Tujiandae kurudi kwenye chukuchuku maana bei ya mafuta haishikiki

Wanabodi huku mtaani harufu ya Mafuta ya kupikia tumeshaanza kuisahau taratibu, bei inazidi kupaa Kila kukicha.

Imefikia kipindi Sasa Matuta ya kupikia limeanza kuwa Jambo la anasa .Kuna watu imebidi tuanze kurudi kutumia mawese hata Kama itatuwia ngumu lakini hakuna namna maana Mambo ni magumu.

Hili Jambo serikali inabidi iliangalie kwa jicho la kipekee Kama wafanyabiashara wanahodhi MAFUTA .ikibidi Basi iundwe bodi ya MAFUTA ya kupikia na Bei elekezi zitolewe kama ilivyo kwenye petrol na diesel.

Ikibidi Serikali iagize MAFUTA kutoka nje kufidia magepu maana Hali ni mbaya mtaani.

----
Bei ya mafuta ya kula sasa haikamatiki katika maeneo mbalimbali nchini huku pia bidhaa hiyo muhimu ikianza kuadimika.

Kutokana na bei kupanda baadhi ya wananchi waliozungumza na Mwananchi wamei sasa wanatumia mafuta mbadala, hasa ya wanyama kama vile kondoo, kwa ajili ya kupikia.

Mwananchi imefanya utafiti katika mikoa tofauti nchini na kubaini kupanda kwa bei ya mafuta ya kula ya alizeti na yale yanayoagizwa kutoka nje, yote yakiuzwa kwa bei mbayo haikuzoeleka.

Kupanda kwa bei ya mafuta ya kula, kumesababisha kupanda kwa bei ya vyakula vilivyoandaliwa kama vile chips na vitafunwa mbalimbali.

Serikali imekiri kuwepo kwa uhaba wa mafuta nchini ambayo inaelekea kwisha baada ya kuwasili kwa meli za mafuta.

Akizungumza na Mwananchi, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Profesa Riziki Shemdoe mbali na kusema changamoto hiyo inaelekea kwisha, hakuweka wazi sababu za kuchelewa kuingia kwa meli hizo.

“Ni kweli kuna hiyo changamoto lakini itakwisha muda si mrefu kwa sababu meli za mafuta zimeanza kuwasili nchini, hivyo, muda si mrefu yataanza kusambazwa mitaani,” alisema.

Kuhusu kupungua pia kwa mafuta yanayozalishwa ndani, Shemdoe alisema ni kutokana na wafanyabiashara kutumia mwanya wa kuchelewa kuingia kwa meli za mafuta kupandisha bei.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa chama cha wasindikaji wa mafuta ya kupikia Tanzania (Tasupa), Ringo Iringo alitaja sababu mbili zilizosababisha bei ya mafuta kuwa juu nchini.

Iringo alisema mvua kubwa zilizonyesha katika msimu wa mwaka jana ni moja ya sababu kwa kuwa mavuno yalikuwa kidogo katika msimu huo na kufanya wenye mafuta wayapandishe bei.

Alisema zao la alizeti ambalo ndilo linazalisha mafuta kwa wingi halihitaji mvua kubwa lakini katika msimu wa mwaka jana mvua zilinyesha kwa wingi kiasi cha kuharibu mazao hayo mashambani.

Mwenyekiti huyo alisema katika maeneo mengi ambako wanategemea kilimo cha alizeti, wengi hawakuvuna ama walivuna chini ya wastani, hivyo, kusababisha bidhaa hiyo kuwa adimu na viwanda vingi kusimamisha uzalishaji wa mafuta.

“Lakini sababu nyingine ni sheria iliyopitishwa bungeni ambayo iliongeza ushuru wa mafuta yanayoagizwa kutoka nje na kuwafanya wafanyabiashara wengi kuachana na biashara hiyo na kupelekea mahitaji ya mafuta kutegemea zaidi uzalishaji wa ndani,” alisema Iringo.

Mwenyekiti huyo alisema mahitaji ya mafuta nchini ni tani 570,000 wakati kiasi kinachozalishwa ni tani 230,000 kwa mwaka, wakati uwezo wa viwanda kuzalisha kwa sasa ni tani milioni 2 kwa mwaka kama vitafanya kazi kwa asilimia 90 hadi 95.

Alisema uwezo wa kusindika mafuta umekuwa ni mkubwa kuliko uzalishaji wa zao hilo licha ya hamasa kubwa inayofanyika.

Iringo alitaja sababu nyingine kuwa ni uhaba wa mbegu bora zinazotakiwa, akifafanua kuwa hali hiyo inapunguza uzalishaji.

Ili kuokoa jahazi, Iringo alisema hakuna namna, zadi ya Watanzania kuwa wavumilifu hadi Mei na Juni ambako mavuno yataanza katika baadhi ya maeneo nchini, kwa kuwa si lazima mafuta kuagizwa nje.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa kwa sasa bei ya alizeti sokoni haikamatiki kwa sababu gunia la kilo 100 linauzwa Sh70,000 hadi Sh80,000, kiwango ambacho anadai hakijawahi kufikiwa katika miaka ya nyuma kwani bei huwa kati ya Sh30,000 hadi Sh45,000.

Katika Jiji la Dar es Salaam, mafuta ya alizeti ya ujazo wa lita tano yanauzwa kati ya Sh25,000 hadi Sh29,000 kutoka Sh19,000 miezi minne iliyopita.

Kwa upande wa mafuta yanayotoka nje ya nchi, dumu la lita 20 lililokuwa likiuzwa Sh50,000 hadi Sh55,000 sasa linauzwa kati ya Sh78,000 hadi Sh80,000. Wakati huohuo, lita tano zinauzwa Sh22,000, lita tatu Sh14,500 na lita moja Sh5,500 kutoka Sh3,500.

Katika wilaya ya Sumbwanga mkoani Rukwa, bei ya mafuta ya alizeti imepaa kutoka Sh50,000 iliyozoeleka kwa lita 20 mpaka Sh90,000. Pia mafuta aina nyingine yanayoagizwa kutoka nje ya mkoa huo nayo yanauzwa Sh105,000.

Muuzaji wa mafuta hayo katika soko kuu la Sumbawanga, Saada Mohammed alisema bei imepaa kutokana na watu kutolima alizeti msimu wa kilimo uliopita huku wengi wakijikita kwenye kilimo cha mahindi.

Katika wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, mafuta ya alizeti kutoka Singida yanauzwa Sh105,000 kutoka Sh58,000 za hapo awali huku ndoo ya lita 10 ya mafuta hayo ikiuzwa Sh56,000 kutoka Sh29,000.

Mkazi wa Msaranga, Agatha Joseph alisema kutoka na bei ya mafuta kuwa juu, analazimika kutumia mafuta ya wanyama kupikia.

“Unaenda dukani kununua mafuta ya Sh1,000 unapimiwa kidogo huwezi pikia hata siku mbili yameisha, kutokana na hii hali imebidi turudie maisha yetu ya zamani na uzuri ni kwamba ninafuga na sikosi mafuta ya kondoo, ndio nayatumia kupikia sasa,” alisema Agatha.

Huko Muheza mkoani Tanga, bei za vitafunwa vya chai kwenye vibanda vya mama lishe na mitaani zimepanda kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta, jambo ambalo limeibua malalamiko kwa walaji.

Gazeti hili limebaini kuwa vitafunwa kama chapati iliyokuwa ikiuzwa Sh300 katika mitaa ya mji wa Muheza na jijini Tanga, hivi sasa imepanda kati ya Sh400 na Sh500 huku andazi likiuzwa Sh300 kutoka Sh100.

“Nimepandisha bei ya chapati kwa sababu mafuta ya kupikia yameadimika, hapa Muheza nimeyakosa, nimeyafuata hadi Tanga... sijui kwa nini yamepotea kiasi hiki,” alisema Hadija Jumanne, mkazi wa Genge mjini Muheza.
NA MM NAOMBA MH DK GWAJIMA ATUUNNDIE BODI YA KUCHUNGIZA RAFRIDER ZIMEKWENDA WAPI JAMANI KILA DUKA MPAKA PHARMACY N SALAMA...NA..ZIKO JUU BEI YAKE TUSHAZOEA 1000 NW 1500 MPK 2000
HIZIBODI ZITASHAAA MWAKA HUU

NA WEWE MWINGINE UNAHTAJI WAUNDE BODI IPI??!
 
Kwani cement ilifikia wapi.
 
MI NASHAURI ANZENI KUHIFADHI ZILE RESIT ZA MAFUTA YA GARI MUANGALIE WIKI MMETUMIA SH NGAPI..MTUPE MREJESHO TUJADILI NA YA KULA

TUNAPIGA KELELEEEE MAFUTA YA KULA HUKU GARI LINATUMIA FEDHA ZAIDI....

SASA GARI.. LIMEKUWA BORA TULIPE TU HMNAA JINSI WAPENDWA .............
 
We mpumbavu, wangapi wana magari?
 
Sijajua CCM inahusikaje na kupanda Kwa mafuta... Inawezekana Lissu angekuwa madarakani kila kitu kingekuwa comfortable?? Hii nchi ina watu wenye mawazo ya hovyo mno , ukiwa ni raisi ngumu kuamin mawazo Yao
Utaelewa tu
 
Korosho nayo ina hasira kwa sababu bei iko chini sana!😬😬😬
1610375.jpg
 
Nafanya hii biashara nipo Iringa mjini hapa kwa kweli hali ni tete , leo siku ya J .3 , napoandika nimetoka kuchukua dumu moja la lita 20 kwa shilingi laki moja (100000) just imagine ? , sa hivi nipo geto napiga hesabu ili ilirudishie lita moja niuze kwa kiasi gani , nusu kwa kiasi gani na robo pia ni set vipi ,
Tisa kumi mafuta yenyewe hayapatika , ina maana nitarajie bei kupanda zaidi ya hapa.
 
kazi kweli kweli
 
Kuna wanaosema tujilaumu wenyewe kwa sababu tulizoea kupiga dili. Argument zinazoleta kichefuchefu!
 
Ila mzee baba alisema mwaka huu hakuna Raha..naona ameamua atuonyeshee. Kwa vitendo kabisa
 
Tutaanza kusikia miito ya kupunguza matumizi ya mafuta ya kula kwamba yanasababisha presha..
 
Back
Top Bottom