Tujaribu kuangalia upande wa pili tunapowalaumu Polisi kila wanapotumia nguvu kuzuia mikutano ya hadhara na maandamano

DaudiAiko

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
302
274
Tunapo wapongeza polisi kwa jinsi walivyo chukulia ujio wa Tundu Lissu ni vyema pia kuwa pongeza watu wote waliojitokeza kwa wingi kwa ku zingatia utaratibu, ustaarabu na amani.

Misingi inayodumisha utulivu kwenye maandamano ya aina yoyote ambayo husemekana kuwa ya amani kwa kawaida ni migumu sana kuzingatiwa.

Vilevile, ni muhimu kufahamu kwamba kuna njia nyingi sana ambazo sio tishio kwa amani zinazo weza kutumiwa na viongozi wote kujenga hoja yoyote kwa wanaohusika katika mipango ya Serikali au wanaofanya maamuzi nyeti kwenye sekta yoyote serikalini.

Viongozi wote wanatakiwa wafahamu hatari iliyopo kwenye mikusanyiko mikubwa ya watu haswa kwenye hafla zenye hamasa kubwa kama siasa.

Muda wa kampeni uheshimike, muda wa kukubali matokeo ya uchaguzi wowote uheshimike na muda wa kuendelea na kazi ya kujenga nchi uheshimike.
 
Nawapongeza CHADEMA kwa maandamano ya amani. CCM na kitengo chake Cha roho mbaya kinachojiita Polisi, walitamani Sana CHADEMA wa misbehave ili wapate kuwatoa roho, lakini CHADEMA, as normal as usual, walikuwa wapole na walinda amani na Mali za Watanzania wengine kwa muda wote wa masaa matano walioandamana.
CCM chaliiiii
 
Back
Top Bottom