Tuje kwenye elimu ya dunia, unapelekwa kwa mganga Kariakoo, mganga anaendesha Vitz amevaa raba mtoni

Daisy Llilies

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
1,017
2,154
Jamani pamoja na kuwa maendeleo sasa watu wameadvance lakini hii habari ya kwenda kwa mganga Kariakoo, kwanza unajua kodi ya Kariakoo ilivyo ghali, mganga anaendesha Vitz lazima safari yako ilipie mafuta.

Mganga anakutuma ulete kilo mbili za mchele, nazi mbili na jogoo mweupe usafishwe nyota. Hii ni dinner ya mganga na mkewe.

Mganga anasema akufanyie kisomo unahitaji laki mbili, bado chano cha laki tano.

Waganga wako Ruangwa bwana, panda basi asubuhi Ubungo terminal, saa tano umefika, tena wale wenyewe kabisa unapelekwa na bodaboda huko machimbo. Saa tisa unakula ugali wa mhogo na samaki nchanga kabla ya shughuli.

Basi na wewe ukumbuke mnara wa sabuni, sukari, majani ya chai, kikoi na vitenge vya bibi. Baada ya shughuli unaacha 20,000.
 
Nimeshangaa vitoto vidogo eti navyo viganga skuizi, unakuta kichwani ame bleach halafu chini kanyuka modo na mdomoni kaweka jiti, sikio lina eleni na vipini vya kutosha.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom