Tujaribu dhana ya kujiajiri kupitia kilimo kwa wahitimu wetu

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
12,835
2,000
Hello JF,

Msinicheke ila leo nimewaza kwa nini sisi wana JF tusijaribu hii nadharia inayosemwa kila siku watu wajiajiri kupitia kilimo?

Najua JF tulishawahi kuwa na kitu kama hiki ila ilikua kwa baadhi ya watu, sijui ilipata changamoto gani?

Graduates ni wengi sana.

Arable land ni kubwa tu Tanzania.

Ni jinsi tu ya ku combine the two.

Mimi ningependa kuona JF ikiongozwa na Maxence tununue mashamba,au tuiombe serikali watupe mashamba tuwa ajiri wahitimu.

Kilimo kitaajiri graduates kuanzia, sourcing, transportation, kulima, advertising, kote huku ni ajira tofauti tofauti.

At least tukishindwa kuwasaidia wahitimu wetu kupitia kilimo then tuna evidence kuwa kilimo hakina tija katika nchi yetu, tuangalie mengine, na wale motivation speakers waangalie mengine ya kusema, lol.

Niliona mahali zamani kidogo, sijui sasa hivi hali ikoje, ila in average graduates wa Tanzania (wale wasio na connection) wanaangia kwenye ajira rasmi ten (10) years after graduation. Miaka kumi ni mingi sana, mzigo kwa serikali na jamii.
 

STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
12,777
2,000
Jambo la msingi la kuishauri serikali ni kuanzisha mkakati kama wa USA, kule wana mashamba ya Serikali na huajiri wakulima kama vile zinavyoajiriwa kada mbali mbali mfano Walimu, afya n.k

Hii nadhani itasaidia kuinua kilimo, kutoa ajira kwa wingi maana Kilimo ni uwanda mpana sana,
Yani laiti kama hili wazo litafanyiwa kazi basi Uchumi utapanda na maisha ya watu wengi yataimarika.

NAWASILISHA.
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
21,208
2,000
Kwa utafiti uliousema inamaanisha natakiwa kusubiri miaka minne mbele.

Nje ya mada.

Rais atakayeingia na kufanya vipaumbele vyake kua kilimo, afya na elimu ndiye Rais atakayefanikiwa kuliko waliopita wa kipindi hichi.
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
21,208
2,000
Jambo la msingi la kuishauri serikali ni kuanzisha mkakati kama wa USA, kule wana mashamba ya Serikali na huajiri wakulima kama vile zinavyoajiriwa kada mbali mbali mfano Walimu, afya n.k...
Chief democratic states nyingi hujitenga kufanya biashara badala yake hua wanamiliki share. Hayo mashamba ya usa ni state owned kwa 100%?
 

Akilindogosana

JF-Expert Member
Jan 12, 2020
1,014
2,000
Wekezeni kwenye masoko. Hicho kilimo kitajiseti chenyewe.

Mfano: Viwanda vikubwa vya kuchakata nafaka kama mahindi kuwa unga/bia/chakula cha mifugo, viwanda vikubwa vya mafuta ya kula kutoka kwenye alizeti, viwanda vikubwa vya kuchakata nyanya kuwa tomato, viwanda vikubwa vya nguo sio mavitenge yaani viwanda vitengeneze, mashati, tisheti, magauni,mashuka mazuri, vitambaa vya suruali, madela, taiti, chupi, vitambaa vya suti ili kukuza pamba. Viwanda vikubwa vya sukari, viwanda vya kuchakata mazao jamii ya mikunde kama kile cha Morogoro n.k

Halafu viwanda viwe na msamaha wa kodi kwenye mitambo na kemikali za kuchakata mazao. Ardhi pia wapewe bure na wafatiliwe kwa kina wasije kuleta mambo ya kiwaki. Halafu mambo ya kutandika kodi/ushuru/tozo zinazotesa biashara na kuua mtaji waache kabisa ili hivyo viwanda vizalishe kwa gharama ndogo ili waweze kushindana kwa bei na bidhaa za kutoka nje ili wauze Hapa nchini, nchi jirani Sadc, EAC, DRC na afrika nzima.

Baaada ya hapo kilimo kitajiset chenyewe tu.
 

