Nimeona ni vizuri nishiriki nanyi uzoefu wa kupata habari mbaya ambazo naona zimejaa sana humu jamii forums na twita labda na mitandao mingine kuhusu ugonjwa wa korona.
Ndugu zanguni mkifanya mchezo mtatoka na magonjwa ya ajabu na hata kupoteza maisha kwa sababu ya hofu.
Siku moja nilimsikia mtaalamu mmoja wa saikolojia akisema watu tujitahidi kuepuka habari mbaya mbaya kipindi hichi maana zitatatuumiza kihisia, zitaleta unyonge, maumivu ya moyo na hofu ambayo vitu hivi vinasababisha kinga ya mwili kushuka hivyo kuchangia vifo vya ghafla na haraka.
Sasa basi mimi kwa kazi zangu huwa natumia muda mwingi sana kusoma habari mbali mbali. Baada ya muda nikaanza kuona mood yangu inabadilika sana. Muda mwingi nakuwa na hofu, mawazo, na mara nyingi nashika tama. Nipo nyumbani napata mshahara kama kawaida hivyo sina shida ya kipato. Baada ya kuangalia vizuri, nikagundua ni taarifa mbaya ambazo nazisoma kila siku hasa hapa JF.
Nilichoamua sasa, taarifa zote za Twitter nimeacha kusoma wala kufuatilia. Maana kule kuna watu wana habari mbaya kama zote.
Na huku JF nimeacha kupost muda mrefu tu, nimeamua kufungua nyuzi positive tu kuzisoma. Nyuzi zote za habari mbaya sifungui. Vile vile natafuta sites nzuri ambapo nitakuwa nasoma na kuangalia mambo yanayo elimisha na kufurahisha tu.
Jamani taarifa mbaya za covid 19 zimetosha. Tangu January hadi May hii imetosha.
Kuhusu vifo, watu wamekuwa wanakufa kila mwaka jamani mbona twatishana sana. Hivi ikiwa kwa mfano ugonjwa huu uliingia later 2019 hadi May 2020 haiwezekani kweli 90% tukawa na vimelea vya huu ugonjwa? Sasa kwa mazingira hayo hivi si kila atayefariki anaweza kuwa na huu ugonjwa?
Ni kweli ugonjwa upo, lakini sio kwa kiwango ambacho baadhi yetu wanatuambia (sijui ni kwa nini hadi sasa ugonjwa huu haujaleta madhara kama ilivyosemwa). Hebu tuwe wakweli, wanafariki watu lets say 100 hadi 1000 kwa siku hivi kweli idadi hiyo inaweza kufichika? Hawa si ndugu zetu tupo nao mitaani?
Mwisho: Nashauri moderators jaribu kuzuia habari mbaya mbaya ambazo zimekuwa zikiletwa na watu fulani fulani kila siku. Sio kwa sababu hawana haki ya kupost ila ni kwa sababu madhara ya habari hizo ni mabaya kuliko faida. Mimi nikiwa ni mmoja wa waathirika hao.
Habari mbona zipo nyingi sana? Zipo habari za kugunduliwa kwa dawa kadhaa, zipo habari za chanjo zaidi ya kumi zipo katika stage za majaribio. Mbona watu hawaleti habari hizo.
Watanzania wengi ni watu wa ajabu sana.