Tujiandae: Tanzania bila CCM Inawezekana!

Ronal Reagan

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,298
3,056
Ndugu Watanzania wenzangu, salaam.

Hakuna tena shaka wala tashwishwi yoyote kuwa CCM haina jema kwa nchi hii. Wengine tulisema sana kuwa licha ujio wa ghafla wa Lowassa UKAWA 2015 (nikiri kuwa mimi ni mmoja wa waliosikitishwa na mambo yale) lakini nilitafakari na kupima na kuona kuwa bado haikuwa sababu ya kuisaliti nchi yangu, bado haikuondoa uhalali na sababu za kuitoa CCM madarakani. Bahati mbaya wengi walishindwa kurudi kwenye utulivu wa fikra na kuishia kupiga kura za hasira na kukomoa; lakini ilitupasa tuone mbali zaidi ya hisia zetu na tofauti zetu.

Sasa wananchi wenzangu, ikifika 2020, chonde chonde wananchi tuweke mbali tofuati zetu tuitoe CCM. Ziko faida na sababu nyingi mno za kuitoa CCM vs za kuibakisha. Kumbukeni huyu Magufuli ndio the very best CCM had to offered us. Imagine this very John is their best lot! Nitoe mifano/sababu chache tu:-

1) Baada ya kuing'oa CCM tutakuwa tumeweka msingi (precedence) kwa chama tutakachokipa dola kuwa tunataka maendeleo na sio uhuni uhuni kama sasa. Na wakishindwa kutupa mahitaji watakuwa wamevunja mkataba na tutawatoa kwenye mamlaka kama tulivyoitoa CCM.

2) Itakuwa ni rahisi kubadili utawala na sheria za nchi pale tutakapoona (wananchi) inahitajika. Tutakuwa tumevunja kuhodhi (monopoly) ambako CCM imejimilikisha kama ilivyo sasa. Yaliyofanyika kwenye mchakato na Bunge la Katiba 2015 ni aibu ya kihistoria na ufisadi wa kiwango cha lami, lakini ile ndio CCM halisi katika ubora na rangi zake.

3) Tutakuwa tumevunja mwiko (mental barrier) ya kuwa bila CCM kutakuwa na vurugu pamoja na upuuzi mwingine wenye kufanana na huo.

4) Tutajenga wigo mpana wa ushiriki na mkusanyiko wa mawazo na hoja zenye tija badala ya siasa mfu za ki-CCM.

5) Kwa mara ya kwanza umiliki wa nchi na Taifa utakuwa mikononi mwa wananchi badala ya genge la wachache CCM.

6) Kama ilivyokuwa punde baada ya uhuru mwaka 1961, wananchi watajawa na ari na mwamko mpya wa nchi yao. Watajitoa na kushiriki kwa hiari kuijenga na kuipigania nchi yao tofauti na ilivyo sasa.
 
Watz wengi wepesi kutongozeka kw virushwarushwa. Ndio maana hakuna msimamo wa dhati

Ujinga na umaskini ni mtaji kwa CCM. Ndio maana wamekuwa wakiwarubuni wananchi kwa vitu vidogo kama t-shirts, kofia, kanga, chumvi, pilau nk

Lakini pia ni jukumu langu na lako kuwaelemishwa wananchi ambao mfumo umewafanya wabaki wajinga na maskini ili wawe daraja la watawala.
 
Back
Top Bottom