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
12,835
2,000
Wekezeni kwenye masoko. Hicho kilimo kitajiseti chenyewe.
Mfano: Viwanda vikubwa vya kuchakata nafaka kama mahindi kuwa unga/bia/chakula cha mifugo, viwanda vikubwa vya mafuta ya kula kutoka kwenye alizeti, viwanda vikubwa vya kuchakata nyanya kuwa tomato...
Waongeze viwanda kwa ajili ya kununua hizo products za kilimo na kuweka mazingira rafiki, sawa asante mkuu, ila hamjanijibu vipi wana JF wakichukua hili jukumu la kusaidia graduates kupitia kilimo, itakuwaje? lol
 

Akilindogosana

JF-Expert Member
Jan 12, 2020
1,014
2,000
Waongeze viwanda kwa ajili ya kununua hizo products za kilimo na kuweka mazingira rafiki, sawa asante mkuu, ila hamjanijibu vipi wana JF wakichukua hili jukumu la kusaidia graduates kupitia kilimo, itakuwaje? lol
Hilo kwa sasa halitawezekana labda kuanzia 2025 baada ya mkuu kutoka (kama ikitokea na upepo wa rais mpya wa 2025 atakuwaje) zaidi ya hapo changamoto ni mambo matatu:

1. Watu wasijulikana

2. Kama dili likitoa hela zoote zitasombwa na kodi au uhujumu uchumi.

3. Mswahili kwenye masuala ya hela sio mtu wa kumuamini. Mfano ni humuhumu Jf zamani hizo palikuwa na watu walisema watawekeza au wameshawekeza Pwani sijui waliishia wapi? Wamefikia kwenye hali gani? Ngoja niishie hapo nisijeonekana snichi.
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
21,208
2,000
Mkuu, mara hii umesahau tulikua na kilimo kwanza na mzee wa msoga + waziri mkuu wake alikua anajiita mtoto wa mkulima, how far did we go?
Nafikiri ishu nzima ilizungukwa na ufisadi pia chief.

Plus Kilimo Kwanza Initiative ilifanywa kama Initiatives nyingi za serikali, wanakutana wao kwa wao wanafikia maamuzi bila kuwashirikisha walio kwenye field halafu wanayaleta hayo maamuzi yatekelezwe na walio field.

Kiimo Kwanza ilikua ni kauli mbiu haikua kiashiria cha kwamba kilimo kimekua kipaumbele.
 

Malchiah

Senior Member
Feb 10, 2021
112
500
Asilimia zaidi ya 60% ya maisha ya Mtanzania yanategemea kilimo. Mimi sishauri ishu ya kutafuta eneo kwaajili ya kilimo bali eneo kwaajili ya kiwanda cha uchakataji wa mazao.

Mfano mikoa ya Kagera na Kilimanjaro zao kuu ni ndizi, lakini unakuta mkulima anapeleka bidhaa sokoni anakosa mteja wa kununua mkungu hata kwa buku, imagine?!

Huwa najiuliza hakuna mtu ameona fursa hata ya kuanzisha kiwanda cha wine ya ndizi nchini?

Hope tuanze na wazo la kuanzisha viwanda endelevu vyema uzalishaji makini kwa viwango vya kimataifa. Miaka ya 80 Arusha kulikuwa na kiwanda cha Tanelec, sijui hawa jamaa mpaka sasa ni washindani kimataifa?

Tanzania tuna resources nyingi, wataalam wakutosha, ardhi ndio usiseme, sijui tunakwama wapi?
 

Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,080
2,000
Mkuu, mara hii umesahau tulikua na kilimo kwanza na mzee wa msoga + waziri mkuu wake alikua anajiita mtoto wa mkulima, how far did we go?
Kilimo kwanza, Mapinduzi ya kijani, Big Results Now, e.t.c

Potelea pote, tuko Tz ya viwanda bila malighafi! Malighafi bila viwanda. Mazao ya mkakati pamba, mkonge, miwa e.t.c viwanda vyenyewe ni cherehani.😂

Everyday is Saturday............................ :cool:
 

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
12,835
2,000
Nimewaelewa wakuu ni viwanda then kilimo na sio opposite, hope wahusika wata take notes
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom