Tujaribu,kujiajiri jamani, tusifikirie kuajiriwa tu

Sumasuma

JF-Expert Member
Jun 23, 2011
342
110
Je ni kweli elimu yetu haitufundishi kujiajili?? mbona wenzetu wahindi wanafanikiwa kujiajil??
 
Elimu yetu haina historia ya kufundisha watu kujiajiri! kwanza tunasoma kufaulu mitihani na si kujua vitu ndo maana utaona wanafunzi wakihangaika sana kutafuta past papers na kusolve maswali. Wakati wa mashirika ya umma watu walitafutwa hata bado wako vyuoni. kaka yangu alisoma IDM mzumbe miezi sita kabla ya kumaliza Tanesco na Posta na simu wakati ule walianza kumfuata fuata so akaenda Tanesco. mtu alikuwa na uhakika na ajira hiyo ikawafanya watu wasijishughulishe na ujasiriamali. Upande mwingine wa shillingi wale wasiokuwa na elimu huko vijijini Nyerere alifanikiwa kuwashika vizuri akawaambia nchi hii ni ya wakulima na wafanya kazi, so wakulima wakaendelea kubaki mashambani wakilima kwa kutumia zana duni huku wakipelembwa na misemo lukuki ya kuwatuliza wananchi km PESA NI MATOKEO! wabongo tukaendelea kulala tuu, UBEPARI NI UNYAMA watu wakaona kuisaka noti niwe bepari sitaki, haya yote yametufikisha hapa tulipo sasa
 
it is all about mindset, kiukweli historia yetu ndio inatutesa. kenya walikuwa mabepari siku nyingi sana wanauzoefu. shule zetu zinafundisha watu kuajiriwa. sasa hivi watu wako kwenye siasa. pita mtaa kwa mtaa, ofisi kwa ofisi na bungeni jamani sikiliza baadhi ya wabunge wanaongea nini, ni udaku udaku udaku! ukipiga gap kidogo eti jamaa mwizi fisadi. tutafika???
 
65% ya graduates wa india wanaomaliza ndoto yao ni kufungua makampuni yao na kujiajiri wao wenyewe,
75% ya wamarekani ni hivyo hivyo!
Tanzania 85% graduates wanafikiria kuajiriwa!
 
Tulisoma enterprenuership ili tufaulu paper na maksi za A na B+ tulipata nyingi kweli,ishu kuja kuiapply A na hizo B+ kuwa uhalisia ndo mtihani,tatizo ni
@mindset zetu zinawaza kuajiriwa
@hatuna ubunifu @capital ishu
@tunaogopa risks ujasiriamali kwa wengi umekuwa ni alternative ya kuongeza kipato baada ya kuajiriwa (90%) na kwa wachache sana ndo chanzo cha mapato (10%)
 
Ajabu,wanaofundishwa kozi za entreprenuership
wengi wakihitmu,wanakwenda kuwa wakufunzi,
wanaajiriwa ili kufundisha wengine...........
Yaani hakuna anaejiajiri....
Hao wanaoitwa wajasiriamali wa sido wako zaidi ya 3000
but wanaoishi kwa biashara zao hawafiki kumi....
 
unajua kokote duniani elimu ya shule inakufundisha jinsi ya kufanya kazi na sio kucreate kazi,hivyo kama kayosaki na donald trump wanavyoshauri ni lazima uitafute elimu hii nje ya uwigo wa shule.sisiti kusema naweza nikatoa pia ushauri piga 0717031290
 
unajua kokote duniani elimu ya shule inakufundisha jinsi ya kufanya kazi na sio kucreate kazi,hivyo kama kayosaki na donald trump wanavyoshauri ni lazima uitafute elimu hii nje ya uwigo wa shule.sisiti kusema naweza nikatoa pia ushauri piga 0717031290

Ni Kiyosaki na siyo Kayosaki mzee wa network marketing.
 
65% ya graduates wa india wanaomaliza ndoto yao ni kufungua makampuni yao na kujiajiri wao wenyewe,
75% ya wamarekani ni hivyo hivyo!
Tanzania 85% graduates wanafikiria kuajiriwa!


mkuu mimi nazani tanzania sio asilimia 85% ni 99.09%. Kuna wakati utafika tu watu wataamua kujiajiri wenyewe nyie subirieni tu. Mambo yakibana sana watu watakuwa creative tu wapende wasipende. Sasa hivi bado utakuta graduate wakiwa vyuoni wanawaza kazi tu but, tambua kwamba bado mambo hayajabana sana ila ndo yameanza kubana.
 
ajabu,wanaofundishwa kozi za entreprenuership
wengi wakihitmu,wanakwenda kuwa wakufunzi,
wanaajiriwa ili kufundisha wengine...........
Yaani hakuna anaejiajiri....
Hao wanaoitwa wajasiriamali wa sido wako zaidi ya 3000
but wanaoishi kwa biashara zao hawafiki kumi....

mkuu ni ukweli kabisa, na mtu asikudanganye na semina za ujasiriamali. Wanao toa semina hawana hata kibanda cha kuuzia vocha sasa nashindwa kuelewa wanatoaje elimu wakati wao kudhubutu wameshindwa?

Tatizo ni spirit ya ujasiriamali ndo watu hawana. Hata mtu akiwa na phd ya ujasiriamali kama hana spiriti ni kazi bure, hata vile vitabu ya ujasirimali zile ni story za watu kutafuta pesa kama huna spirit ni kazi bure
 
Mi nafikiri na miundombinu ya nchi sio mizuri sana kwa kujiajiri, kwa mfano ukiangalia mfumo wetu wa kodi haumsaidii sana mzawa zaidi ya mwekezaji kutoka nje, unaweza kuanza biashara leo lakini kabla ya mwezi tra wanakutembelea na kukupiga kodi ya ajabu, mbali na hilo hata rented place kwa business zinapanda kiholela sana, wenye nyumba wanapandisha kodi kodi hizo kulingana na mahitaji yao binafsi, kwa mfano ukiona schoola fees zimepanda jua kuwa huo mzigo utaubeba mpangaji. Hatuwezi kufika katika mfumo huu unless uwe mkwepa kodi au ufanyie biashara katika nyumba yako mwenyewe. Hata ukiangalia ile epz (economic processing zone) bado ina matatizo kibao ambayo wawekekezaji wanailalamikia bado tuna kazi kubwa ya kufanya ili tuwe wajasiriamali wa kweli tusioteteleka.
 
65% ya graduates wa india wanaomaliza ndoto yao ni kufungua makampuni yao na kujiajiri wao wenyewe,
75% ya wamarekani ni hivyo hivyo!
Tanzania 85% graduates wanafikiria kuajiriwa!

Hizi takwimu umezipata wapi????
Au unajifurahisha tu?
System ya nchi ikiwa mbovu, mambo mengine yanakuwa magumu sana.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom