Tujiandae kuidai ripoti ya CAG, inatakiwa iwe Public document

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,397
3,884
Kwa taarifa nilizopata ni kwamba ndani ya siku saba toka CAG amemkabidhi ripoti yake Rais wa JMT, ripoti hiyo inabidi iwasilishwe bungeni.

Sasa kuna mtifuano unaoendelea na kila mtu anasema lake. Labda Rais atamsimamisha CAG na kuunda tume ya kumchunguza. Labda hili au lile. Jambo moja lisilo na mjadala na ambalo NI LAZIMA lifanyike ni kwamba Rais iwe mvua au jua inabidi aiwasilishe Bungeni ile Ripoti. Tuna ndege za kutosha za kuipeleka hata asubuhi siku hiyo hiyo ya saba.

Hilo haliishii hapo, inapowasilishwa Bungeni, officially inatakiwa kuwa a public document accessible kwa wabunge wote na wananchi wa kawaida.

Ushauri wangu ndugu wananchi wenzangu....tusiongee sanaaa maana mambo ni mengi na muda ni mchache. Sisi tuanze countdown tuisubiri hiyo ripoti. Wakiamua kutoijadili tutaichambua wenyewe kama karanga. Tuchore mstari, ndani ya siku saba, tunataka ripoti ya CAG itolewe kwa Umma.
 
Wanatutoa kwenye reli kwa kumtumia Piere. Hii kampeni kwa sasa yaweza kuwa ngumu kwa sababu ya likwid.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ndani ya siku hizi zilizobaki kuna jambo moja au mawili yatatokea. Linaweza kuwa kuhusu Liquid au Mjane au kitu kingine. Nategemea wameshatukomaza kujua modus operandi yao.

Msiba wa Ruge ulitumika pia kufanya mambo mawili matatu wakijua attention ya wengi iko kwingine.
 
Siongelei habari za mahakama. Nao watazingua na kutuchelewesha....
 
Nimepata wazo. Kama ripoti hii haitapokelewa au kusomwa Bungeni kwa muda uliotajwa na Katiba, Wabunge wote ambao hamkubaliani na maamuzi hayo hamna sababu ya kubaki Dodoma. Rudini majimboni kwenu mara moja kujadiliana na kuwauliza watu mnaowawakilisha wanasemaje.

Kinyume cha hapo na nyie mnakuwa ni wadau katika maamuzi haya. Tayari wengi tuna mashaka na baadhi ya viongozi wa upinzani, huu ni mtihani tuone kama mtaufaulu kwa kufanya maamuzi sahihi.
 
Siku saba zinaisha lini?

Sent using Jamii Forums mobile app
... CAG alikabidhi ripoti yake Aprili 02, 2019; so leo Aprili 04 ni siku ya tatu inakatika hivyo. Sheria inasema "ndani ya siku 7" ni lazima ikabidhiwe Bungeni na kuwa open kwa wanyonge which means angeweza kuikabidhi hata siku ile ile aliyokabidhiwa.
 
Nimepata wazo. Kama ripoti hii haitapokelewa au kusomwa Bungeni kwa muda uliotajwa na Katiba, Wabunge wote ambao hamkubaliani na maamuzi hayo hamna sababu ya kubaki Dodoma. Rudini majimboni kwenu mara moja kujadiliana na kuwauliza watu mnaowawakilisha wanasemaje.

Kinyume cha hapo na nyie mnakuwa ni wadau katika maamuzi haya. Tayari wengi tuna mashaka na baadhi ya viongozi wa upinzani, huu ni mtihani tuone kama mtaufaulu kwa kufanya maamuzi sahihi.
... hakuna tafsiri wala maana nyingine bali ni KUVUNJA KATIBA. Hiyo ndio maana yake.
 
Bandiko lako ni la kizalendo sana na tetesi zinasema
Kuna ufisadi wa zaidi ya trion 2+ mwanajamii forum mwezetu #technically alileta uzi hapa watu wakambeza haya sasa kama mtaiona tena.
 
Hili jambo likipita kizembezembe hivi nitasubiri zangu season ya Game of Thrones na kuendelea na mambo yangu mengine. Mimi na habari zozote za siasa za Tanzania itakuwa ndiyo bye bye.
 
Msema kweli mpenzi wa mungu kwa mara ya kwanza naona anataka kuficha ripoti ili madudu yake yasionekane ,atoe ripoti tuone ufisadi wake wa matilioni uliovunja rekodi .
 
Hii report kimsingi ni wananchi wa Tanzania, kama bunge halitaki kuipokea kwa sababu dhaifu kabisa, basi itakua vema CAG Prof. Assad aiweke hadharani tutaijadili wenyewe.

Bunge wenyewe waendelee kujaili madeni ya wabunge.
 
Back
Top Bottom