mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,168
- 1,071
Uchumi wa nchi yetu umeshikwa na wageni kwa asilimia kubwa.Udhaifu wa usimamiaji masuala mtambuka ya uendeshaji uchumi yalipelekea uozo kuzoeleka na kuwa sehemu ya maisha {utamaduni} ya baadhi ya viongozi,watendaji,wafanyabiashara,wanasiasa,wanazuoni n.k.
Mathalani katika masuala ya ulipaji kodi mazingira hayakuwa rafiki kwa serikali kupata stahili zake kwa mapato mengi kuishia kwenye mifuko ya wafanyakazi wa mamlaka za kodi wasio waaminifu na mawakala wa wafanyabiashara.Vitisho vya kuadhibiwa kwa kukwepa au kutolipa kodi vilikuwa mahsusi kwa ajili ya kujinufaisha kupitia rushwa,hongo,mlungula..Wanasiasa nao hawakuwa mbali kujinufaisha {kupokea rushwa ya kusaidiwa vitu,fedha,kwa mgongo wa misaada}toka kwa wafanyabiashara kwa mgongo wa upendeleo maalumu kupitia mamlaka yao kisiasa,n.k
Taifa limepita katika mapito makubwa ya kudumazwa kiuchumi na wachache kujilimbikizia mali na utajiri wa nchi huku wengi wakiogelea kwenye lindi la umaskini na ufukara .Ni wazi kwa miaka mingi iliopita hususani mara baada ya uchumi wetu kuanza kukua kwa kiwango cha kati kupitia uwekezaji uliofanywa ktk miaka 15 to 20 iliopita {Madini,Viwanda vya kati,Biashara ,ujenzi,Bima,Benki,makazi, n.k}.
Kuna haja ya kufungua kurasa mpya kwa kuruhusu misamaha ya kimkakati sababu ya uozo mkubwa sana uliopo katika kila nyanja taifani.Tujenge nchi mpya,uwekezaji mpya,fulsa mpya,serikali mpya...