Tujiandae na uchaguzi wa marudio 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujiandae na uchaguzi wa marudio 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by meningitis, Sep 16, 2012.

 1. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  ni dhahiri chadema ya sasa imekua na kujizolea washabiki pande zote za Tanzania na kwa kiasi kikubwa ccm inaendelea kupoteza ushawishi kwa vijana,wakulima na wafanyakazi.
  Kwa maoni yangu mwaka 2015 chadema itapata ushindi baada ya awamu ya pili ya uchaguzi.hii inamaanisha uchaguzi utatoa matokeo ya kufungana kati ya mgombea wa chadema na ccm.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Katika taratibu za uchaguzi zilizopitishwa na Mkapa ni kwamba yeyote atakayepata simple majority anatangazwa mshindi. Sidhani CCM na Chadema zitatoka sare 45%-45%. Hapo ndipo uchaguzi itabidi urudiwe. Nahisi Chadema itapata zaidi ya 65%
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  meningitis, Jasusi,

  ..mimi nahisi CCM watakataa matokeo kuwa wameshindwa na tutaelekea kwenye situation kama ya Zimbabwe au Kenya.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  bahati mbaya ya Zimbabwe na Kenya viongzi wa africa walikuja amka na kualaani hilo zoezi.CCM wanalia chambo katiba iwape njia ya kupinga matokeo na serikalia za uamoja wa kitaifa.Zenji waombe hifadhi CUF na Bara waombe CDM. ADC itumike kupunguza cura za cuf Zenj.

  Waanze mpatia Lipumba Ubunge kama Mbatia
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Tukifika hapo tujue CCM wameshindwa kikweli. Chadema lazima iwe na plan B. Tunajua Zimbabwe Patrotic Front walishindwa na tunajua Kenya Raila alishinda. Hatuwezi kuunda serikali ya mseto na mafisadi. We need a plan B
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  Jasusi,

  ..wataanza na kutangaza kwamba CDM imeshindwa. baada ya hapo CDM wakikataa serikali ya umoja wa kitaifa wataambiwa ni waroho wa madaraka na wapenda vurugu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. t

  tenende JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Serikali ya mseto ni sumu!.
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kwa vyovyote vile, nitapinga kwa nguvu zangu ushirikiano wa madaraka na mafisadi. Afadhali tuitwe waroho wa madaraka kuliko kushirikiana katika upokwaji huu wa haki za Watanzania kujichagulia.
   
 9. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Umetumia vigezo gani mpaka umeyasema haya? CCM haikubaliki.
   
 10. Foum Jnr

  Foum Jnr JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 27, 2012
  Messages: 272
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  mark my word, utaratibu wa sasa wa siasa za afrika ni kwa mshindi kuibiwa ushindi wake, halafu mapigano baina ya wananchi wa chama tafauti, baadae suluhishi linalounda serikali ya umoja wa kitaifa. Tumeona Zimbabwe, Kenya na kila kona ya dunia, Vyama tawala vieweza kuadopt njia za kuzima ukweli wa kauli za wananchi na kubakia madarakani kwa mtindo huu. Tanzania 2015, Chadema itashinda bara, CCm itatangazwa mshindi, fujo itatokea mwisho jumuia za nje na za ndani Afrika including Kenya na Uganda watakaa nao both chini kupush for coalition goverment huku chama tawala kikiendelea kuwa na maamuzi makuu ya nchi. Sio mtabiri wa ghibu bali najaribu ku-analyse uatawala wa nchi jirani Afrika na msukumo wa jumuia za kimataifa ushahidi tumeona including ndanu ya Tanzania huko visiwani.

  Vyama vya upinzani havitaweza kushinda na kupewa ushindi wao bila ya kupush for reforms hususana katika Tume za Uchaguzi, mahakama na Vikosi vya ulinzi vya nchi. upendeleo mkuu uliobakia katika chama tawala ni nguzi hizo tatu, na kamwe hazitawekwa katika mfumo wa uadilifu na haki kwani ni kufuta interest za wahusika. Ningelipenda kuona vyama vya siasa vikiweka nguvu ya kweli kweli kuzirekebisha taasisi hizi tatu, only then uchaguzi utakuwa fair and free.
   
 11. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Zambia waliweza, na hata Malawi wameweza. Naamini Tanzania tutaweza tu.
   
 12. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #12
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hapo umehesabu na kura za kuchakachua?
   
 13. N

  Nonda JF-Expert Member

  #13
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Kwani CCM inatangazwa mshindi kwa vigezo gani?

  Link tumeyauchaguzivyombovyadola
   
 14. Foum Jnr

  Foum Jnr JF-Expert Member

  #14
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 27, 2012
  Messages: 272
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Time will tel borther, time will tell:shetani:
   
 15. Foum Jnr

  Foum Jnr JF-Expert Member

  #15
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 27, 2012
  Messages: 272
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  the best option ya kuushinda utawala wowote ni umoja, bahati mbaya upinzani umekosa hilo kutokana na kutoaminiana, kutokuwa na compromise katika sehemu zenye interest nazo na upo pia uroho na choyo baina yao. Umefika wakati kwa chadema na cuf kukaa chini na kutafuta njia za kuweka umoja kwa kutumia mkataba unaoainisha wazi area walizokubaliana. Chadema inaweza kufaidika na cuf iliopo ndani ya serikali visiwani kujijenga zaidi, na cuf pia kuweza kujipanga kwa yale majimbo yaliyo na majority. Moja ya ushauri mkuu kwa CUF ni kutoweka mgombea bara katika nafasi ya urais na profesa Lipumba kupatiwa jimbo lilosafe ili kuzidisha nguvu ya wasomi na wenye vission ya uchumi mbadala ndani ya bunge. kwa chadema kutoweka mgombea visiwani, ukweli ni kupoteza wakati na funds kuwa na mgomba urais zanzibar, tusijidanganye! good political move kwa chadema kutoshiriki bububu, waste of resources, hekima ni kuona mbele.

  majimbo yalio na wanachama wengi wa chadema kutokana na statistics hususan za uchaguzi uliopita waachiwe wenyewe wajipange na kusaidiwa kwa hali na mali na strategies baina yao cuf na cdm ili kuweka mshindi, na vile vile kwa upande wa cuf, yapo yenye nguvu mawili matatu bara (lol) na mengi visiwani. cha msingi baina yao ni kufanya juhudi za makusudi kuwapoteza wale mguu viongozi maslahi katika safu zao kwani wengi wao ndio wanaosababisha kuvunjika kwa miungano yao kutokana na fitina za hapa na pale. kujipanga kwa dhati, kuastahmiliana na kusaidiana kimikakati kubadili utawala.

  over confidence ya upinzani ndio pengo kubwa la kushindwa katika uchaguzi, kutoaminiana baina yao ni ufa umoja ndio njia sahihi ya kusukuma gurudumu la maendeleo ya kweli ya kisiasa. Hizi ni ndoto, sifikirii kama wanaweza kukaa pamoja kwa dhati na kushirikiana. kila mmoja anamuona mwenzake adui, na ndio mwanya kwa utawala kuendelea kusihika hatamu za nchi.
   
 16. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #16
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  mkuu!
  Anayeingiza matokeo na kusoma matokeo ni binadamu!
   
 17. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #17
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Ningekuwa na mamlaka makuu ningemwacha sheikh yahaya husein na jeshi lake la maruani sijui angeitabiaje ccm 2o15 duh! kweli mungu ameumba watu na viatu mwaka huo lazma wavivue
   
 18. N

  Nonda JF-Expert Member

  #18
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Hakuna katika CHADEMA wala CUF atakayekuazima sikio lake.
  Vita ya panzi...........
  Hivi vyama vya upinzani ni vya ajabu kweli.
  Hakuna tume huru ya uchaguzi, mahakama na vyombo vya ulinzi vinatumika kisiasa....ni kazi ngumu kukibwaga chini chama dola.
   
 19. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #19
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Uchaguzi ujao utafanyika chini ya katiba mpya, nadhani simple majority haitakuwapo tena.
   
Loading...