzi kuwa mtu akijenga eneo lililotengwa atabomolewa ila kama barabara intamfuata atalipwa fidia.
 
Angalia sasa unavyodhihirisha hapa ' Upopoma / Upumbavu ' wako halafu GENTAMYCINE ' akiwadharau ' kwa kuwaambieni hamna ' Akili ' mnakasirika na kukimbilia kusema Mimi ni mwana CHADEMA na Mpinzani. Sasa kama kumbe unajua fika kuwa Mheshimiwa Rais alishakuwa na ' Msimamo ' wake juu ya Makazi na Ujenzi holela wa Wananchi unadhani nini sasa kimepelekea Waziri huyu wa Ardhi leo hii kuja na huo Uamuzi? Na je Waziri huwa anamuwakilisha nani? Je unataka kuniambia kwamba haya ' Maamuzi ' ya Waziri Lukuvi Mheshimiwa Rais hayajui au hakuyabariki? Yaani hadi sasa hivi hujui ni nini ' Kimelengwa ' hapo baada ya Chama kusoma vyema ' Saikolojia ' ya sasa ya Watanzania wengi ambayo imejaa Kukata tamaa, Kuumia na Kuchoshwa na Maamuzi ambayo yanawaumiza wengi halafu na hao hao wengi wao ndiyo Chama kinawategemea hasa kwa ' Chaguzi ' za mwaka huu na zile Kubwa na muhimu za mwakani?

Nimekudharau mno tu!
 
eti (wenye vyao kila pembe, wametukaa kooni. nyama ya mbuzi na ng'ombe, sasa hali masikini. haya cjui maneno ya mshairi gani vile. 😯😯😯
 
" Serikali ya awamu ya Tano kupitia Waziri wake wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi imesema kwamba kuanzia sasa ( namaanisha leo hii na usiku huu ) hadi pale Yesu Kristo au Mtume Mohammed watakapokuja kutukomboa Wanadamu haitabomoa tena Nyumba za Wananchi waliojenga maeneo ya Makazi yasiyo rasmi badala yake itarasimisha Makazi holela ".

Chanzo taarifa: UVCCM Tanzania

Naomba Kukumbushwa hivi kuna matukio gani muhimu ambayo yatahitaji mno ' huruma ' ya Wananchi ( Watanzania ) Masikini hasa kwa mwaka huu wa 2019 na ule ujao wa 2020? Nitashukuru kama nitakumbushwa katika hili kwani Mimi nimeshasahau.

Nawasilisha.
Waziri anakesha anazunguka anakula vifungu migogoro ipo palepale

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom