Tujiandae kumrithisha nini mtoto?

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
May 23, 2008
1,933
2,000
Tulia kidogo halafau tafakari jambo hili.
Wewe ni mzazi (hata kama si mzazi jiweke kwenye nafasi hiyo tupate HEKIMA), punde tu, mmepata mtoto wa kwanza. Ukijua kuwa ndiye atakayerithi yale ambayo unayahangaikia jana na leo na kesho, na ndiye atakayelifanya jina lako liendelee kubaki likiheshimiwa au kudharauliwa.

Anakuja mzazi mwenzako, anakuuliza "Tumrithishe nini mtoto wetu?"

Unatafakari kwa dakika chache na kumjibu, "Nafikiri ni busara sana tukimrithisha mali na pesa za kutosha. Tangu sasa inabidi tufanyekazi ya ziada kuona kuwa tunanunua mashamba, tunaanzisha biashara mbalimbali, na ikibidi kuwa na hata viwanda. Atakapokuwa mkubwa ataviendeleza. Kisha na yeye atawarithisha hadi wajukuu zetu, na pia kwa vitukuu,vilembwe, vining'ina...mhh. Unajua wakati huo sisi tutakuwa wazee hivyo itakuwa ni kupumzika tu. Unafikiriaje?"

Unapomwangalia usoni, uso wake umebadilika, amejawa na huzuni kubwa mara hii. Kisha unamwuuuliza tatizo ni nini?

Anakujibu kwa upole "Mimi nafikiria tofauti." "Unafikiria nini?" Unamwuuliza. Anajibu " Nafikiri tujitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kumrithisha si huyu tu, bali na watakaofuta maadili mema yaani tabia njema. Sisi tuwe mfano wa tabia hiyo. Suala la elimu si la kulipuuza. Lakini sioni kama litakuwa jambo la fahari sisi kuwa na mali lakini watoto hawana maadili, hawana heshima, hawajui kuwaza vilivyo yaani kwa usahihi. Natamani wawe ni wenye uwezo wa kujitegemea kifikra, wasioishi kwa utegemezi wa fikra za wengine. Tukifanya hivyo watoto wetu watakuwa watawala. Ndio, watakuwa viongozi bora katika kizazi chao. Ni wangapi wana elimu lakini ni mateja? Ni wangapi wamerithishwa mali lakini wanatapanya? Wangapi wanaviwanja vya urithi wanaviuza che? Mpenzi! Hebu lifikirie hili la maadili na hilo la mali, tujadili vizuri nakisha tuweke msimamo mpya wa familia yetu, unasemaje?"

Karibu kwenye mjadala
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom